Kweli hata mie niliona anaongea na mie nilishasema mara nyingi, yule hafai kuwa pale hata ukimuona anaongea unajikuta unatamani hata kwenda kulala. Hizi kazi za kuongoza raia ni tofauti kabisa na jeshi na kwa vile alishakuwa mstaafu jamaa angemwacha tu akastaafu. Ukiona anavyoongea unaelewa ni kwanini stand hii pamoja na hatua ilikofikia inashindwa kuendelea.
Unajifikilia ingekuwa kwa mkuu wa mkoa wa Simiyu/Shinyanga hii stand ingekwama kweli, jibu ni hapana. Uwezo wa kuchambua na kushawishi huyu mzee hana, spirit ya kuona mambo yanakimbia kwa spidi hana ..mwisho wa siku, tuna mtizamaji tu.
Aliongea eti tumepewa soko, soko lenyewe liko wapi ..hata sielewi liko wapi labda mlioko hapo mtwambie kuna hatua gani kuhusu soko. Kila kitu kipo kwenye 0. Meli tumeambiwa iko kwenye 0, stand inarudi kwenye 0 yaani every project iko kwenye 0 not even nearing the commencement. Serikali ya mkoa iko hoi kuliko ajuza wa miaka 200