Happiness Essau
Senior Member
- Aug 9, 2016
- 166
- 100
Ndugu Alexism, si rukhsa kutukana tu mengine yote unaruhusiwaIli ni wazo zuri kwa maendeleo ya Mkoa na Manispaa.. Ushauri ni kwamba ruhusu mawazo huru au tofauti na mawazo yenu na kutoa nafasi kwa watu wote maana tumezoea mambo yakishindikana kwenda kwasababu ya kumuliki hoja na mawazo..
Mheshimiwa RAS
Kwa heshima na taadhima kwa niaba ya wananchi wako tunakuomba uutumie muda wako adhimu uwatembelee hawa Mabwana wakubwa wa Bukoba Water and Sanitation(BUWASA), na kuwauliza kwa nini hatupati maji?
TANESCO wasipotoa huduma hututangazia tuwe tayari! BUWASA ni wepesi kutuma bills kubwa kubwa kwetu bila kutoa huduma.
Mheshimiwa nikuambie kitu!
Tangu BUWASA wanifungie maji mwaka 1992 maji hayajawahi kukatika kwangu!
Tangu walipowaleta hawa Wahindi "eti" kuboresha huduma leo ni kilio kila nyumba.
Mheshimiwa nafahamu una majukumu mengi lakini BUWASA wamekuwa na kazi nyingi kukuzidi.
Naomba nirudie tena; Sisi tumekuwa watumishi wa BUWASA badala ya wao.
Kwa ufupi sasa mimi sipati maji na kama yatapatikaa saa kumi na moja alfajiri hadi saa mbili asubuhi. Nisielewe hawa malaika watateremshwa lini ili na wao waishi kama mashetani. Ni wepesi wa kuleta bills kubwa kuliko matumizi lakini bila kutoa wao kutoa huduma.
Wako boi wa BUWASA
Ramadhani Kingi
Ndugu Lind, hii ni mipango ya miezi tisa (9) ambayo ni vipaumbele vya mbunge. JF kazi yake ni kuhimiza utekelezaji wa ahadi hizi za mbunge kwa muda huo. Eneo letu la mradi ni Bukoba sio KageraYaani ili kulikwamua jimbo katika umaskini mnawaza stendi na kuwawezesha mama ntilie tu ,hapo lazima mkae tu,vp kuhusu ukusanyaji wa mapato yatokanayo na ziwa victoria?,kuwa na viwanda ili kupata ajira za uhakika,elimu juu ya kilimo cha mazao mchanganyiko maana kagera wanajua ndizi na kahawa tu wakati mkoa una mvua za kutosha na udongo mzuri kusaport mazao ya aina mbalimbali ya chakula na biashara?.Ki ukweli uwezeshaji wowote lazima uanzie kwenye akili za wawezeshwaji wenyewe -watu wa chini kabisa,lazma kuwepo na amsha amsha kwani watu wamekata tamaa ya maisha ukijumlisha na tetemeko ndo kabisa kila siku tunaona na kusikia kwenye vyombo vya habari.Vinginevyo mipango yenu itabakia kwenye makablasha yenu mwanzo mwisho na hakuna kitakachofanyika.
Dah wewe Dada hii nafasi hawakukosea kukupatia maana unajua mpaka basi. hongeraNdugu Lind, hii ni mipango ya miezi tisa (9) ambayo ni vipaumbele vya mbunge. JF kazi yake ni kuhimiza utekelezaji wa ahadi hizi za mbunge kwa muda huo. Eneo letu la mradi ni Bukoba sio Kagera
Tukiongelea maendeleo ya Kagera kila mwanakagera ana nafasi ya kuchangia maendeleo ya kwao awe ndani ya Kagera au nje ya Kagera. Watu wa nje ya Kagera tunawategemea zaidi kwamaana wengi wao wana mitaji wanaweza kuja kuwekeza kwao. Kama tunavyokuwa na ushawishi katika siasa na chaguzi tunatamani kuona pia ushawishi wao katika shughuli nyingine za maendeleo. Kama wanavyofatilia, fadhili kampeni na chaguzi vivyo hivyo tunawahitaji wafatilie na kufadhili shughuli nyingine za maendeleo
Hata hivyo km ulivyokwisha kusema, mipango ya uwekezaji inapasa kuwa ya kumwinu mtu wa chini. Soko tunalihitaji lkn tunahitaj zaidi viwanda, uwekezaji ktk kilimo n.k
Shukrani[emoji120]
Changamoto ya taarifa ni kubwa ndugu!Salaam ndugu zangu wana Tushirikishane.
Ni siku nyingine tena yenye kila dalili za kuwa na baraka zote za muumba wetu hivyo tuna kila sababu ya kumshukuru na kuomba rehema zake. Ni wiki moja sasa tangu niulize juu maendeleo ya utekelezaji miradi tajwa ndani ya mradi wa Tushirikishane lakini niseme tu bado tuna tatizo la kupata habari za mrejesho toka kwa viongozi wetu. kwa wale mliofatilia mjadala niliouanzisha ni dhairi mtakubaliana na mimi kuwa hakukuwa na majibu ya kujitosheleza ya kile nilichouliza kwa lengo la kupata ufafanuzi.
Nisiwe mbinafsi sana nimshukuru Mb. Mh. Lwakatare alitoa jibu japo kama tulivyowazoea hawa wanasiasa wetu majibu yao uwa ni yale ya juu juu lakini nimshukuru kwa ilo. ombi langu kwako mh. Mb. Lwakatare wana JF especially wale walio hapa Tushirikishane tungependa kupata ufafanuzi wa kina ni figisu figisu zipi zinazokwamisha kuanza kwa miradi hiyo ambayo tunatambua wazi haiko mikononi mwa serikali kama ili kama vip tuzihoji mamlaka za juu kwanini ziweke kiza kinene kwenye miradi hiyo? Mh. ukiweza kutuhabarisha ukwamishaji huko wapi tutaweza kukupa ushirikiano wa kuwauliza wenye mamlaka ili tuje na majibu muafaka maana ni wajibu wetu na ni haki yetu ya msingi kujua kinachojiri.
Jambo la pili linaloendelea kunisikitisha ni kwa jinsi viongozi wetu wasivyoona umuhimu wa kutumia mitandao ya kijamii nimejaribu kumtafuta Meya wa Manispaa maana yeye ndiye mwenye picha nzima ya miradi hii lakini kwa bahati mbaya bado simpati kokote Ndugu yangu chief Kalumuna katika ulimwengu huu wa utandawazi bado kweli usiwe mtumiaji wa Social Network? naomba mlio na bahati ya kukutana nae mwambieni kuwa yawezekana anayakosa mengi ya ulimwengu huu kwa kutokuwa kwenye Social media. Maana yeye ndo mtoa majibu mkuu sasa endapo hapati jumbe kama hizi dah ni dhairi tunatwanga maji kwenye kinu na maendeleo tunayoyapigania yatachukua muda kutufikia wana bukoba
Naibu Meya Ndugu Jimmy najua ni mtu active sana na kwa bahati ni mtumiaji mzuri wa mitandao lakini kimya chake kwenye masuala ya maendeleo ya bukoba kinanipa wasiwasi. maana namuona sana kuchangia kwenye masuala mengi yahusuyo uhai wa siasa na demokrasia ya Tanzania ila sio kutuhabarisha wana bukoba kwenye yale tuyatumainiayo kuyaona wana bukoba wenye fikra na mitazamo chanya kwa bukoba tuitakayo.
Ndugu yangu Jimmy. naomba nikupe mfano mdogo sana wa kiongozi ninayempenda katika nyanja za siasa na huyu si mwingine ni Mh. Nassari Mb. wa Arumeru. yuko active kwenye kila jambo na anajua namna ya kueleza umma wa wana arumeru juu ya kinachohitajika kufanyika au hatua zilizofikiwa. juhudi zake za kutoa mrejesho zinawapa nguvu wana arumeru kuchangia kwa hali na mali katika maendeleo yao.
nisiwachoshe kwa maneno mengi sana bali niseme wazi kuwa viongozi wetu vunjeni ukimya muwe watu wa kuzungumzia maendeleo msijiweke kimya maana kwa style hii ya ukimya mnaonekana kama hamko nasi. Wana bukoba tunapenda kusikia na kuona Bukoba ikipiga hatua ndani ya miaka hii minne kabla ya 2020, na hii itakuwa ni nafasi pekee kwenu kusimama mbele ya wanabukoba tena mkiwa vifua mbele kuwa tumefanya ili na linaonekana kuliko zile ahadi za miaka ya nyuma ambayo it was business as ussual
Muwe na siku njema
nimekupenda sana mheshimiwa kwakuwa karbu sana na mkuu wa mkoa na kushirikiana naye vizur ..napenda sana kuwa huru na kiongozi mwngne sio mambo ya kutunishiana misur kila mtu anajiona yupo juuView attachment 404994 LEO NIMEWASILISHA RIPOTI YA KIKAO NILICHOKIFANYA NA BAADHI YA WANA KAGERA WAISHIO JIJINI DAR ES SALAAM KWA MKUU WA MKOA KAGERA.
View attachment 405000 View attachment 405001 View attachment 405002 View attachment 405003 View attachment 405003 View attachment 405003 View attachment 405004
MH. MKUU WA MKOA,
KAGERA.
MAAZIMIO YALIYOPITISHWA KWENYE KIKAO KILICHOITISHWA NA MH. WILFRED LWAKARATE(MB), MBUNGE WA JIMBO LA BUKOBA MJINI, KUJADILI ATHARI ZA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA, KUONA JINSI YA KUSAIDIA WALIOPATWA NA MADHARA.TAREHE 18 SEPTEMBA, 2016 KWENYE HOTELI YA KEBBY'S, MWENGE, DAR ES SALAAM.
1. Kwa kauli moja kikao kimetambua na kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua zakuridhisha kufuatia janga hili, ikiwa ni pamoja na ;
i. Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa, (Mb), Waziri Mkuu, pamoja na kiongozi mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mh. Freeman Aikael Mbowe (Mb) kufika B ukoba mara moja kuona athari za tetemeko na kushiriki mazishi ya watu waliofariki kutokana na janga hili na pia kuwafariji waliojeruiwa na kuathirika kwa namna mbali mbali.
ii. Kuandaa mkutano wa kuishirikisha jumuiya ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na jumuiya ya wafanyabiashara kwa lengo la kukusanya misaada kwa ajili ya kukabiliana na janga hili.
iii. K uandaa matembezi ya hisani kwa ajili ya kukusanya fedha za kusaidia nakukabiliana na madhara ya janga hili.
iv. Viongozi waandamizi mbali mbali waserikali, wakiwemo Mawaziri, Viongozi mbalimbali wa kisiasa, Makatibu wakuu na wakuu wa vitengo muhimu vinavyo husiana na maafa kufika kwenye eneo la tukio kwa haraka.
2. Kwa kauli moja kumuomba Mh. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa ndiye baba wa nchi, pamoja na shughuli zake nyingi, kutenga siku mapema itakavyo mpendeza kufika mkoani Kagera kuwapa pole wananchi wake kutokana na janga hili. Tunaamini walioathirika watafarijika sana kumuona Rais wao akiwa nao kwenye eneo la tukio.
4. Kwa kuwa janga hili la kitaifa halina itikadi ya siasa, dini, rangi, kabila wala ubaguzi wa aina yoyote ile, hivyo ushiriki wa watu wote ni muhimu sana.
5. Kwa kutambua ukweli wa walioathirika zaidi ni wananchi wa mkoa wa Kagera, inawapasa wao kuwa msitari wa mbele katika kushiriki katika juhudi zote zinazofanyika, kwa njia na jinsi yoyote inayowezekana, iwe ni kwa hali au mali, mshikamano wao katika janga hili ni muhimu sana. Mpaka sasa, imejidhihirisha kwamba ushiriki wa wana Kagera bado ni hafifu sana. Wana kagera wanahimizwa kutokukata tamaa nakuamsha hari ya kushirikiana katika kuusaidia mkoa wao kwa nidhamu ya hali ya juu . Ili kusisitiza umuhimu huo, mfano wa kwamba ili kuweza kupewa msaada wa usafiri (lift) ni lazima uwe njiani, unahusika.
6. Kwamba kutokana na mkoa wa Kagera kukumbwa na maafa makubwa na mengi mfululizo kuanzia miaka ya 1970 zilipoanza chokochoko za nduli Iddi Amini wa Uganda, vita vya Uganda , Ukimwi, mdudu wa migomba (ekiuka), madhara ya wakimbizi kutoka nchi jirani yaliyo leta ujambazi , kufa kwa Vyama vya Msingi vya Ushirika na Chama Kikuu cha Ushirika (BCU/ KCU) kulikoambatana na kuanguka kwa bei ya zao la kahawa, kuanguka kwa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kulikosababisha bei za bidhaa za viwandani ambavyo vingi vipo Dar es salaam, kuwa juu kuliko sehemu nyingine yoyote ya Tanzania, ugonjwa wa mnyauko ambao umeangamiza kabisa migomba na zao lake ndizi, na sasa ni janga la tetemeko. Majanga hayo yote ni sababu kubwa kwa mkoa wa kagera kushuka sana kiuchumi kutoka kati ya mikoa mitatu tajiri miaka ya 70 - 80 hadi kuwa kati ya mikoa mitano masikini sana nchini. Serikali inaombwa ichukue hatua za makusudi kutoa upendeleo wa kisera wa kuusisimua upya uchumi (a stimulus package) kwa mkoa wa Kagera kwa kufanya yafuatayo :
i. Kutoa msamaa wa kodi zote kwenye bidhaa zote za ujenzi zinazouzwa mkoani Kagera kwa kipindi cha miaka kumi.
ii. K wa kutambua madhara ya mdororo wa uchumi wa mkoa wa Kagera kwa muda mrefu hivyo kuwepo tatizo kubwa la ajira na umasikini, miradi yote ya ujenzi wa miundombinu ya kijamii kama mashule, zahanati, vituo vya afya na majengo mengine ya serikali yatakayo jengwa upya au kukarabatiwa, ugawaji wa kandarasi ufanywe kwa mtindo wa uwezeshaji kwa makampuni yaliyopo na yanayoendesha shughuli zao mkoani kagera yenye uwezo, wakishirikiana na makampuni ya wana -Kagera walioko nje ya mkoa pale inapobidi . Vigezo vitaandaliwa ili vizingatiwe.
7. Kwa kutambua kuwa serikali imeunda kamati za maafa za Kitaifa na Mkoa ambapo Wabunge wa mkoa wa Kagera wameshirikishwa, ni vyema ushiriki kwenye kamati hizo upanuliwe na kuzijumuisha taasisi za dini ambazo mkoani kagera zimekuwa na mchango mkubwa katika utoaji wa huduma za jamii kwa miaka mingi. Hatua hii itasaidia kuongeza ufanisi katika zoezi zima la uthamini wa madhara, ukusanyaji wa taarifa na usambazaji wake. Aidha kwenye hizo kamati uwepo umuhimuwa ku wahusisha wataalam wa habari kuongeza ufanisi katika upashanaji wa habari .
8. Kwa kuzingatia mamlaka ya Mbunge anayopewa na katiba ya jamhuri ya Muungano wa T anzania, mifuko ya majimbo pia itumike kusaidia kwenye majanga yamaafa kama haya.
9. Kwa kukubali kwamba bado uitikiaji na ushiriki wa wana -Kagera bado ni hafifu sana, juhudi mpya zifanyike kwa kuishirikisha Serikali ya mkoa wa Kagera, Wabunge wote wa mkoa na viongozi wa dini zote kuitisha mkutano/ kusanyiko jingine haraka iwezekanavyo hapa dar es salaam kwa lengo la kuwashirikisha wana-Kagera na wadau wengine wote wenye mapenzi mema, katika kuonyesha kuguswa kwetu kama jamii na tatizo hili, tukusanye rasilimali kusaidia kwenye janga hili. Ndiyo njia pekee ya kuonyesha kuwa tunahitaji kupatiwa msaada wa usafiri (lift), hivyo ni vyema tukawa njiani.
NB : Katika kikao hicho cha wana kagera ahadi za jumla ya Tshs. 6,780,000/= zilitolewa na pesa taslimu Tshs. 1,480,000/= na kuleta jumla ya Tshs. 8,260,000/=
Sekretarieti iliyoundwa inaendelea kuratibu ukusanyaji wa michango hiyo ili itakapokamilika iwasilishwe sehemu husika.
Imewasilishwa leo tarehe 22/09/2016
Ofisi ya mkuu wa mkoa.
Wilfred Muganyizi Lwakatare (Mb)
Jimbo la Bukoba Mjini.
K. N.Y Wana Kagera wanaoishi Dar es Salaam (Waliohudhuria kikao hicho).
NAKALA KWA;
Mh. Waziri Mkuu.
Viongozi wakuu wa madhehebu ya kidini.
Viongozi wa vyama vya siasa.
Waheshimiwa wabunge wote wa mkoa Kagera.
Waandishi wa Habari.
Shukran sana kaka SangaPoleni sana wana bukoba kwa maafa mliyoyapata naimani mungu atawatia nguvu na kusimama upya na kuendelea na mipango yenu, naimani mungu yupo pamoja nanyi na sisi tunawaombea