TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni

Kigamboni hapafai au sehemu ya barabara ndo haifai?
 
Daraja la Kigamboni litaleta madhara makubwa sana it's just the matter of time tutaishia kulia kwa kuwapoteza ndugu zetu. Daraja limeelemea upande mmoja . Kwa ufupi 'Lililipuliwa'
Mhhh,kwa hili kesho mahakamani lazima wambane melo mahakamani
 
Tunaomba tume maalum iundwe ifanye uchunguzi wa ubora wa hili daraja.
 
Daudi A. Bashite aka P. Makonda... Aliahidi angeijenga, sijui utekelezaji utaanza lini....!! Kweli kipande hicho ni kero kubwa....
 
Hivi mleta uzi hukuona umuhimu hata wa kuweka picha kidogo ili tushuhudie?
 
Ndio maana mm huwa silipi hela kwenye vibanda vyao!!! Sio barabara tu hata Huduma pale kwenye vibanda n mbovu!! Wamama wamezeeka,,wakaka mandevu kama cjui nn?? Wanaacha kuweka tudada tuvutie wateja wanaleta blaa blaaa
 
Daraja la Kigamboni litaleta madhara makubwa sana it's just the matter of time tutaishia kulia kwa kuwapoteza ndugu zetu. Daraja limeelemea upande mmoja . Kwa ufupi 'Lililipuliwa'
Una uthibitisho?
 
Daraja la Kigamboni litaleta madhara makubwa sana it's just the matter of time tutaishia kulia kwa kuwapoteza ndugu zetu. Daraja limeelemea upande mmoja . Kwa ufupi 'Lililipuliwa'
Nitarudi nikapime
 
Dr F. Ndugulile tunaomba uje utoe ufafanuzi. Kuishi kigamboni na kufanyakazi upande wa mjini kwa mmiliki wa gari inakugharimu 3000/- per day. Gharama hii ni nje ya gharama nyingine yoyote.

Bado ili ulipe hio 3000/- inabidi kupita sehemu ambayo inaharibu kabisa gari lako. Mimi nimehamia huko miezi kama 7 iliopita, gari langu lilikuwa kama jipya, ndani ya miezi mitatu halifai kabisa! Nikabadili vikorokoro vyote vinavyohusiana na matairi ila sasa hivi tena halifai kabisa.

Hivi huwa unapita hii njia? Inawezekana unapita na VX kwahio huwezi kuhisi ubovu wa hii barabara. Ni aibu kipande cha 1.2km sasa hivi kinakaribia mwaka kinatusumbua. Daraja limegharimu 200bn lakini kipande ambacho gharama yake haiwezi kuzidi 2bn kinakuwa kibovu na kichafu hivi.

Hatuwezi kufanya kitu chochote kwa ukamilifu?
 


Nakumbuka siku ya ufunguzi wa daraja tuliambiwa mwezi mmoja tu ile bara bara itakuwa na lami.
 
Hongera sana mkuu kwa kuwakumbusha ,nimependa sana hyo chorus kuhusu uwanja wa taifa.
 
Hii barabara ya mwasonga kibada kimbiji ni kibwa sana. Inahitaji ijengwe kwa lami ili ifungue fursa.
Barabara ya Kibada-Mwasonga ipo kwenye mpango wa kujengwa kwa kiwango cha lami. Kwa mwaka ujao wa fedha upembuzi yakinifu unaendelea.
Natambua kuwa barabara hii imeharibika sana katika kipindi hiki cha mvua. Tayari nimeshawajulisha Tanroads kuikagua na kuchukua hatua za dharura. Matenngenezo makubwa yatafanyika baada ya mvua kukatika.
 
Pia barabara za Kisota ni mbaya sana. Toka zichongwe hazijawahi kufanyiwa ukarabati. Halmashauri tunaomba mtuangalie.

Nadhani Kisota ni katika maeneo ya kigamboni lililosahaulika sana. Au labda kisota iko chini ya wilaya nyengine na Sio Kigamboni ?

Kuna juhudi zinaendelea za kutaka kukarabati barabara za Kisota kwa ushirikiano kati ya wakazi wa Kisota ba Halmashauri.
Kama ni mkazi wa eneo na hauko kwenye mtandao wa wakazi wa Kisota. Ni-inbox jina na namba yako ili uweze kuunganishwa na kupata taarifa ya kinachoendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…