TARIFA FUPI YA MWEZI NOVEMBA 2016 KUHUSU MAENDELEO YA MRADI WA TUSHIRIKIANE KATIKA JIMBO LA NZEGA MJINI
A) ukamilishaji wa ujenzi wa kituo kipya cha mabasi Nzega
Kazi ambayo inaendelea kwa sasa ni uchimbaji wa kisima, kisima kimekwisha chimbwa tayali, hatua iliyobakia kwa sasa nikufunga pampu, ili kisima kianze kufanya kazi, vile vile mchakato wa kutangaza washindi wa zabuni ajili ya ujenzi wa vibanda vya biashara unaendelea na mda wowote kuanzia sasa washindi watatangazwa ili waweze kuanza ujenzi wa mabanda ya biashara.
B) Ujenzi wa nyumba ya Daktari katika kituo cha afya Nhobola
mradi huu kwa sasa upo katika hatua ya upauaji wa jengo, hii ilikuwa ni hatua inayofuatia baada ya ujenzi wa boma ukiwa umekwisha kamilika, kama tarifa picha ya maendeleo ya mpango kazi huu inavyoonyesha, kwaiyo hatua iliyopo sasa na inayosubiliwa ni upauaji wa jengo hilo, kamati ya ujenzi pamoja na uongozi wa kijiji ulishakaa na kujadili makadirio ya pesa inayoitajika kwa ajiri ya kazi ya upauaji wakakubaliana hivyo basi mda wowote kuanzia sasa kazi ya upauaji inaanza.
C) Kukamilisha mpango wa muda mfupi wa upatikanaji wa Maji safi na salama-Nzega kwa kuongeza mita za ujazo 1300
Hatua iliyopo sasa ni majaribio na urekebishaji wa miundombinu ya maji, ikiwa ni mabomba, matanki kazi inayofanyika ili kuweza kuangalia ufanisi unaokuwepo baada ya kazi ya ukamilishaji wa matengenezo ya machujio mawili ya maji kukamilika, vile vile uongezaji wa mashine mbili za kumpampu maji kuongezewa, na kuwa mashine tatu, zitakazo fanya kazi kwa pamoja
tofauti na awali ambapo chujio lilikuwa moja na mashine iliyokuwa ikifanya kazi ya kupampu maji ilikuwa moja, vile vile baadhi ya matanki ya maji yalikuwa hayafanyi kazi, hivyo sasa zoezi lililopo ni kukarabati miundombinu hiyo ya maji ili zoezi la majaribio liweze kuendelea na kuendelea kukarabati maeneo ambayo ya taonekana bado yana tatizo ili badae zoezi likamilike na wakati wa nzega waweze kupata maji kwa uhakika zaidi.
D) Kukamilisha mabweni na madarasa ya kidato cha 5&6-Sekondari ya Bulunde
Mradi huu kwa sasa umesimama hii ikiwa ni hatua ya awali ya ukamilishaji wa kuinua jengo kukamilika , hivyo hatua inayosubiliwa kwa sasa ni upauaji wa mabweni hayo ambayo ujenzi wake wa boma umekamilika kama habari picha za maendeleo ya mpango kazi huu zinavyoonyesha.
hivyo basi wahusika wa ujenzi kwa sasa wapo katika zoezi la kuanza kazi ya upauaji wa mabweni hayo, kwaiyo kazi ya upauaji ikianza tutakuja wapatia mrejesho wa maendeleo hayo.
Imetolewa
Afisa mawasiliano Nzega.