Mjadala wa Wachangiaji M1 JF Jukwaa la Historia 2013

Mjadala wa Wachangiaji M1 JF Jukwaa la Historia 2013

Mzee Mohamed Said acha kumuondoa Mwl Nyerere kwenye orodha ya waasisi wa Tanu.

Pascal Mayalla

Nguruvi3
Proved,
Naam Mwalimu kaikuta TANU nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Aggrey na Sikukuu mwaka wa 1952.

Mimi siwezi kumtoa Nyerere kwenye orodha ya waasisi wa TANU kwani kadi yake ni no. 1, kadi ya TANU Territorial President.

Kadi no. 2 ni ya Ally Sykes na kadi no. 3 ni ya Abdul Sykes.

Hivi ndivyo nilivyoandika historia ya Nyerere katika kitabu cha Abdul Sykes (1998).

Historia ya kadi za TANU na namba za kadi za wanachama wake iliwashangaza wengi kwani nilieleza historia zao pia.

Iddi Faiz kadi yake no. 24 na ya ndugu yake Iddi Tosiri ni no. 25.

Denis Phombeah kutoka Nyasaland kadi no. 5 na Dome Okochi Budohi kutoka Kenya no. 6.

Hawa ni viongozi wa TANU kama walivyokuwa viongozi African Association.
 
Labda tulikuwa tukipishana mzee wangu, nilishachungulia humu mara kadhaa kuona kama kuna madini mapya uliyoyaweka ila sikubahatika kukutana nayo. Nilifikiri labda uko "busy" unaandika kitabu, n.k.

Ila shukran sana kufahamu kuwa bado unaendelea kuwekeza humu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Nitazifuatilia. Kuna mapya najifunza kupitia mada zako.
Gold...

View: https://youtu.be/bgiP_SI0-vI?si=Hb9-lfZK2qvQagSX
 
Back
Top Bottom