Peaky...
Kitabu cha Abdul Sykes si historia ya upande mmoja.
Kuna historia ya wazalendo wengi waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Wazalendo hawa huwasomi popote katika vitabu vilivyotangulia ila katika kitabu cha Abdul Sykes.
Unaweza ikiwa kitabu unacho ukaangalia Faharasa (Index) utakuta majina yao.
Mimi naongelea historia ya uhuru wa Tanganyika kuanzia 1924 Dr. Kwegyr Aggrey alipokutana na Kleist Sykes na Dr. Aggrey akamshauri Kleist kuasisi African Association.
Sikuanza historia ya uhuru katika miaka ya 1950.
Wengine waliokuwapo wakati huo nimewataja mfano Martin Kayamba, Erica Fiah, Ali Jumbe Kiro, Juma Mwindadi kwa kuwataja wachache.
Mimi naijua historia ya kweli kwa sababu nimeiandika na hakuna mtafiti mwingine aliyeipinga kwa kuja na kitabu chenye historia inayopingana na historia niliyoandika.
Kitabu sasa kina umri wa miaka 25.
Lakini kubwa hii ni historia ya watu ambao wengi wao mimi niliwafahamu udogoni kwangu.
View attachment 2972736
Juma Mwindadi Mwalimu Mkuu wa shule ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika
Mwafrika wa Kwanza Mjumbe katika Bodi ya Dar es Salaam Municipal Council
Mwafrika wa pili ni Kleist Sykes
View attachment 2972739
Erica Fiah
Mwafrika wa kwanza kuwa na gazeti ''Kwetu.''