Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #41
Shadow...Nilipata muda wa kupitia machapisho yote hakika kila mtu alifanya kwa nafasi yake. Hongereni sana
Ahsante sana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Shadow...Nilipata muda wa kupitia machapisho yote hakika kila mtu alifanya kwa nafasi yake. Hongereni sana
Machapisho yako mengi unawa-define waislam wenzako kama vile ndio watu pekee walihusika kwenye uhuru. Article zako nyingi unajivuna sana kutaka kuonyesha umuhimu wako katik jamii na usomi wako.Peaky...
Nashukuru naheshimika.
Wala sijaandika Uislam ambao wewe unataja dini.
Hili nimelieleza mara nyingi hapa na kwa ushahidi nikionyesha vitabu vyangu nilivyoandika na kuchapwa ns wachapaji wakubwa ulimwenguni kama Oxford University Press.
Nimepokea tuzo kadhaa kwa uandishi wangu.
Nimealikwa kuzungumza na kutoa mada kwenye vyuo vingi: University of Johannesburg, Kenyatta University, University of Ibadan, University of Iowa, Northwestern University nk.
Ikitokea niko katika mji na jamaa wakajua niko mjini kwao hawakosi kunikaribisha hata kwa kikombe cha chai.
Huku ndiyo kukosa heshima?
Peaky...Machapisho yako mengi unawa-define waislam wenzako kama vile ndio watu pekee walihusika kwenye uhuru. Article zako nyingi unajivuna sana kutaka kuonyesha umuhimu wako katik jamii na usomi wako.
Hata kwenye hii comment yako umerudia yaleyale, Ego
Hujanielewa. Sikatai wewe kuandika historia, weka balance kwenye machapisho yako. Uhuru haukupambaniwa na waisalamu pekee. Kuna michango mingi ya watu wengine pia nje ya uislam.Peaky...
Umesema kweli.
Hakika wazee wangu wamefanya makubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika kuanzia enzi ya Wajerumani.
Naamini unaijua historia ya Nduna Abdulrauf Songea Mbano katika Vita Vya Maji Maji, historia ya Khadija Mkomanile kwa kuwataja wachache.
Wanahistoria walioandika historia ya Maji Maji hawakupenda kuandika majina yao halisi ya ''Abdulrauf'' na ''Khadija.''
Khadija Mkomanile kabla hajanyongwa alipewa jina jipya ''Yasintha.''
Naamini unalijua kaburi la halaiki walipozikwa majemadari 67 walionyongwa na Wajerumani Songea wengi wa majemadari hawa ni Wasilam na aliletwa Fr. Yohanned Haffliger kutoka Peramiho kuja kuwabatiza kabla ya kunyongwa na akawapa majina ya Kikristo.
Naamini unaijua historia ya Hassan Omari Makunganya, Abushiri bin Salim Al Harith na Mtwa Abdallah Mkwawa.
Kuhusu ''ego,'' ikiwa unanina hivyo ni bahati mbaya wanaonijua vizuri wao ndiyo wanaweza kusema.
Historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika nayo inafuata mkondo huo:
Waasisi wa African Association 1929: Cecil Matola (President), Kleist Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ali Said, Mpima, Zibe Kidasi, Suleiman Majisu, Raikes Kussi na Watson Watts.
(Seminar Paper ya Aisha ''Daisy'' Sykes, East Africana, Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, ''The Life of Kleist Sykes'' Ref. No. JAN/HIST/143/15 (1968).
TAA Political Subcommitee 1950: Dr. Vedasto Kyaruzi (President), Abdulwahid Sykes (Secretary), Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Hamza Mwapachu, Steven Mhando na John Rupia.
TAA Executive 1953: J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President; J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias and Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer, Ally K. Sykes Assistant Treasurer.
Committee members Dr. Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z. James, Dome Okochi, C. Ongalo and Patrick Aoko.[1]
[1] Tanganyika Standard, 19 th June 1953.
Unadhani nimefanya vibaya kuandika historia hii?
Na kama Waislam ndiyo waliohusika hairuhusiwi kuandika historia yao?
Peaky...Mohamed Said
Sijakufahamia tu hapa JF. Nakufahamu toka uko University of wales mwaka 1992.
Nimesoma vitabu vyako vingi, na articles mbali mbali, nimesikiliza interview zako.
Nilichokigundua kwako, una elimu nzuri na uelewa wa historia. Lakini unalazimisha kuwa portray waisalamu kama watu pekee waliopambania uhuru, kama watu pekee wanaostahili pongezi.
Peaky...Hujanielewa. Sikatai wewe kuandika historia, weka balance kwenye amchapisho yako. Uhuru haukupambaniwa na waisalamu pekee. Kuna michango mingi ya watu wenvine pia nje ya uislam.
Ukitaka kuandika historia kama nguri wa historia, usijikite kuongelea watu wa dini yako tu. Andika historia kwa kutabua michango wote walioshiriki. Vingunevyo andika machapisho ya Kiislamu tu.
Nitakuelewa zaidi ukijikita kuongelea Uislamu pekee kuliko kujaribu kupindisha mambo ili kui favor dini yako. Eg Islam and politics in Tz presented (1989) Al haq international karachi.
Sawa ndugu. Nakuheshimu sana, nimefatikia publication zako nyingi tu. Nimekiona hicho nilichosema. Ukiondoa udini ukabalance mambo, una uelewa mzuri.Peaky...
Mbona historia niliyoandika nimewataja wote waliopigania uhuru wa Tanganyika?
Umesoma kitabu cha Abdul Sykes?
Pitia Name Index usoma majina.
Ndugu Wawili Katika Historia ya Kupigania Uhuru wa Tanganyika: Steven Mhando na Peter Mhando
NDUGU WAWILI KATIKA HISTORIA YA TANU: STEVEN MHANDO NA PETER MHANDO Imenichukua muda mrefu sana kuitafuta na kupata picha ya Steven Mhando na mdogo wake Peter. Niliipata picha ya Peter Mhando na baadae picha ya Steven Mhando kaka yake. Hawa ndugu wawili ni kati ya wazalendo waliounda TANU na...www.jamiiforums.com
Nakushauri tu jikite kwenye dini.Peaky...
Nalazimisha vipi ilhali mimi sina nguvu yoyote.
Historia imeandikwa na inasomeshwa na wazee wangu hawamo katika historia hiyo.
Ningekuwa na nguvu ya kulazimisha si ingesomeshwa historia niliyoandika katika kitabu cha Abdul Sykes?
Peaky....Sawa ndugu. Nakuheshimu sana, nimefatikia publication zako nyingi tu. Nimekiona hicho nilichosema. Ukiondoa udini ukabalance mambo, una uelewa mzuri.
Wasio waislam umewaongela kwa uchache tu. Kuwataja sio tatizo, content iliyowahusu haiendani na content unayowapa waislamu.
Yeye alikuwa anajenga HOJA ya wazee wangu DAR na wengineo.. na uislamu hakuna mwenye akili anayeweza kubaliana nae.Uzuri wa @Yerricko Nyerere alikua anajenga hoja katika mtazamo wa maslahi mapana ya umoja wa kitaifa
Nina imani Unaelewa ninachokisema. Udini basi, sina shida na historia unayotoa, ila usiingize udini.Peaky....
Ikiwa una taarifa ambazo unaona mimi sikuziweka nakuomba ziweke hapa tuzisome.
Lakini nashangaa hujasema lolote kwa nini historia ya kweli ya uhuru ilifutwa ikapachikwaa ya uongo.
Leo nimeweka historia ya kweli baadhi yenu mnateseka.
Hivi kweli mnatamani haya yote niliyoeleza kama vile yasingeandikwa?
Peaky....Nakushauri tu jikite kwenye dini.
Inside10,Yeye alikuwa anajenga HOJA ya wazee wangu DAR na wengineo.. na uislamu hakuna mwenye akili anayeweza kubaliana nae.
Peaky...Nina imani Unaelewa ninachokisema. Udini basi, sina shida na historia unayotoa, ila usiingize udini.
Binafsi Nimesema nakufahamu vizuri, na publications zako nimesoma sana.Peaky....
Sina elimu ya dini.
Na ndiyo maana leo kalamu tangu inasomwa katika Dictionary of African Biography mradi wa Harvard na Oxford University Press New York.
Nasomwa ndani ya Cambridge Journal of African History.
Nimezungumza Northwestern University, Chicago chuo kinachoongoza katika historia ya Afrika nk.
Nimetajwa kuwa na maktaba kubwa yenye historia ya Julius Nyerere nk.
Nimekutana na mabingwa wasomi wa African Studies.
Nashukuru leo hujahangaika kuweka picha na hizo nishani..Inside10,
Kutokubaliana na mimi si tatizo.
Nimepokea nishani kutoka taasisi za kuheshimika na nimealikwa vyuo vikuu kadhaa kuzungumza.
Unaukataaje udini wakati machapisho yako yote yamejaa udini?Peaky...
Nami nakujibu kuwa ningekuwa naandika dini leo nisingekuwa katika orodha ya wataalamu wa historia ya Afrika Library of Congress, BBC, VoA na kwengineko.
Nina imani unaelewa ninachokisema.
Peaky...Binafsi Nimesema nakufahamu vizuri, na publications zako nimesoma sana.
Nisichokubaliana na wewe ni kuendekeza udini. Kwa historia una uelewa mpana nakubali. Shida udini, udini, udini.