Nipe ushahidi wa kimaandiko kuhusu hiyo comment yake.
- Maana yangu ni kwamba kama alisema umendika kweli, hiyo pekee ingekupa nguvu zaidi ya kufanikisha lengo lako la kuandika hiyo historia.
- Halafu usingekaa kimya, hiyo kauli yake ingekusukuma na kukupa nguvu ya kutaka historia ya kwanza ifutwe na kufundishwa hii yako, maana mmoja wa wahusika kathibitisha kuwa ya kwanza imedanganya.
- Hao hanao ku-challenge mpaka leo kuhusu huo uongo, ungewashinda kirahisi sana kwa kuwaonyesha kauli ya Nyerere, ambayo lazima ingekuwa imeandikwa popote pale nje ya maneno yako.
Nyerere hakuwa na chuki dhidi ya uislamu bali baadhi ya watu ambao baadhi yao walikuwa ni waislamu. Sio UISLAMU wao uliofanya afarakane nao. Kama angekuwa na chuki na uislam, vipi kina
Tumbo, C. K, KaselaBantu, J, Kambona, O walikuwa waislam?
Nakuhakikishia, uliwasikiliza hao unaowaita wazee wako baada ya kuwa wametofautiana na Nyerere. Hiyo tu inatosha kuonyesha sumu na chuki uliyolishwa na wewe ulipopata nafasi ya kuandika ukaamua ufanye revenge kwa kumchafua Nyerere. Ndio maana unajibu kinafiki hapo eti unaogopa kuandika utamvunjia heshima. Ni heshima gani uliyombakishia baada ya kuandika hicho kitabu chako ambayo leo unaogopa kumvunjia?
Kuhusu harakati za uhuru historia zimeanza mwaka 1884 baada ya mkutano wa Berlin. Historia ya uhuru haijaanza na kina Sykes wala na waislamu. Kabla ya Nyerere na Sykes kuzaliwa walikuwepo Watanganyika ambao waliukataa utawala wa kigeni katika jamii zao.
- Kama akina Sykes walikuwa na fedha, wasomi nk. mbona hakuna hata mmoja wao alie enda UNO kudai uhuru wa Tanganyika badala yake akaenda Nyerere?
Nyerere aliweza kuaminika kwao haraka hivyo kwa sababu ya uwezo wake wa elimu na uwezo mkubwa wa kujenga hoja kitu ambacho hao kina Sykes hawakuwa nacho.
Lastly, usipende sana kujibu hoja kwa kutaka watu wakasome kwanza mawazo yako kwenye kitabu cha Sykes. Hicho kitabu ndicho kinachohojiwa usahihi wake, kwa nini utake tena kikasomwe kama reference? Unapotaka kukitumia hicho kitabu kama proof kwa hoja zako, wakati hicho kitabu umekiandika wewe, ni sawa kusema "There are only two rules one, the boss is always right and two if the boss is wrong look rule one" .
Peaky...
Umeandika maneno mengi lakini nitajaribu kukueleza niliyonayo kwa hayo uliyoeleza.
Mwalimu hakunyanyua kalamu kusema lolote kuhusu kitabu cha Abdul Sykes kwa hiyo hakuna ushahidi wa maandishi hata kama kweli alizungumza na Prof. Haroub Othman na mpashaji wangu mwengine ambae habari zake bado sijakupa.
Lakini elewa kuwa hayo hapo juu nikuelezayo yametokea kitabu kishachapwa.
Mimi sijataka historia ya zamani ifutwe.
Nataka iwepo sana kwani historia hiyo ndiyo inayisadikisha ukweli wa yaliyomo katika kitabu cha Abdul Sykes.
Unasema kuna wanao kipinga kitabu changu.
Kitabu kinapingwa na kitabu na kitabu hakiandikwi ila baada ya utafiti.
Hili halijafanyika.
Hata kitabu cha Mwalimu Nyerere kilichoandikwa na Prof. Shivji at al. hakijaweza kujibu kitabu changu wala kutumia nyaraka na picha adimu nilizowapa za Mwalimu wakati wa kudai uhuru.
Nimeeleza kwa kirefu kuhusu uhusiano wa Nyerere na Waislam baada ya uhuru.
Wako wanaisema hii ndiyo moyo wa kitabu.
Ningemdogosha Nyerere au kumvunjia heshima ningekiua kitabu changu na kisingefikia kuchapwa mara nne.
Nimemweleza Mwalimu kwa namna ambayo msomaji kila akisoma anajiuliza maswali na anajifunza yale ambayo hakupata kuyajua.
Hakuna mahali popote wazee wangu walipotofautiana na Nyerere si Abdul Sykes si Dossa Aziz wala si babu yangu Salum Abdallah.
Historia zao nimeziandika na zinafahamika.
Ni kweli baada ya Berlin Conference 1884 ndipo Wajerumani wakapigana na Abushiri bin Salim, Mtwa Abdallah Mkwawa, Hassan Omari Makunganya, Nduna Abdulrauf Songea Mbano Mangi Meli kwa kuwataja viongozi wachache.
Nashukuru umelileta hili la safari ya Nyerere UNO.
Uliwaka moto hapa JF kiasi cha miaka 10 iliyopita nilipoeleza kuwq hotuba ya Mwalimu Nyerere iliandikwa mwaka wa 1950 na TAA Political Subcommittee kutokana na mapendekezo ya katiba kwa Gavana Edward Francis Twining.
Na mtu aliyesaidia sana kuandika mapendekezo haya alikuwa Earle Seaton Mshauri wa TAA katika mambo ya Mandate Territory.
Seaton alimfahamisha Abdul Sykes zamani sana kuwa kama TAA inataka kupiga hatua ya maana ni lazima ianzishe mazungumzo na UNO si na Gavana.
Mipango hii ikaanza mara moja.
Hii ni historia ndefu siwezi kuieleza yote hapa ila nitakueleza kuwa mipango yote na mikakati ya Tanganyika kuzungumza UNO ilianza Nyerere hajawa kiongozi wa TAA pale New Street, Dar es Salaam.
Wala hakuna aliyemfikiria Nyerere katika mipango hii.
Lakini ni wazi kuwa atakaekwenda UNO atakuwa kiongozi wa TANU.
Uwezo wa Mwalimu Nyerere hakuna wa kuupinga lakini ni nani waliokuwa nyuma yake?
Bila kusoma kitabu cha Abdul Sykes utaijuaje historia ya Julius Nyerere?