Watu wamepewa mitaa hadi barabara hao wengine watoto wao wamekuwa na wadhifa mkubwa hapa Tanzania ! ni nini ambacho hawajakumbukwa?
Nyiokunda,
Nazingumzia historia ya uhuru wa Tanganyika kama ilivyohifadhiwa.
Sizungumzi kuhusu kurejesha hisani wala majina ya mitaa mfano Mtaa wa Bibi Titi Mohamed.
Nimesoma kama undergraduate Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam Political Science na kulikuwa na kozi ikisomeshwa: Government and Politics in East Africa.
Katika kozi hii tulikuwa tunafundishwa historia ya nationalist politics Kenya, Uganda na Tanganyika na Zanzibar.
Mwalimu alikuwa wakisomesha historia ya TANU na kumtaja Nyerere peke yake.
Sikupata kumsikia akimtaja Abdul Sykes na wazalendo wengine hata siku moja.
Katika semina za somo hili ndipo mwalimu wangu aliponipenda sana kwani nilikuwa nikichangamsha mijadala kwa kuibomoa historia tuliyosomeshwa darasani.
Mwalimu akinisikiliza na kunitia moyo nieleze ninayoyajua na hasa nilipoeleza kuwa African Association imeasisiwa na babu zangu.
Siku hiyo darasa zima liliangua kicheko.
Mwisho wa siku niliyecheka nilikuwa mimi na wanafunzi wenzangu wakawa wameduwaa.
Mwalimu wangu huyu Mashaallah akinipa alama za juu.
Kozi nyingine ambayo mwalimu alinipenda ni The Rising of the Working Class tukifunzww siasa za watu wa tabaka la chini walivyopigania haki zao duniani kote.
Fikiria ndani ya semina mwalimu ananipa nafasi ya kueleza historia ya babu yangu Salum Abdallah mwanachama wa African Association Dar-es-Salaam kuanzia 1929 na Tabora kuanzia 1948 alipoongoza migomo mitatu ya wafanyakazi (General Strike) 1947, 1949 na 1960.
Migomo yote hii ipo katika historia ya Tanganyika lakini hakuna popote jina la babu yangu limetajwa katika vitabu vya rejea tulivyokuwa tukisoma.
Mwalimu wangu huyu na yeye alinipenda na akipenda kuniita kwa majina yangu matatu: Mohamed Said Salum.
Kisa ni kirefu.
Ndipo nilipoamua kuandika kitabu na nilianza utafiti katika Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam nikiwa mwanafunzi.
Mswada wa kitabu changu ulisomwa kwa mara ya kwanza na walimu wangu wa historia Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam.
Napenda kusema kuwa baadhi walitumia katika paper zao katika journals na vitabu waliyosoma na kujifunza kutoka mswada wangu.
Bahati mbaya hakuna aliyefanya "acknowledgement" kwangu.
The rest is history.