Mji mdogo wa Himo usipopewa hadhi ya Halmashauri chini ya Rais Samia wananchi watamkumbuka sana Hayati Magufuli

Kibosho1

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2017
Posts
2,621
Reaction score
4,293
Kupitia mgombea wa ubunge wa Vunjo Dkt. Charles Kimei aliahidi kuishawishi serikali iweze kuufanya mji mdogo wa Himo kuwa halmashauri ili kupanua mji huo unaokuwa kwa kasi na pia itafanya maendeleo kuja kwa haraka sana sababu baadhi ya huduma wananchi wanalazimika kwenda mpaka Moshi (manispaa).

Hayati Magufuli katika kampeni zake alipita eneo hilo na kuahidi kutekeleza wazo hilo kama wananchi watampa Kimei kura.

Nakumbushia tu mama Rais Samia anasema atafamya yale yale ya mtangulizi wake je ataupa hadhi mji huo?
 
Msimpangie vya kufanya, Wala hayupo pale kutekeleza ahadi za mwenda zake,tumuache afanye kazi tutamuhukumu baada ya awamu Yake,Cha muhimu timizeni vigezo hadhi hazipandishwi Kama zawadi Kama alivokuwa anafanya mwenda zake akiamua Leo ilala iwe jiji inakuwa,
 
Naunga mkono hoja. Himo inakidhi masharti ya kuwa Halmashauri.Wakazi wengi wanalazimika kwenda Moshi kupata huduma za kiofisi hii inaongeza gharama na kupoteza muda wa kufanya kazi za kimaendeleo.
 
Kupitia mgombea wa ubunge wa Vunjo Dkt. Charles Kimei aliahidi kuishawishi serikali iweze kuufanya mji mdogo wa Himo kuwa halmashauri ili kupanua mji huo unaokuwa kwa kasi na pia itafanya maendeleo kuja kwa haraka sana sababu baadhi ya huduma wananchi wanalazimika kwenda mpaka Moshi (manispaa)...
Hakiki taarifa zako. Mji wa Himo uko "HALIMASHAURI" ya Moshi. Ni kweli ofisi za Halimashauri zipo mbali sana na mji mdogo wa Himo na pia zipo sehemu isiyo ya Kimkakati. [ilipokuwa sekondari ya Kolila].

Sijajua ni huduma zipi unazozungumzia kuwa wanalazimika kuzipata "MANISPAA". Hakuna uhusiano wowote wa mji wa Himo na Manispaa ya Moshi. Ni maeneo ya wilaya mbili tofauti kabisa.
 
Halimashauri zipo mbali sana na mji mdogo wa Himo na pia zipo sehemu isiyo ya Kimkakati
Sasa yeye alishauri zihamishiwe Himo na kuifanya halmashauri ili baadhi ya huduma ziwe karibu na pia ni mji unaokuwa kwa kasi,kabla haujaanza kuvurugika uanze kupangwa sasa
 
Mnamblackmail SASHA kwa kutishia kumkumbuka magufuli???!
 
Hakiki taarifa zako. Mji wa Himo uko "HALIMASHAURI" ya Moshi. Ni kweli ofisi za Halimashauri zipo mbali sana na mji mdogo wa Himo na pia zipo sehemu isiyo ya Kimkakati. [ilipokuwa sekondari ya Kolila].

Sijajua ni huduma zipi unazozungumzia kuwa wanalazimika kuzipata "MANISPAA". Hakuna uhusiano wowote wa mji wa Himo na Manispaa ya Moshi. Ni maeneo ya wilaya mbili tofauti kabisa.
Mkuu hamna wilaya mbili ipo wilaya ya Moshi tu ila ipo halmashauri ya Moshi vijijini na halmashauri ya manispaa ya Moshi mjini.
 
Hebu nitajie wilaya zinazopatikana mkoa wa Kilimanjaro. MANISPAA ya Moshi ni wilaya inayojitegemea na HALMASHAURI ya Moshi ni wilaya ingine kabisa. Niko Himo
 
Kupitia mgombea wa ubunge wa Vunjo Dkt. Charles Kimei aliahidi kuishawishi serikali iweze kuufanya mji mdogo wa Himo kuwa halmashauri ili kupanua mji huo unaokuwa kwa kasi na pia itafanya maendeleo kuja kwa haraka sana sababu baadhi ya huduma wananchi wanalazimika kwenda mpaka Moshi (manispaa).

Hayati Magufuli katika kampeni zake alipita eneo hilo na kuahidi kutekeleza wazo hilo kama wananchi watampa Kimei kura.

Nakumbushia tu mama Rais Samia anasema atafamya yale yale ya mtangulizi wake je ataupa hadhi mji huo?
Kila Rais na zama zake mkuu.Na inawezakana hata yeye asingeipa Himo hadhi ya Halimashauri,mbona ni kamji kadogo!
 
Mkuu tayari ni mji mdogo wa Himo.Unadhani unaweza kuipa nyama kidogo hoja yako ili ueleweke
 
Sheria za Halmashauri zinasemaje kuhusu kuunda Miji hiyo
Himo inakosa sifa kwa kukosa ardhi, wenyeji wamemiliki ardhi yote na hawatakubali kuitoa kwa serikali.
Labda Kibosho 1 afafanue suala la ardhi, pale pembeni tu yule Shayo wa Scolastica alinunua maeneo mpaka kwa kibabe na kuna jamaa ana kiwanja hapo jirani kamgomea kumuuzia Shayo mpaka leo bado akanunua viwanja kumzunguka ili kumfungia na km asingeenda ndani!!
tuyaache Himo bado
 
Hebu nitajie wilaya zinazopatikana mkoa wa Kilimanjaro. MANISPAA ya Moshi ni wilaya inayojitegemea na HALMASHAURI ya Moshi ni wilaya ingine kabisa. Niko Himo
Nitajie mkuu wilaya Moshi vijijini mkuu. Wilaya za kili ni siha, rombo, hai, mwanga, same, Na moshi
 
🤔
 
Kupitia mgombea wa ubunge wa Vunjo Dkt. Charles Kimei aliahidi kuishawishi serikali iweze kuufanya mji mdogo wa Himo kuwa halmashauri ili kupanua mji huo unaokuwa kwa kasi na pia itafanya maendeleo kuja kwa haraka sana sababu baadhi ya huduma wananchi wanalazimika kwenda mpaka Moshi (manispaa).

Hayati Magufuli katika kampeni zake alipita eneo hilo na kuahidi kutekeleza wazo hilo kama wananchi watampa Kimei kura.

Nakumbushia tu mama Rais Samia anasema atafamya yale yale ya mtangulizi wake je ataupa hadhi mji huo?
Sasa ni zamu ya kuendelea visiwani sio bara
 
Nitajie mkuu wilaya Moshi vijijini mkuu. Wilaya za kili ni siha, rombo, hai, mwanga, same, Na moshi
Moshi Manispaa, Moshi DC (vijijini), Hai, Siha, Rombo, Mwanga na Same. Kilimanjaro kuna wilaya 7. Moshi vijijini ni wilaya yenye majimbo ya uchaguzi ya Moshi Vijijini na Vunjo ilihali Moshi mjini ni jimbo linalojitegemea. Ofisi za wilaya ya Moshi vijijini zilikuwa KDC na sasa zimehamia ilipokuwa Shule ya Kolila. Ofizi za manispaa zipo jirani na jengo la KCC (Kilimanjaro Commercial Complex)
Na kama Moshi ingekuwa wilaya moja basi ingekuwa imeshakuwa jiji zamani kabla ya Tanga au Mbeya. Changamoto ya udogo wa eneo ndio imefanya isiwe jiji hadi sasa. Mazungumzo yanaendelea kati ya wilaya zote mbili ili sehemu ya Moshi DC ihamishiwe Manispaa. Na hata kuondoa ofisi KDC huenda ni sehemu ya mpango huo kwani eneo litamegwa hadi Kiborloni.
 
Back
Top Bottom