Tetesi: Mji Mkuu wa Irani Umeshambuliwa vibaya sana na vikosi vya US na Israel

Tetesi: Mji Mkuu wa Irani Umeshambuliwa vibaya sana na vikosi vya US na Israel

Troll JF

Platinum Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
10,592
Reaction score
15,404
Vyanzo vyangu kutoka Iran vinaripoti kuwa kumetokea milipuko mikubwa nchini humo.

Video zinazoonyesha milipuko karibu na kituo kikubwa cha makombora nje kidogo ya mji wa Isfahan zimethibitishwa.

Kitengo cha BBC Verify kimechambua video tatu zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwemo moja inayoonyesha moshi mzito na mabaki ya moto yakipaa angani karibu na kituo cha makombora cha kusini mwa Isfahan.

Katika moja ya video hizo, mwanaume aliyekuwa akirekodi anasikika akielezea mshangao wake baada ya kusikia mlipuko huo.

Wakati huo huo, video nyingine inaonyesha moto mkubwa karibu na uwanja wa ndege kufuatia mashambulizi yaliyoripotiwa katika mji wa Mashhad ulioko kaskazini mashariki mwa Iran.

Video hiyo, ambayo pia imethibitishwa, ilirekodiwa asubuhi ya leo kutoka ndani ya gari lililokuwa likipita karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mashhad.

Uthibitisho wa eneo ulifanyika kwa kulinganisha alama za barabarani na mazingira yanayoonekana kwenye video na picha za ramani za eneo hilo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran, inaelezwa kuwa hifadhi kubwa za mafuta pamoja na maghala huenda zilikuwa miongoni mwa malengo ya mashambulizi hayo.

Uwanja huo wa ndege pia unahusishwa na moja ya vituo vya jeshi la anga la Iran, ingawa bado haijathibitishwa rasmi ni sehemu gani hasa zimeathirika kutokana na video hizo.
 
vyanzo vyangu kutoka Irani vinaniambia kuwa Irani imelipuliwa
Kwahiyo? Kwani imeanza jana kulipuliwa? Is it news? Objective ilikua kung'oa utawala kama milipuko hata Iran inalipua kila siku ndege, viwanda, radar, na miji kibao tu middle east.

Nadhani yote hii ni deflection baada ya aibu ya hii wiki iliyopita..
 
Iran itaenda kugeuzwa gofu iwe kama Somalia, baadae waje kuanza kujenga nchi upya, hizi vita za siku hizi namna zinqvyoanza na muendelezo wake mtu mpaka unashangaa.

Nikitazama kule Urusi v Ukraine, vita iliyoanza kama utani leo ina mwaka wa tatu, na bado inaendelea tu hata mwisho wake hauonekani karibuni.

Hii ni dalili baadhi ya mataifa ulimwenguni yameshachoka mazungumzo kama njia za kumaliza misunderstanding, now wameamua kila mmoja aoneshe nguvu zake kijeshi.
 
Israhell nayo itakuaje
Au anaepigwa ni iran pekee Israhell ndio wateule wanalindwa na mungu wao 😁
 
@Reviser
@Boqin
@Zenora
@Cookie

Vipi habari iliyokua verified na BBC nyi Mnaweka tetesi? Au mpaka mtukaniwe mama Zenu?

Ukishatukana unapata faida gani???
 
Back
Top Bottom