Papa Mopao
JF-Expert Member
- Oct 7, 2009
- 4,153
- 2,647
Leo ngoja nije na mada ya aina yake, kuna huu mji unaitwa YAKUTSK / YAKUTIA, huu mji unapatikana Siberia nchini Russia/Urusi ya Mheshimiwa Vladmir Putin.
Maajabu ya huu mji kwa upande wa hali ya hewa baridi yake inacheza kwenye -71°C, -96°F na wakati mwingine unapungua kidogo ila baridi yake bado ni kali kwa kiasi chake. Ukirusha maji ya moto hewani sekunde kadhaa yale maji yanaganda haraka sana na kuwa kama barafu au snow fulani hivi, mito karibu sehemu zote maji yake yameganda yamekuwa barafu, magari hayazimwi kuyafanya engine isigande, asilimia kubwa ya wenye magari huwa wanajaza mafuta full tank ya kuwasaidia kuzifanya engine za magari yao iendelee kuunguruma kuzuia barafu ndani ya engine.
Wakaazi wake wakiwa nje kwa maana ya nje ya majengo lazima waufanye miili yao ijishughulishe kuupata joto mwili, ukitulia tu waweza pata madhara kiafya na wakati mwingine unaweza kusababisha hata kifo, wengi wao huvaa makoti hadi matano na suruali mbili au tatu mazito mazito, soksi matatu au manne viatu vizito vyenge ngozi isiyoweza kupitisha baridi, ajabu sana. Kila mahali barafu tupu, mitaani, mimea barafu, waya umeshika barafu, ukitoa ndizi na kuuacha nje kwa dakika mbili tayari umekuwa barafu na unaweza kuutumia kama nyundo kabisa kuupigilia msumari, nyama yoyote iwe mbichi au uliopikwa ukiuacha nje kwa dakika kadhaa barafu tupu.
Sokoni buchani nyama zinauzwa nje kabisa na kila aina ya nyama kuanzia nyama ya ng'ombe sijui samaki na kadhalika huuzwa nje na nyama karibu zote zimeganda, wauzaji wanasema kipindi hiki cha baridi kali haijawahi kutoka nyama kuoza na unaweza kuuza kwa muda mrefu na hupati hasara ya bidhaa zako sokoni.
Hii dunia kuna mambo mengi sana ya kustaajabisha, tuendelee kujifunza maajabu ya NATURE duniani!