Mjomba anawachukia watoto wangu?

Pole sana !
Hapo shida ni kipato tu Mwenyezi Mungu akubariki upate kipato na kwako kwa mara nyingine, mjomba/shangazi/cousin watawapaenda wewe na familia yako

Mtu kitu !
 
Inategemea na mazingira mkuu! Huenda jamaa huko atakoenda itamlazimu kuishi mazingira yenye utata hasa kwa mwanamke! Mfano kwenye madini au kwenye zege ambapo anaweza kujikuta analala site kwenye mahema ambapo wanaume wamejaa!
Aende na mkewe nae mkewe ataungana na wamama wengine wa huko mgodini na kwenye kubeba zege kwenye kazi za kutoa huduma Kwa wafanyakazi Kama chakula, vinjwaji, sigara, sweets na mahitaji mengi tu ya binaadam.

Wakati umefika wa watu kutambua hizi sio nyakati za lelemama!!

Family inajengwa uimara wake Kwa ushirikiano wa wote baba na mama.

Siafiki Kwa family kutengana kisa changamoto za kiuchumi Kwa maana nafasi hiyo Ndio hutumika kuvunja family na pia hii umjengea picha mbaya mwenza wako Kwa kuona kwamba wewe baba/mzazi umeshindwa majukumu yako mpaka uyatelekezee Kwa wazazi wa mwenza wako.

Kiapo cha “katika shida na raha” ni muhimu sana kikaelezewa umuhimu wake na maana yake halisi Kwa kila wanandoa wapya na wale wanandoa wakongwe wakumbushwe kila mwaka kuhusu hicho kiapo.
 
Usukumani mama hana urithi kwao. Kwa ufupi huyo mwamba hapo alipo anafugwa kwa bibi yake maana hapo siyo kwao! Hapo ni kwenye makazi ya mjomba wake maana ndiye mrithi wa hapo!
Duh,kwa maoni yangu, mila mbovu hii.
 
Huu ni ukweli mchungu watu wengi wasiotaka kuukubali.

Mjomba kama nae elimu hana ni lazima atajenga chuki kwako na kwa wanao kwa sababu anawaza inawezekana umerudi kujiandalia mazingira ya kujichotea vya urithi.
 
Nyie huwa mkifanikiwa mna maneno sana, ohoo tuliteswa, tulinyanyaswa. Wewe Ulirudisha mpira golini kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi, ukaona ni sawa kabisa.

Mjomba wako unaweza kuta naye ana matatizo yake na hana pa kuyapeleka. Na mtu kuwa kimya au serious haina maana kwamaba anamchukia mtu yeyote, achilia mbali wanao. Kuna watu wako kimya wanatafakari, ila wewe unaanza kuji hisi kwa sababu uko kwake au kwao.

Tizama kila mtu ana handle shida zake tofauti, mpo nyie mnao lia lia na wapo watu wako kimya kimya kivyao vyao.
Acha kujihisi utagombana na watu bila sababu.

Hujawahi kuongea na huyo mjomba wako akakwambia anawachukia wanao, au wewe na mkeo. lakini unahisi tu anawachukia wanao.

Nakwambia siku ukiwa na kwako nyie ndio huwa mnaanza kulipiza visasi hata bila kuelewa unamlipizia nani, yani mis directed hunger.

Acha fikra hasi, ongea na watu kwanza ndio uwe na conclusion ya mawazo yako.
 
Ndio maana mseven alisema mtu mpumbavu, mvivu ni ngumu kuishi nchi zilizoendelea, lazima utakufa tu, lkn kwa africa waweza kuishi kwa vizinga maishani yako yote.
 
Pole mzee.... mwanaume kushindwa kulinda familia yake ni stress kubwa sana
 
Sina ujuzi ila kazi yoyote naweza Fanya ikiwa sijui ukinipa maelekezo nafanya
Mkuu sikupangii cha kujibu lakini, hili jibu ni jepesi sana kwa mtu alie kwenye hali kama yako.

Hii inaleta tafsiri kuaa hiyo hali unayopitia pengine wewe ndo sababu...huwezi niambia una mke na watoto eti huna ujuzi wowote.

Mwanzo ulikua unafanya kazi gani? Jieleze mkuu watu wanataka kukusaidia, halafu wewe unasema sina ujuzi wowote. Kweli?

Jiongeze hapo kamanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…