Habari Wadau
Nimekuwa nikimfatilia huyu jamaa anayeitwa Mwarabu Fighter a.k.a body guard wa Chibu dangote bin laden platnumz.
Sasa katika kumwangalia kwangu namuona jamaa kweli ni mkakamavu na amekomaa kweli. Lakini najiuliza maswali kadhaa,
1. Je huyu jamaa ana mafunzo yoyote ya kijeshi?
2. Je anaruhusiwa kumpiga mtu pindi akimsogelea diamond?
3. Je ukimsogelea diamond atakufanya nini?
4. Je sheria inamruhusu kumpiga mtu atakayemsogelea Diamond platnumz??
5. Je anajua kutumia silaha?
6. Je pale alipo ana silaha yoyote?
Na je ametoa wapi utaalamu wa kuwa body guard? Maana kuwa mzinzi binafsi sio kazi rahisi kwani unatakiwa kupata mafunzo maalum nchi mbalimbali au pia kwenye majeshi vikosi maalum..
Mwenye kumjua huyu jamaa naomba taarifa zake tafadhali. Bila kisahau elimu yake na wasifu kwa ujumla (CV)
ASANTENI