Mjue gwiji wa sheria nchini Dkt. Lamwai

Kwa sababu janabi ni wa dini yako? Jinga sana wewe
 
Hakika ila ilikuwa kivumbi haikuwa rahis kumjua Nani atashinda kwa kipindi kile?

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
kwenye kampeni za Hiza kulikuwa na mzee mmoja aliyeitwa sheikh Mtopea, huyu mzee aliichachafya CCM Jimbo la Temeke lilikuwa liende CUF. Mzee huyo alijipatia umaarufu na kuibua msamiati wa neno 'mpiga debe' kwenye uchaguzi mkuu wa 2000. CUF walianzisha msamiati wa neno 'ngangari' wakilitumia kama hamasa kwa vijana kuwaunga mkono katika kuwapa kura. Utasikia viongozi wa CUF wakisalimia mkutano ile salamu yao ya Haki,,, haki sawa, ikisindikizwa na neno 'ngangari' vijana wanaitikia 'ngangari kinoma' IGP wa wakati huo akaona isiwe taabu kama wao ni ngangari basi wao (polisi) ni 'ngunguri' aliwajibu CUF. Huo msemo uliwatetemesha sana polisi wakidhani vijana wa CUF watafanya fujo katika mikutano ya kampeni, jimbo la Temeke ndilo lilikuwa na joto la juu kwa uchaguzi
 
Mjomba walipambana nae mpka mwisho aka fail kabisa nikamkuta mwananyamala kisiwani katulia Kwa bimdogo
Any way alikuwa Genius sana kwenye sheria enzi hizo
R I P bro still we love you
 
Ila sijui wanatumia uchawi gani mbwembwe nying ila ikawa holaa

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Natamani kujua miaka yako na wadhifa wako Tz
 
Ila sijui wanatumia uchawi gani mbwembwe nying ila ikawa holaa

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
kipindi hicho mrema alikuwa anagombea urais mwaka 2000 kupitia TLP ya Leo Leokamwa kama mwenyeki wa chama hicho. Kampeni za mrema mwaka huo zilipoa sana. CUF walikuwa moto sana. Joseph Selasini ndio kwanza alikuwa anagombea ubunge Kinondoni kwa tiketi ya NCCR Mageuzi iliyopoteza umaarufu uchaguzi mkuu wa mwaka huo. Akina Masumbuko Lamwai, Ringo Tenga, Ndimara Tegambwega na wanamageuzi wengine ndiyo majina yaliyoshika hatamu katika upinzani hasa ule uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa 1995
 

Acha za kuambiwa wewe, najua unapsta redio mbao za vijiweni! Sisi tuliosoma sheria kabla hata ya Lamwai tunajua wababe wa sheria, na hakuna PhD ya miaka miwili popote duniania hata ungeenda Afghanistan! Watu wasomi waliomo humu wanapiuona upupu uliouandika humu wanaona kama hata darasa la nne tu hukufika!
 
Mabere Marando yuko wapi?
Maradhi yanamsumbua sana kwa sasa

Tumuombee tahfeef kwa Mola

huyu ndio alikabidhiwa 'ukili' wa kusuka kikapu cha huu Upinzani tunaoushuhudia Tanzania nwishoni mwa miaka ya 1980s na akaifanya kazi hii kwa uzalendo mkubwa sana

Mabere Nyaucho Marando na Kingunge Ngombale Mwiru hawa watu wanatakiwa pale Makao makuu ya Ccm Dodoma na ofisi Ndogo ya Lumumba yawekwe masanamu yao makubwa sana kuwaenzi

Balozi Juma Mwapachu wakati anaondoka CCM 2015 baada ya kukasirishwa kukatwa kwa Lowassa akisema 'Kingunge ' ndio hirizi ya Ccm ya Miaka yote

Yaaani uchawi ule wa Kingunge wa kizalendo sana hadi alipotaka kushiriki kuitoa Ccm 2015 alishindwa yaani ni sawa na fundi aliekaza bawaba za mlango hata akashindwa kuja kuitoa siku alipohitaji kuung'oa Mlango ule ule
 
Mkuu sisi wabongo tuna wivu Sana hatupendi kuambiwa ukweli kwa miaka Ile hasa kwa wabongo jamaa alikuwa gwiji Nani angemuweza? Nani asiyetaka kumsikiliza akipinga hoja na kujenga hoja ? Mwanasheria yupi alikuwa ataki kuwa kama yeye?

Kwani wabongo hatupendani?

Kwani yeye ni WA Kwanza kusoma kwa miaka miwili?

Mbona wapo na wazungu wengi Tu...

Mkuu stuka

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…