Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Hii sio chit-chat wala chai. Ni habari ya ukweli. Kuna mtekaji mahiri duniani anayewateka watu kwa urahisi kabisa bila vitisho wala silaha. Mtekaji huyu ameteka mamilioni ya watu, wazee kwa vijana, maskini kwa matajiri, na hata wasomi wenye PhDs. Ajabu ni kwamba anaowateka hawalii, wanacheka tu na kushangilia. Wanaharakati wa haki za binadamu hawathubutu kumlaani. Wanauchumi wanamsifia. Wanadai akiwateka watu wengi, mapato yanaongezeka na uchumi unakua!
Ajabu kubwa zaidi ni kwamba anaingia hadi madhabahuni na kuwateka waumini makanisani. Lakini mapadre hawamkemei, na wao wanamkumbatia na kumtetea kwa vifungu! Wengine wanamwalika kwenye sherehe za arusi, lakini huwezi kusikia anayepaza sauti na kusema: "Mtoeni mtekaji huyo, mfukuzeni." Wanamwacha tu anakaa nao mpaka mwisho wa sherehe; na wengine wanapiga naye "selfie" kwa furaha!
Mtekaji huyu si mwingine bali ni chupa yenye kileo! Hii inaitwa pia pombe, divai, bia, gongo, ulanzi, mbege na majina mengine mengi. Si unakubaliana nami sasa kwamba mtekaji huyu hatumii bunduki wala pingu? Si unajua jinsi alivyowateka mamilioni ya watu duniani? Ameteka akili. Ameteka familia. Ameteka mataifa. Huenda hata wewe amekuteka lakini hujui. Je, mtekaji huyu analeta athari katika jamii? Jibu ni NDIYO.
Athari kuu za mtekaji kileo:
Kama umetekwa na mtekaji huyu, huwezi kujinasua kwa nguvu zako. Waganga hawawezi kukusaidia. Na hata ukikusanya watu muandamane kumpinga, ni bure tu. Sana sana mtapigwa buti na walinda amani.
Kama unatamani kuachana na mtekaji huyo, leo nakupa njia rahisi ya kumshinda. Ni rahisi sana kuliko unavyofikiri. Ukiifanyia kazi sasa hivi utakuwa huru kweli kweli.
Maandiko yanasema “Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.” (Yohana 8:36). Ni Yesu tu ndiye anayeweza kukuweka huru kweli kweli mbali na ulevi. Ufanyeje sasa ili uachane na vifungo vya ulevi? Tafadhali endelea kusoma...

- Anapofusha fikra: Mlevi hufanya maamuzi mabaya akiwa ofisini; na akiwa barabarani anasababisha ajali nyingi.
- Anaharibu afya: Magonjwa ya ini, moyo, akili, na hata kansa huambatana na ulevi.
- Anavunja familia: Talaka, mapigano, na manyanyaso mengi huanzia kwenye "kilauri"
- Anafungua mlango wa dhambi nyingi: Ulevi unazaa uzinzi na uasherati, mauaji, na kutokuwa na hofu ya Mungu.
- Mbaya zaidi anawapeleka watu katika moto wa milele. Biblia inasema wazi kuwa walevi hawataurithi ufalme wa Mungu (1 Wakorintho 6:10).