Juzi kuna Uzi ulikuwa unatamba hapa. Swali lilikuwa linauliza Nyinyi mnaomwamini Mungu mna kitu gani cha kujivunia?Hii sio chit-chat wala chai. Ni habari ya ukweli. Kuna mtekaji mahiri duniani anayewateka watu kwa urahisi kabisa bila vitisho wala silaha. Mtekaji huyu ameteka mamilioni ya watu, wazee kwa vijana, maskini kwa matajiri, na hata wasomi wenye PhDs. Ajabu ni kwamba anaowateka hawalii, wanacheka tu na kushangilia. Wanaharakati wa haki za binadamu hawathubutu kumlaani. Wanauchumi wanamsifia. Wanadai akiwateka watu wengi, mapato yanaongezeka na uchumi unakua!
Ajabu kubwa zaidi ni kwamba anaingia hadi madhabahuni na kuwateka waumini makanisani. Lakini mapadre hawamkemei, na wao wanamkumbatia na kumtetea kwa vifungu! Wengine wanamwalika kwenye sherehe za arusi, lakini huwezi kusikia anayepaza sauti na kusema, "Mtoeni mtekaji huyo, mfukuzeni." Wanamwacha tu anakaa nao mpaka mwisho wa sherehe; na wengine wanapiga naye "selfie" kwa furaha!
Mtekaji huyu si mwingine bali ni chupa yenye kileo! Hii inaitwa pia pombe, divai, bia, gongo, ulanzi, mbege na majina mengine mengi. Si unakubaliana nami sasa kwamba mtekaji huyu hatumii bunduki wala pingu? Si unajua jinsi alivyowateka mamilioni ya watu duniani? Ameteka akili. Ameteka familia. Ameteka mataifa. Huenda hata wewe amekuteka lakini hujui. Je, mtekaji huyu analeta athari katika jamii? Jibu ni NDIYO.
Athari kuu za mtekaji kileo:
- Anapofusha fikra: Mlevi hufanya maamuzi mabaya akiwa ofisini; na akiwa barabarani anasababisha ajali nyingi.
- Anaharibu afya: Magonjwa ya ini, moyo, akili, na hata kansa huambatana na ulevi.
- Anavunja familia: Talaka, mapigano, na manyanyaso mengi huanzia kwenye "kilauri"
- Anafungua mlango wa dhambi nyingi: Ulevi unazaa uzinzi na uasherati, mauaji, na kutokuwa na hofu ya Mungu.
- Mbaya zaidi anawapeleka watu katika moto wa milele. Biblia inasema wazi kuwa walevi hawataurithi ufalme wa Mungu (1 Wakorintho 6:10).
Kama umetekwa na mtekaji huyu, huwezi kujinasua kwa nguvu zako. Waganga hawawezi kukusaidia. Na hata ukikusanya watu muandamane kumpinga, ni bure tu. Sana sana mtapigwa buti na walinda amani.
Kama unatamani kuachana na mtekaji huyo, leo nakupa njia rahisi ya kumshinda. Ni rahisi sana kuliko unavyofikiri. Ukiifanyia kazi sasa hivi utakuwa huru kweli kweli.
Maandiko yanasema “Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli.” (Yohana 8:36). Ni Yesu tu ndiye anayeweza kukuweka huru kwelikweli mbali na ulevi. Ufanyeje sasa ili uachane na vifungo vya ulevi? Tafadhali endelea kusoma...
Tafakari haya maandiko utapata jibu la swali hilo... Kama hayaeleweki sema hujaelewa niniJuzi kuna Uzi ulikuwa unatamba hapa. Swali lilikuwa linauliza Nyinyi mnaomwamini Mungu mna kitu gani cha kujivunia?
Asante Mangwea1900 kwa kusoma. Nisaidie kueneza ujumbe huu kwa wote waliotekwa na ulevi, wajue njia ya kuwa huru.
Asante Mangwea1900 kwa kusoma. Nisaidie kueneza ujumbe huu kwa wote waliotekwa na ulevi, wajue njia ya kuwa huru.
Unachokiandika hata hukijui. "Si Kila anayekunywa pombe ni mlevi" huo mstari unaoutaja kwenye biblia unasema "mlevi" wala hausemi "mnywaji".Kama tulivyoona, ulevi ni dhambi. Walevi hawataurithi ufalme wa Mungu (1 Kor 6:9-11). Hivyo tubu dhambi hiyo ya ulevi na umkiri Yesu kuwa ni Bwana awezaye kukuokoa na kukuweka huru mbali na dhambi. Fanya hivyo sasa umuache mtekaji huyo kabla hajakupeleka kaburini au kwenye hukumu ya milele. Ulevi sio starehe, ni pingu zisizoonekana. Ni sumu inayoua polepole. Hivyo usiwe miongoni mwao wanywao kileo. Ukiomba sala hii ya toba, utaokoka sasa hivi na kupata nguvu ya kushinda ulevi. Omba hivi:
“Ee Mungu Baba, nimetambua mimi ni mwenye dhambi. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi hii ya ulevi na dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana na Mwokozi wa ulimwengu. Yesu Kristo karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda ulevi na dhambi zote. Niwezeshe kushinda vishawishi vyote vya ulevi. Niwezeshe kuishi maisha matakatifu kuanzia leo. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa na kuniweka huru mbali na ulevi. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen.”
Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Nguvu na neema ya kushinda ulevi tayari imeingia ndani yako. Uambie ulevi: "bye-bye!" Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuishi maisha ya utakatifu. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu, ujiunge nalo, watakupa msaada zaidi wa jinsi ya kuendelea kiroho.
Mungu akutunze na kukufunika kwa ulinzi wake. Washuhudie walevi kuwa Yesu amekuokoa na amekuwezesha kuacha ulevi. Mungu akubariki sasa na hata milele. Amina.
Kwendraaa, kwani kuna faida gani ukifa ukiwa na ini zima? Ama Figo nzima? Kila mtu atakufa vile ilivyopangwaKama tulivyoona, ulevi ni dhambi. Walevi hawataurithi ufalme wa Mungu (1 Kor 6:9-11). Hivyo tubu dhambi hiyo ya ulevi na umkiri Yesu kuwa ni Bwana awezaye kukuokoa na kukuweka huru mbali na dhambi. Fanya hivyo sasa umuache mtekaji huyo kabla hajakupeleka kaburini au kwenye hukumu ya milele. Ulevi sio starehe, ni pingu zisizoonekana. Ni sumu inayoua polepole. Hivyo usiwe miongoni mwao wanywao kileo. Ukiomba sala hii ya toba, utaokoka sasa hivi na kupata nguvu ya kushinda ulevi. Omba hivi:
“Ee Mungu Baba, nimetambua mimi ni mwenye dhambi. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi hii ya ulevi na dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana na Mwokozi wa ulimwengu. Yesu Kristo karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda ulevi na dhambi zote. Niwezeshe kushinda vishawishi vyote vya ulevi. Niwezeshe kuishi maisha matakatifu kuanzia leo. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa na kuniweka huru mbali na ulevi. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen.”
Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Nguvu na neema ya kushinda ulevi tayari imeingia ndani yako. Uambie ulevi: "bye-bye!" Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuishi maisha ya utakatifu. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu, ujiunge nalo, watakupa msaada zaidi wa jinsi ya kuendelea kiroho.
Mungu akutunze na kukufunika kwa ulinzi wake. Washuhudie walevi kuwa Yesu amekuokoa na amekuwezesha kuacha ulevi. Mungu akubariki sasa na hata milele. Amina.
Nimeipenda sana hiyo "kwendraaa" 😀Kwendraaa, kwani kuna faida gani ukifa ukiwa na ini zima? Ama Figo nzima? Kila mtu atakufa vile ilivyopangwa
Ndugu yangu flankUnachokiandika hata hukijui. "Si Kila anayekunywa pombe ni mlevi" huo mstari unaoutaja kwenye biblia unasema "mlevi" wala hausemi "mnywaji".
HAYO NI MATATIZO YA KUJULIA DINI UKUBWANI.
AdventistNimeipenda sana hiyo "kwendraaa" 😀
Ndugu yangu Mjamaa1 shida sio kufa na ini zima au ini lililoharibika. Shida ni kwamba ukifa katika hali ya ulevi, utateseka milele jehanam. Kwa sababu ulevi ni dhambi. Na walevi hawataingia mbinguni.
1 Kor 6:9-11
Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.
WeweNani Adventist, wewe?
Hujasoma uzi huu?Wewe
Ndio Kristo alivunja Sabato vibaya mnoHujasoma uzi huu?
Kwanini Yesu Kristo aliivunja Sabato? Sababu hizi hapa
Yesu Kristo alipokuja duniani alifanya mambo mengi ambayo hayaruhusiwi kufanywa siku ya Sabato. Kwa mfano, aliwaponya wagonjwa na pia aliwaruhusu wanafunzi wake wavunje masuke ya nafaka siku ya Sabato. Hiyo ilikuwa kinyume na sheria ya Sabato. Wakati wa Musa, Mungu aliwaagiza Wana wa Israeli...www.jamiiforums.com