Mjue Steve Ndaula, mmiliki wa kampuni ya BMC iliyowatapeli watu zaidi ya Sh. Bilioni 16 kisha kukimbilia Dubai

Mjue Steve Ndaula, mmiliki wa kampuni ya BMC iliyowatapeli watu zaidi ya Sh. Bilioni 16 kisha kukimbilia Dubai

Mpaka Mchungaji wa KKKT alipewa cheo baada ya kutoa milioni 200!

Huyu Mkulungwa katisha!

Screenshot_20230401_192608.jpg
 
Watu wavivu hupenda kutafuta njoa ya kupata pesa bila jasho. Watanzania wengi ni wavivu, ndiyo maana ukianzisha kitu ambacho halafu ukawaambia wanaweza kutajirika bila jasho, lazima utawapata.

Angalia leo michezo ya kubahatisha ilivyojaa. TV na redio zote ni matangazo ya michezo ya kubahatisha. Na wengine wengi wanaendelea kubuni michezo mingine kwa sababu imeonekana kuwalipa kiurahisi.

Huko Kanda ya Ziwa mpaka wapo walipwahi kuwatoa mpaka watoto wao maalbino wauawe ili wao wapate hela.

Umaskini mkubwa wa Watanzania wengi upo kichwani, ndio unaosababisha umaskini mwa mali.
 
Ukishaona mtu anajiita mtaalamu wa forex, cryptocurrency ama bitcoin jua kabisa utapeli hauko mbali. Hakuna hela inayopatikana kilaini. Biashara nyingi kwenye miaka mitano ya kwanza huwa panda shuka hadi unatamani kuachana nayo. Sasa hawa washenzi wanakwambia unaweka leo unavuna saa hiyohiyo.

Halafu hawa wastaafu ambao kwenye ujana wao wote hadi wanastaafu hawajawahi fanya biashara nadhani hizo pesa wangezitumia tu kuishi maisha yao ya kawaida kabisa bila hekaheka. Yaani hata kama ni biashara ni hizi ndogondogo kama bustani ya mboga, ufugaji wa kuku wa kienyeji, kiduka kidogo cha Mangi nk.
 
Back
Top Bottom