Daimler
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 556
- 974
Mjumbe wa Kamati ya Itikadi na Uenezi Mkoa wa Dar es Salaam, Frey Edward Cosseny, amewarusha tena roho juu wafuasi wa Vyama vya Upinzani baada ya kudai kuwa, kuna Wabunge wengine sita wanafuata baada ya Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya (CHADEMA) kujiunga na CCM.
Frey Cosseny amedai kuwa, Wabunge watakaojiunga na CCM kutokea CHADEMA ni wanatokea Mikoa ifuatvyo:
Mkoa wa Kilimanjaro - Wabunge wawili (02),
Mkoa wa Dar es Salaam - Wabunge wawili (02),
Mkoa wa Manyara - Mbunge mmoja (01),
Mkoa wa Mara - Mbunge mmoja (01).
Haya Wazee wenzangu wa mapovu camp, naomba tutiririke hapa kubashiri Wabunge hao walio mbioni.
Kwa Mkoa wa Mara nahisi Ester Matiko (Tarime Mjini) hatasalimika na hizi radar za CCM. Utakuwa ni usajili mzuri.
Tutaje wa Mikoa mingine.