Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tuma hivyo vitabu hapa hasa hicho cha AnitaNilikuwa nimekaa zangu kwenye mgahawa fulani. Akaja mkaka mzuri tu na alikuwa amependeza. Akakaa kiti cha mbele yangu.
"Mambo? Nimependa nikae na wewe hapa." Akaniongelesha.
"Haina shida." Nikajibu.
"Mbona huna kinywaji au chochote? Agiza chochote. Usikae kinyonge hivyo" Aliuliza.
Nikamjibu "Nimeagiza chakula. Ndio nakisubiri."
"Oh sawa. Vizuri tufahamiane. Me naitwa James, naishi (******). Nafanya kazi hapo (****) Bank kama branch manager. Nikufahamu na wewe please!"
"Naitwa Ederra. Naishi (******).". Nikajitambulisha.
Akaendelea na stori nyingine kwa dakika chache kisha akainuka na kusema angerudi pale punde. Baada ya dakika tatu akarudi.
"Nimerudi Ederra. Nilienda kuangalia gari yangu. Nilikuwa na wasiwasi kama nilikuwa nimepandisha vioo." Akasema huku akikaa tena kwenye kiti.
"Sawa. Karibu tena."
"Asante. Nilikuwa naogopa isije kunyesha mvua au watu wakaniibia KiBMW changu. Unajua gari yenyewe ni mpya nisije kupata hasara. Nilichoka kutembelea Harrier nikaona ninunue na hii"
"Yeah wasiwasi ndio akili." Nikamuunga mkono.
Chakula kikafika. Na yeye akaagiza. Nikawa naendelea kula huku nikisikiliza stori za magari yake, kazi yake nzuri, anapoishi na nyingine kama hizo mpaka nikamaliza kula.
Mhudumu alipokuja kuleta chakula cha jamaa nikamuomba bill.
"Acha tu nitalipa Ederra. Unalipaje wakati mimi niko hapa?" James akaingilia kati.
"Oh sawa. Nashukuru sana."
Nikamuaga kuwa naondoka. Akaniomba namba ya simu. Nikamwambia anipe yake ningemtafuta. Akanipa business card yake na kung'ang'ania nimpigie pale pale lakini nikamwambia asijali ningemtafuta tu. Nikaondoka.
Ile business card niliitupa kwenye dustbin baada ya kupotea kwenye upeo wa macho yake. Nisamehe James. Sio kwa ubaya.
Mwanaume unapotumia nguvu kutaka kuonesha magari unayoendesha, kazi yako unayoiona nzuri, unapoishi na mafanikio yako mengine kwa mwanamke ambaye ndiye kwanza unakutana naye unadhani ndiyo utamvutia?
Hii tabia haivutii. Meseji ya nje unayoileta kwa kufanya hivyo ni kuwa wewe ni mtu wa maana sana na mwenye mafanikio. Meseji hii ya nje sio inayoathiri mvuto wako kwenye akili ya mwanamke.
Meseji iliyojificha (ya ndani kabisa) ndio inayoathiri mvuto wako. Hiyo ni kwamba hujiamni na unadhani huna thamani wewe kama mwanaume na hivyo unalazimika kutumia vitu kama magari, kazi, mafinikio ili uonekane una thamani. Hakuna mwanamke anayejielewa anavutiwa na mwanaume wa hivi.
James asante kwa kunilipia chakula. Lakini wewe na wanaume wengine wenye akili kama zako badilikeni. Itawasaidia.
Jifunzeni kuwa na tabia zinazowavutia wadada. Mnaweza kusoma vitabu hivi viwili mtanishukuru baadae.
1) "UNLOCK HER LEGS: How to Effortlessly Attract Women..." By Dominic Mann
2) "MWANAUME WA DHAHABU : Jifunze Namna ya Kuwatawala Wanawake na Kutawala Mahusiano." By Anita Shija
Mwanaume tafuta uvisome yasije kukukuta ya James. Hasa hicho cha Kiswahili. Usipovipata njoo nikutumie bure tu. Utachangia bando lakini.
Unamaanisha ..James au "Anita shija"?Bro umetisha sana
Umewaza kama mimi.. hata hii account ni mpya mahususi kwa uzi huu.Anita shija ,
Hili tangazo la kitabu chako umelidesign vizuri sana,
Hongera!
Wewe ndo ulimchukulia vibaya na karoho kako ka mashindanoUko sahihi kwa ulichokifanya. Nakupongeza. Binafsi nakereka sana ninapokutana na mtu unayekutana naye mara ya kwanza alafu anaanza kutaja mafanikio yake kimaisha wakati hujamwuliza. Si katika mahusiano tuu hata katika urafiki wa kawaida hata ikiwa ni mwanaume mwenzako. Picha ya kwanza inayoonekana hapo ni ulimbukeni, na anaona hilo gari au kufanya kwake kazi bank au taasisi flani kubwa kubwa ndo silaha pekee ya kuwachapia wanawake. Wanasahau kuwa kuna bad boys wanakula pisi kali huwezi amini.
Back in 2007 niliwahi kukutana na class mate wangu wa advance pale UDSM karibu na hill park. huyu dogo alisoma economics na mimi nikasoma education. Sasa mbwembwe zake kwa sababu hatukuonana muda mrefu cha kwanza akaanza kuniambia anafanya kazi wizara ya viwanda, hapo hapo akanionyesha gari yake, hapo hapo kanionyesha picha ya nyumba yake anayojenga changanyikeni. Hapo hata sijamwuliza wala hajaniuliza kuhusu issues zangu. Upuuzi wake alidhani mimi nitakuwa nimeenda kufundisha sekondari kama ilivyozoeleka kumbe niko kwenye taasisi nyingine kubwa tena mshahara hatupishani sana. Hata hivyo nikaona ujinga kujitambulisha kihivyoo, tukaachana bila kumwambia nafanya kazi wapi. Na sasa hivi kama ni elimu nimeshamzidi ngazi moja. Dharau mbaya
Ukishaona demu anakuita mkaka ujue kashawaka na wewe huyoWewe unaonaje hizo flowline zake, maana wanawake ndizo flow zetu hizo
Hilo neno "mkaka" ndilo linatumiwa na nyie Kinadada, lakini mengine mmh!
Bora umekuwa mkweli tu maana wengine huwa wanafiki sana mwanzoni na kujifanya hajali mambo ya status😅 ila deep down huwa wanaume tunaelewa kuwa mademu wengi bila kujikosha kwa simu za dili za hela ndefu au vitu vya thamani ni nadra kupata attention.[emoji28][emoji1787][emoji1787][emoji1787]sawa...hakuna asopenda hela..ht mimi napenda kweli tena haswaa....ila kuna namna wanakosea approach....kujimwambafy kwa maneno inakeraaaaaaaa[emoji1787]
Watoto wazuri leo mmeamua kutupa semina ya kuwa win kabisa😂 kweli dunia inaenda kasiHaha..
Barbie umenichekesha..! Ku unlock feelings tu ama mpaka pochi iliyokuwa locked.??
Anyways, tafuta hichi 'the power of pussy' - by Kara King..!!
C'ssy Heaven Sent uliwahi waambia wanaume hili kwenye ile thread yako..!!
Wanawake ni warahisi kama una kile wanachokitaka. Key to attraction aidha uwe handsome, uwe na status na influence kwenye jamii, uwe na hela. Mwanamke huwa anapenda kimojawapo hapo.Labda ni wewe tu kwasababu una akili zako.
Ila wanawake sasa ni warahisi sana.
Huu uzi ushakuwa wa kusomeshana vitabu sasa
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Bro umetisha sana
Ahsante kwa muongozo kwa mabahariaSikuwa tayari. Sivutiwi na wanaume wasiojiamini. Na sio mimi tu. Kujiamini ndio silaha kuu ya kuvuta warembo.
Cha bure mjini ni salamu tu, mara nyingine huwezi kuipata hata hiyo salamuHapo kwenye bando!
Ooh af mie ndio namiliki zile apartments masaki pale maeneo ya Chole Road kama unaelekea Village Supermarket.Khaaa nimuonee wivu stranger[emoji1787][emoji1787][emoji1787].am not an idiot....
We km unataka urfk na mimi..sawa. .
Ss unapoanza kujitangaza kwangu ili iweje....
Acheni ushamba..ila sio kosa lake alikulia kijijin huko ushubwadani ....
Ss anahisi kila mtu anaulimbukeni
Na wewe km una tabia hizo achaa....mnaboa
Hujaulizwa unasema[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kifupi umeeleweka, kuji attach uwanaume wako na mafanikio yako it presents weakness!Excellent! Hawa watu wana mengi mno ya kujifunza. Kutangaza mafaniko kwa mwanamke mgeni bila kuulizwa ni ishara ya kuwa nafsi yako inakwambia kwamba wewe huna thamani kama mwanaume, thamani ya kutosha kupata ukaribu wa huyo mwanamke.
Kwa hiyo kukosa kwako thamani ndio unataka kufidia kwa kutumia hivyo unavyomiliki. Kaka zetu pateni haya madini yatawasaidia. Na tutaendelea kuwafunulia tabia zisizovutia ili wanaokubali kijifunza wajifunze.