Mkaka mzuri, ana magari na kazi nzuri ila amenikosa kwa utongozaji wake wa kitoto

Mkaka mzuri, ana magari na kazi nzuri ila amenikosa kwa utongozaji wake wa kitoto

Sasa huyo rafiki yako kazama au position ya mshikaji imemzamisha

Hapo position ya mchizi ndo ilimfanya azamee mana kwa wanawake usipokua na mwonekano basi atleast uwe na vihela ili umpate sasa demu akuzungushe weee afu badae ajue wewe ni mtu fulani afu ndo akukubalie apo unadhan ni nn kimemleta kwako?? Obviously ni pesa na sio kingine
 
Nilikuwa nimekaa zangu kwenye mgahawa fulani. Akaja mkaka mzuri tu na alikuwa amependeza. Akakaa kiti cha mbele yangu.

"Mambo? Nimependa nikae na wewe hapa." Akaniongelesha.

"Haina shida." Nikajibu.

"Mbona huna kinywaji au chochote? Agiza chochote. Usikae kinyonge hivyo" Aliuliza.

Nikamjibu "Nimeagiza chakula. Ndio nakisubiri."

"Oh sawa. Vizuri tufahamiane. Me naitwa James, naishi (******). Nafanya kazi hapo (****) Bank kama branch manager. Nikufahamu na wewe please!"

"Naitwa Ederra. Naishi (******).". Nikajitambulisha.

Akaendelea na stori nyingine kwa dakika chache kisha akainuka na kusema angerudi pale punde. Baada ya dakika tatu akarudi.

"Nimerudi Ederra. Nilienda kuangalia gari yangu. Nilikuwa na wasiwasi kama nilikuwa nimepandisha vioo." Akasema huku akikaa tena kwenye kiti.

"Sawa. Karibu tena."

"Asante. Nilikuwa naogopa isije kunyesha mvua au watu wakaniibia KiBMW changu. Unajua gari yenyewe ni mpya nisije kupata hasara. Nilichoka kutembelea Harrier nikaona ninunue na hii"

"Yeah wasiwasi ndio akili." Nikamuunga mkono.

Chakula kikafika. Na yeye akaagiza. Nikawa naendelea kula huku nikisikiliza stori za magari yake, kazi yake nzuri, anapoishi na nyingine kama hizo mpaka nikamaliza kula.

Mhudumu alipokuja kuleta chakula cha jamaa nikamuomba bill.

"Acha tu nitalipa Ederra. Unalipaje wakati mimi niko hapa?" James akaingilia kati.

"Oh sawa. Nashukuru sana."

Nikamuaga kuwa naondoka. Akaniomba namba ya simu. Nikamwambia anipe yake ningemtafuta. Akanipa business card yake na kung'ang'ania nimpigie pale pale lakini nikamwambia asijali ningemtafuta tu. Nikaondoka.

Ile business card niliitupa kwenye dustbin baada ya kupotea kwenye upeo wa macho yake. Nisamehe James. Sio kwa ubaya.

Mwanaume unapotumia nguvu kutaka kuonesha magari unayoendesha, kazi yako unayoiona nzuri, unapoishi na mafanikio yako mengine kwa mwanamke ambaye ndiye kwanza unakutana naye unadhani ndiyo utamvutia?

Hii tabia haivutii. Meseji ya nje unayoileta kwa kufanya hivyo ni kuwa wewe ni mtu wa maana sana na mwenye mafanikio. Meseji hii ya nje sio inayoathiri mvuto wako kwenye akili ya mwanamke.

Meseji iliyojificha (ya ndani kabisa) ndio inayoathiri mvuto wako. Hiyo ni kwamba hujiamni na unadhani huna thamani wewe kama mwanaume na hivyo unalazimika kutumia vitu kama magari, kazi, mafinikio ili uonekane una thamani. Hakuna mwanamke anayejielewa anavutiwa na mwanaume wa hivi.

James asante kwa kunilipia chakula. Lakini wewe na wanaume wengine wenye akili kama zako badilikeni. Itawasaidia.

Jifunzeni kuwa na tabia zinazowavutia wadada. Mnaweza kusoma vitabu hivi viwili mtanishukuru baadae.

1) "UNLOCK HER LEGS: How to Effortlessly Attract Women..." By Dominic Mann

2) "MWANAUME WA DHAHABU : Jifunze Namna ya Kuwatawala Wanawake na Kutawala Mahusiano." By Anita Shija

Mwanaume tafuta uvisome yasije kukukuta ya James. Hasa hicho cha Kiswahili.
Nnaomba unitumie vitabu hivi through embackgrace@gmail.com
 
James hakukosea ila James amejikita kwenye Uhalisia zaidi kuhusu tabia za wanawake so demu akahisi jamaa anamchoraaa...
James hakukosea. Alikutana na mwanamke tofauti na wanawake walio wengi. Na wanawake wa namna hiyo wako wachache sana. Walio wengi wanaangalia neema zilizo kuzunguka. Gari nzuri, kazi nzuri, maisha mazuri n.k ili akitoa invoice isiwe shida kulipwa.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Juzi kati nilichukua namba ya demu hata jina hatujajuana kasema ana shida ya vochaa nkamtumia tumechat kidogo akaomba 50K[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] yani ni dak 5 baada ya kuweka vocha tu sasa hapo si balaaa
Hahahaaa. Wanawake wa jinsi hiyo huwa nawaona hawajielewi au wanatuona sisi ni wajinga na huwa wanajikosesha mengi. Atoe kwanza ushirikiano ndio aome hiyo 50K. Siwezi toa 50k bila kuwa na uhakika au viashiria vya uhakika vya kuiona ile triangle.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Unatongozwa kadri unavoonekana... Hio ndio sheria ya Wanaume....

Upo Bar,,, utaambiwa nataka mzigo tunafanyaje.... bei. nk
Umevaa kimalaya utatongozwa kimalaya hvohvo.
Upo Bank,, utaombwa namba ya simu.......
Umekaa kisifa sifa,, supa wumani,,, utatongozwa kisifasifa hvohvo...

Usiwapangie watu mitongozo,,, Kazi yako iwe kukataa au kukubali... Coz mbinu isiyofanya kazi kwako ilifanya kwa mwenzako..
OVER..
 
"Ila amenikosa"

Hii kauli inanipa ujumbe flani kwamba wewe ni mtu wa aina gani...
 
nikisema wewe ni Anita shija nitakuwa nimekosea mkuu
 
Kam kweli umemdrop umefanya vyema Ni mjinga atakuwa muhaya huyo ila pia ulikosea pale ungeenda kumuandikia msg Kali namna hi uliotuma huku jf akili s mkae sawa na aone kwamba siyo kila mwanamke anashoboka na magari ishu Zak
Very good kujiamini Ni muhimu San unaweza usiwe. Na gar Ila unaconfidence
 
Shukrani sana bibi author Anita shija, promo yako nimeieleewa . Nice ads
 
Mkuu, mimi napitaga na mademu bila ata ya kusema neno. Issue ni feelings, haukumpenda huyo chalii.

Usidanganye watu wakasome vitabu mpaka macho yapasuke, hakunaga skills wala jitihada, hayo ni mapenzi hayana formula
Mapenzi yanahusika kwa namna moja ama nyingine na saikolojia pamoja na social skills..

Ni kitu unachoweza kujifunza kabisa na uakawa vizuri kwenye sekta hiyo,

Sio wote wana akili nzuri ya kutongoza na kuinteract na watu wa jinsia tofauti (kutokana na malezi na maosha aliyopitia mtu inawe,a kumuathiri).
 
Wadada wa kibongo ndo mnapokosea, huyo jamaa bado humfaham kabisa, na hiyo ni tabia ya wanaume wote.. Kama uko single, kwani ungekufa kumpigia na kumfaham zaidi?
Hiyo ya kujikweza sio tabia ya wanaume wote ni baadhi tu, na tabia hizo zina wa turn off sana wanawake wenye akili zao timamu na wanaojiamini kwa uzuri wao trust...

Ni lazima uelewe , unajikwezwa una BMW, gari ambazo huyo mtoto wa kike toka yipo kindergarten hadi anamaliza chuo anaona wazazi wake wanabidili tu models???, hizo gia kalingishie huko uswazi
 
Back
Top Bottom