Tetesi: Mkakati wa upigaji wa fedha katika anuani za makazi

Tetesi: Mkakati wa upigaji wa fedha katika anuani za makazi

Wanahesabu hadi vibanda vya wachoma mihogo, yaani kwenye stend za daladala lililo ndani ya hifadhi ya barabara
 
Kuna taarifa kwamba upo MKAKATI wa makusudi wa upigaji wa fedha kwenye zoezi la anuani ya makazi 'postcodes' kwa baadhi ya wakurugenzi nguli, wabobezi , viburi na wasio na kwenye kutengeneza hila za wizi panapokuwa na fursa.
Mbinu wanayo ipigia mkakati ni

(1) kulipa pesa waajiriwa hewa ambao watajumuishwa kwenye zoezi bila kujitambua na majina yatakayotumika ni ya wake waliofanya interview na pia wengine walioshiriki mafunzo na kutochukuliwa.

(2) Uendeshaji wa zoezi kwa kuwapumzisha waajiriwa (ambapo wanakuwa hawalipwi siku za mapumziko) lakini kutoa malipo mfululizo ambapo malipo ya siku zote za mapumziko manguli hao watabeba na kutia kapuni

(3) Kulipa malipo tofauti kinyume na Yale ya 20,000/= yaliyoelekezwa ambapo baadhi watalipwa sahihi na baadhi hawatalipwa sahihi

(4) kuzuia malipo ya posho ya wawenyeviti wa mitaa/ vitongoji na hata baadhi yacwatendaji kwa hila mbalimbali ambapo wao kama wakurugenzi mwishoni watayaidhinisha na kushiba vizuri kabisa

Ni wajibu wa vyombo na mamlaka husika kufuatlia kwa ukaribu na kudhibiti haya.
Wacha tule Tu
 
nasikia kuna halmashauri moja wao wanafanya hii kazi kwa siku 7 pekee sasa sijui hizo siku nyingine fedha atachukua nani
 
Back
Top Bottom