Mkanda wa jeshi (Herpes zoster/ shingles) fahamu kuhusu dalili na tiba yake

Mkanda wa jeshi (Herpes zoster/ shingles) fahamu kuhusu dalili na tiba yake

unasitiza usafi wa mwili na mavazi kwani bila hivyo unaweza kuta unaendelea kujiambukiza, vilevile lishe bora ni muhimu
 
kwani lishe bora inaimarisha kinga mwilini, epuka au punguza kwa mda huu matumizi ya corticosteroid kwani ushusha kinga
 
mfano wa corticosteroid ni predinisolone, beclomethasone na hydrocortisone ingawa wataalamu wengine wangeweza kutumia
 
Mkanda wa Jeshi ni kiashiria kuwa kinga ya mkeo ipo chini.
Akapime VVU kwanza.
Dawa nzuri ya mkanda wa jeshi ni vidonge Acyclovir.
Erythromicin hutumika pale tu mkanda wa jeshi umepata maambukizi ya bakteria na kuanza kutoa usaha.Vingenevyo hamna haja ya kutumia Erythromicin.
Iwapo mkanda wa jeshi umepata usaha na hawezi kutumia erythromicin basi dawa muafaka hapo ni cloxacillin vidonge.
 
P?le sana Ila jitaidi kumfanyia Vipimo zaidi. Mama anapokua mjamzito kinga zinashuka so ni raisi kupata magonjwa mbalimbali.
 
Nashukuru kwa maliwazo hayo.

Mke wangu anaendelea vizuri sasa. Aliweza kwenda kazini Jumatatu hadi Jumatano. Vipele vinaonekana kwanza kukauka. Vimetengeneza crust. Maumivu kiasi kidogo sasa. Aliongezewa vidonge vya Acyclovir, Indomethacin na Vitamin B kwa ajili ya kuleta hamu.
Ndugu Jeff unadhani hapo inakosekana ipi?
 
ok hapo sawa kwani indocin ni moja ya non steroidal antiinflamatory drugs (nsaids) inaondoa maumivu
 
Kuwa na mkanda wa jeshi si kuwa na UKIMWI ila ni ishara kuwa kinga yako imeshuka, mkanda wa jeshi unatibika kama unavyotibika UKIMWI. Vyakula vya kuepuka ni vile vinavyoharibu kinga ya mwili ambavyo bilashaka wavijuwa. Kama una swali uliza.
Nataka kujua dawa ya mkanda Wa jeshi,na vyakula vyakuepuka ni nini
 
Ndugu wanaJF (wataalamu wa tiba). Napenda kufahamu endapo kuna ukweli kwamba mtu akiugua ugonjwa uitwao mkanda wa jeshi anakuwa tayari ameshapata UKIMWI? Na endapo ana ugojwa huo afanyeje ili apone kwa urahisi? Kwa upande wa vyakula atumie vyakula gani ili kurahisisha uponaji? Nawasilisha.
Jitahidi kutibu Herpes Zoster mapema unapoona dalili. Kuna dawa ya kupaka wiki moja tuu unapona. Kwa kuwa inaambatana na maumivu makali (kuliko uchungu wa kujifungua) kuna dawa ya kupunguza maumivu. Usipoiwahi ndani ya diku mbili kwa tiba sahihi waweza kupata ulemavu aklu kifo.

Google Herpes Zoster treatment kisha uone current medicine upone faster.
 
Mjibu aliyatoa Zanzibar A ni ya kitaalamu zaidi na hayana mjadala.Mhusika anapaswa kwenda hospitali kufanyiwa vipimo na baadae atapatiwa matibabu sahihi ya mkanda wa jeshi.July jamiiforum atakutana na watani zake watamshauri apake mavi ya asubuhi ya jogoo maana tayari wameshaanza kumtania apakaze vitunguu!!
 
Mkuu, Nimesema mkanda wa jeshi unatibika na unapona kabisa kama unavyotibika na kupona kabisa UKIMWI.
Nani anatibu na kuponya ukimwi. Kama c mimi, kaka, dada, binamu, shemeji nk wanaugua gonjwa hili. But tiba sijawahi sikia
 
Magonjwa / conditions tofauti na UKIMWI zinaweza kusababisha mkanda wa jeshi. Rejea kifo cha Mwalimu Nyerere, ambaye tumeambiwa alifariki kwa kansa ya damu (Leukemia) naye alikuwa na mkanda wa jeshi.

Kwa Mujibu wa Hayati Mchungaji Mtikila Mzee aliondoka kwa Shoti ya Umeme wa Kikubwa!
 
Mkanda wa jeshi ni ugonjwa unaosababishwa na virusi waitwao Varicela Zoster (miongoni mwa Herpes Virus). N. B Ni virusi hawa hawa huleta ugonjwa wa tetekuwanga utotoni (chicken pox) ambao ukipona wale virusi huweza kubaki mwilini katika mishipa ya fahamu wakiwa dhaifu kutokana na kuzidiwa na kinga ya mwili. Baada ya miaka kadhaa kupita endapo kinga ya mwili itakuwa dhaifu virusi hawa hupata nguvu (reactivated) na kuanza kuleta dalili kama muwasho na baadae vipele vinavyofuata jinsi mishipa ya fahamu inavyoenda, kwa nje huonekana mfano wa mkanda wa jeshi, huweza kuambatana na maumivu makali yanayoweza kudumu miezi hata miaka (postherpetic neuralgia). Kwa kifupi ni hivyo mkuu
 
Back
Top Bottom