Mkanda wa jeshi (Herpes zoster/ shingles) fahamu kuhusu dalili na tiba yake

Ni moja ya miongoni mwa magonjwa nyemelezi (opportunistic infection) kwa watu ambao immunity yao ipo suppressed/compromised haswa haswa PLHIV huwa hutokea katika stage 2
 
Mkanda wa jeshi ni ugonjwa unaosababishwa na virusi waitwao Varicela Zoster (miongoni mwa Herpes Virus). N. B Ni virusi hawa hawa huleta ugonjwa wa tetekuwanga utotoni (chicken pox) ambao ukipona wale virusi huweza kubaki mwilini katika mishipa ya fahamu wakiwa dhaifu kutokana na kuzidiwa na kinga ya mwili. Baada ya miaka kadhaa kupita endapo kinga ya mwili itakuwa dhaifu virusi hawa hupata nguvu (reactivated) na kuanza kuleta dalili kama muwasho na baadae vipele vinavyofuata jinsi mishipa ya fahamu inavyoenda, kwa nje huonekana mfano wa mkanda wa jeshi, huweza kuambatana na maumivu makali yanayoweza kudumu miezi hata miaka (postherpetic neuralgia). Kwa kifupi ni hivyo mkuu

Mkuu kuna uhusiano gani kati ya mkanda wa jeshi na HERPES SIMPLEX....na pia je HERPES SIMPLEX ina madhara gani baada ya kukaa mda mrefu mwilini?
 
Mkuu hakuna uhusiano kwani haya ni magonjwa yanayosababishwa na virusi aina mbili tofauti japo wapo kundi moja la herpes viruses (herpes simplex husababishwa na herpes simplex virus (HSV), wakati mkanda wa jeshi husababishwa na Varicela zoster herpes virus).

Mtu huambukizwa herpes virus kwa njia ya mgusano, ikiwemo kujamiiana, na kirusi akiingia hubaki mwilini maisha yote ya mtu huyo (asilimia kati ya 30-95 ya watu wazima wanasadikika kuwa na herpes virus) japo kuwepo kwa kirusi mwilini sio lazima mtu aonyeshe dalili, dalili huonekana pale kinga ya mwili inaposhuka pengine kwa stress, kuugua magonjwa mengine, hata kipindi cha hedhi kwa wanawake.

Herpes simplex wengi wetu tumewahi kuiona kama vipele vidogo vyenye maji yasiyo na rangi mdomoni mtu anapokuwa na homa kisha hupona vyenyewe baada ya muda (cold sores), lakn pia kuna herpes genitalia (ambayo hutokea sehemu za siri.. Kama vipele vidogo vinavyowasha.
 
HABARINI WAKUU!!
Ni ugonjwa wa aina gani hasa kitaalam?
Dalili zake ni zipi, nini sababu ya ugonjwa huu na matibabu yake ni yapi??
SHUKRANI...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shingles herpes zoster ni ugonjwa unaosababishwa na virus ukiambatana na maumivu makali katika sehemu husika

Mara nyingi hushambulia watoto, wazee vikongwe na watu wenye upungufu wa kinga mwilini .
Herpes Mara nyingi hutokea baada ya mgonjwa kushambuliwa na viral pneumonia au viral bronchitis na virus hivi kukimbilia kwenye centra nervous system

Matibabu ni antivirus kwa ushauri wa daktari
 
Mkanda wa jeshi ni ugonjwa unaosababishwa ni virusi vile vya tetekuwanga. Unapopata tetekuwanga na ukaitibu wale virus hawafi wanaenda kujificha kwenye pingili za uti wa mgongo upande mmoja wapo, wa kulia au wa kushoto. Sasa kinga ya mwili inaposhuka wale virus wanapata nguvu wanatoka kwenye maficho yao na wanaanza kukushambulia. Mashambulizi yake utapata homa kali, maumivu ya mwili na vipele vya tete kuwanga vitatoka kufuata kila mshipa wa damu. Ndomana unaitwa mkanda wa jeshi coz hautokei mwili mzima bali upande ule ambao wale virusi walijificha pindi ulipotibu tete kuwanga. Huo ndio mkanda wa jeshi. Dawa kupata dawa n na matibabu nenda hospitali ya maana coz kwa hospitali ambazo hawana specialist wanaweza kukwambia una fungus kwenye ngozi kumbe ugonjwa hawajaufahamu.
 
asee kumbe ndio hivyo
 
Ahsante sana!!
Ubarikiwee...

Ahsante sana kwa maelezo mazuri!!
Ubarikiwe!!

Unajua kuelezea mkuu.Hongera sana

Good Neighbour
 
Watazunguka wewe lakini hiyo ni dalili ya UKIMWI na mpaka ifikie hivyo ujue upo mwisho mwisho!
 
Back
Top Bottom