Mkandarasi wa barabara ya Mbeya mjini inayokwenda kwenda Zambia amesusa kutokana na kutolipwa na serikali?

Hiyo njia inafumuliwa na kujenda kila baada ya miaka mingapi,
Baada ya kujengwa miaka ya 1970s ilifumuliwa na kujengwa 1990s, ikajengwa tena 2014 au 15
Ujenzi ni sehemu mojawapo nzuri sana ya kupiga pesa za raia bila kelele nyingi.
 
Unasema hakuna shida, huku unasema kuna tatizo la wakandarasi kulipwa.

Sema moja, ujenzi unaendelea au umesimama?
 
Kwani ni yeye tu, miraxi yote imesimama kama miradi ya SGR
 
Sawa nimeelewa wanatakiwa wakusanye kwanza. Kwa hiyo wakikusanya priority ni kulipa madeni? Na bado wanakopa?
Serikali haifanyi mambo kama watu kwamba inakusanya ndio inapanga matumizi Bali wanaweka Bajeti wakati hawana cash so itakayopatikana ndio inagawiwa kulingana na vipaombele.

Ikipatikana kidogo basi miradi Huwa haipati hela kabisa
 
Unasema hakuna shida, huku unasema kuna tatizo la wakandarasi kulipwa.

Sema moja, ujenzi unaendelea au umesimama?
Unaendeleaje ila Kwa kusua sua.Ujenzi sio kukwangua Barabara tuu hata kujenga makalvati ni Ujenzi huo.
 
Mkandarasi ni kampuni gani?
Na hiyo barabara ni ya ukubwa gani na ina Kilomita ngapi?
 
Watu wengi wamelalamika ujenzi kusimama, una ushahidi wa ujenzi kuendelea? Hata picha ya karavati zinazoendelea kujengwa?
Watu wengi wanadhani ujenzi ni mpaka waone magreda Mitaani,hata ukienda kambini pale Iwambi ukakuta wanasaga kokoto ndio sehemu ya ujenzi huo.

Kilichopo NJ ujenzi unaosua sua kabisa ,Hilo liko wazi maana wakandarasi hawajalipwa.
 
Okay, nadhani ukubali tu kuwa kuna shida. Ujenzi ukiwa unaendelea, hauhitaji kushawishi watu sana. Si tunaona mwendokasi hapa Dar, hakuna maneno ya kusaga kokoto
 
Nimepita Mwezi Wa Nne Hakuna Lolote
Kazi Imesimama
 
Serikali haifanyi mambo kama watu kwamba inakusanya ndio inapanga matumizi Bali wanaweka Bajeti wakati hawana cash so itakayopatikana ndio inagawiwa kulingana na vipaombele.

Ikipatikana kidogo basi miradi Huwa haipati hela kabisa
Huo ni uongo. Huwezi ku-engage contractor wa nje wa kiwango cha China Construction Company kwa hela ya kudunduliza, mradi wenyewe mkubwa kama huu, ambao unahitaji kuwa underwritten!
 
Nipo Mbeya toka katikati ya mwezi wa nane... ujenzi kipindi hiko ulikuwa umesimama kabisa kiasi cha watu kujichukulia vifusi vilivyowekwa kwa ujenzi.

Wiki ya 39 ndio umeanza tena... na wengi wanasema kuwa sababu ya ujenzi kusimama ni malipo.

Mkandarasi anaitwa CHICCO.
 
Upo mbeya ipi wewe tuliza mtk
 
naona wanaendelea sahivi
Labda wameondoka tena baada ya watu wa Mbeya kurusha chupa Zuchu aliposema mitano tena kwa mama! Mbeya mbona watakoma!

Ila huyu mtoto laana kabisa, hebu ona ishara anayowafanyia watu wa Mbeya baada ya kushodoa na kauli yake ya mitano tena kwa mama! Basata watamwita? Au hiyo inaruhusiwa toka kwa wasanii, isipokuwa kuisema serikali na Raisi Samia?

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…