Mkandarasi wa Uturuki, Yapi Merkezi athibitisha pengo la $1.8bn katika ufadhili wa Tanzania SGR

Mkandarasi wa Uturuki, Yapi Merkezi athibitisha pengo la $1.8bn katika ufadhili wa Tanzania SGR

Duh yaani Huku Chawa kule Mchwa...., Duh na wakimaliza huko watageuka Kupe kuanza kunyonya Damu (thinking about it nadhani na Kupe pia wapo)
 
Watu waliuliza Kwa nini tunafanya miradi mingi mikubwa kwa pamoja wakaitwa vibaraka wa mabeberu na wengine kama kina Lissu wakaambulia kupigwa risasi.

Hela tulizokuwa tunaambiwa zipo Kwa ajili ya hii miradi zimekwenda wapi?
Na wewe unakubali kabisa hizi propaganda na unaona poa tu...., sitashangaa na kesho wakianza kutafuta ufadhili zaidi wa Bwawa la Nyerere kwa kusema pesa haipo na wao kuendelea kutunisha akaunti zao binafsi..., After all mmeshawapa loophole ya kupeleka lawama kwa Marehemu....
 
Haya yanafanyika katika nchi ambayo maji na umeme bado si vitu vya uhakika kwa qananchi!! Mradi wa doll Billion 10 utarejesha faida lini?
Kwani lengo ni kutengeneza faida au kutoa huduma? Kwaiyo tusijenge barabara kuelekea vijiji kisa hatuwezi pata faida ya pesa?
 
Hiyo Siku ni Lini maana huwa mnaishia kusema ipo Siku toka awamu 1
Siku hio huenda sio your life time bali vitukuu vyako...., upuuzi unaofanyika leo impact yake itakuja..., unadhani watu wakiwa na nothing to loose na wachache mababu zao wamechota kila kitu na kuzungukwa na masikini wa kutupwa hao masikini watawaangalia tu.....
 
Wakati serikali ya Tanzania ikiendelea kuficha ukweli, Kampuni ya ujenzi ya Uturuki ya Yapi Merkezi imeripoti pengo la dola bilioni 1.8 (zaidi ya shilingi trilioni 4.5 za kitanzania) katika ufadhili wa mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa nchini Tanzania huku ikiendelea kuwezesha Dodoma kutafuta ufadhili wa mradi huo kote Ulaya.

Makamu Mwenyekiti wa Yapi Merkezi, Erdem Arioglu, ambaye hivi karibuni alimuongoza Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na ujumbe wa Serikali katika nchi za Hispania, Sweden na Poland kutafuta ufadhili wa mradi huo, aliliambia gazeti la The EastAfrican kuwa harakati za kuchangisha fedha hizo ni ufuatiliaji wa ahadi mbalimbali zinazofikia dola bilioni 2.2. kuelekea mradi wa dola bilioni 10.4.

Alikanusha kuwa Yapi iliongoza misheni hiyo walipochunguza Mpango B - ufadhili mbadala ili kushughulikia matatizo yake yenyewe ya mtiririko wa pesa - lakini walifanya hivyo katika nafasi zao kama mkandarasi mkuu kwa awamu nne za kwanza za mradi.

Source: THE EASTAFRICAN
Turkey contractor confirms $1.8bn gap in funding Tanzania SGR
Huu mradi meko aliuleta kufisadi pesa tu,mradi karibia miaka 6 haujafika hata dodoma umeshakula matrlioni...mama abdul nae anakula tu pesa na mbarawa,kadogosa anaweza kua tajiri mkubwa mana ndio msimamizi wa huu mradi.
Mradi thamani yake ya ujenzi haieleweki yani ccm ni majambazi wa mchana kweupe
 
Sure mradi ulikuwa unaenda vizuri sana, nadhani kuna watu wenye personal interest wanahujumu huu mradi ambayo ni game changer kwenye transportation industry.
Huu mradi meko alianzisha bila kujua thamani yote ya mradi,alijiona yeye ni one man show...huu mradi mpka sasa haujulikana gharama yake
 
Lengo la mradi ni kutengeneza faida au huduma ?
Nimekuuliza kati ya bafu na choo kwako utaanza na kipi? Maana kwenye maelez9 yangu ya awali nimejadili kuhusu shida ya maji wewe umeiruka!
 
Nimekuuliza kati ya bafu na choo kwako utaanza na kipi? Maana kwenye maelez9 yangu ya awali nimejadili kuhusu shida ya maji wewe umeiruka!
Kwani hapa hapa tunazungumzia mradi wa ujezi wa vyo na mabafu?
 
Kuna tatizo la jumla katika uwezo wa kufikiri kwa wengi wa viongozi na wanaoitwa wataalamu nchini.
Kuna sababu gani ya kuanza kujenga vipande vya SGR mpaka Mwanza au Kigoma badala ya kumaliza na kutumia DSM -Moro -Dodoma?
Akili ya kawaida inatuonesha tujenge kwa awamu na kumaliza vipande vya mwanzo.
Jenga na tumia Dar -Moro, ukimaliza endelea Moro-Dodoma, ikiwa tayari na kutumika unaendelea Dodoma Isaka,......
Kuwa kiongozi au kuitwa mtaalamu ni jambo moja na kutumia akili kwa ufanisi ni jingine.
 
Wakati serikali ya Tanzania ikiendelea kuficha ukweli, Kampuni ya ujenzi ya Uturuki ya Yapi Merkezi imeripoti pengo la dola bilioni 1.8 (zaidi ya shilingi trilioni 4.5 za kitanzania) katika ufadhili wa mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa nchini Tanzania huku ikiendelea kuwezesha Dodoma kutafuta ufadhili wa mradi huo kote Ulaya.

Makamu Mwenyekiti wa Yapi Merkezi, Erdem Arioglu, ambaye hivi karibuni alimuongoza Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na ujumbe wa Serikali katika nchi za Hispania, Sweden na Poland kutafuta ufadhili wa mradi huo, aliliambia gazeti la The EastAfrican kuwa harakati za kuchangisha fedha hizo ni ufuatiliaji wa ahadi mbalimbali zinazofikia dola bilioni 2.2. kuelekea mradi wa dola bilioni 10.4.

Alikanusha kuwa Yapi iliongoza misheni hiyo walipochunguza Mpango B - ufadhili mbadala ili kushughulikia matatizo yake yenyewe ya mtiririko wa pesa - lakini walifanya hivyo katika nafasi zao kama mkandarasi mkuu kwa awamu nne za kwanza za mradi.

Source: THE EASTAFRICAN
Turkey contractor confirms $1.8bn gap in funding Tanzania SGR
Tushashikwa pabaya tena....!
 
Back
Top Bottom