Mkandarasi wa wizi wa nyeti kasababisha madhara makubwa

Mkandarasi wa wizi wa nyeti kasababisha madhara makubwa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Kuna baadhi wanadai ni kile chama cha majambazi lakini kiuhalisia hakina akili kubwa namna hiyo.. Maana chenyewe kiko hoi bin taaban chali kabisa

Haya ni matukio yakuja na kupita
Yapo
Yalikuwepo
Na yatazidi kuwepo
Baadhi ambayo yaliwahi kuvuma sana ni
Mtu joka wa buguruni
TV za kumuona nwizi
Popobawa
Mumiani mnyonya damu
Mchuna ngozi
Nknk

Sass hili la wizi wa nyeti za wanaume limekuja na madhara mengi hasa ya kijamii
Hofu ya kuibiwa nyeti
Watu kusingiziwa uongo
Watu kupigwa, kujeruhiwa na kuumizwa sana
Uharibifu wa mali
Upotevu wa pesa na mali
Watu kukamatwa kwa kusema uongo
Taharuki kwenye jamii

Kwa bahati mbaya sana matukio ya namna hii huenea haraka kama moto wa nyasi kavu mbugani

Kwa kifupi kuna watu wanafaidika na haya mambo la sivyo mamlaka husika zingetoa elimu kwa haraka kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari
Katika hali ya kawaida kabisa ni nani alishawahi kushuhudia mtu aliyeibiwa nyeti zake?

Kama huo uwezo ungekuwepo mbona wanawake wangeringa sana? Maana wangekuwa na uwezo wa kuondoka nazo asubuhi na kuzirudisha jioni (LTE edition)
Sanasana wachache walioweza kwa uchache ni wanamazingaombwe kwenye viini macho tena kwa muda mfupi sana

Hakuna mganga mwenye uwezo wa kuchukua nyeti za mtu.. Achilia mbali huu uvumi kwamba wachukuaji wakikushika tu bega mzigo wote unaondoka

Sasa watu hawajiulizi
Huyo mchukuaji ana nguvu gani ya kuhamisha nyeti za mtu
Kishapo anazihifadhi wapi
Soko lake like wali
Zinauzwaje
Zinahifadhiwaje
Zinasafirishwaje
Zinaenda kutumikaje

Kama mtu ana uwezo wa kukushika tu bega na mzigo ukahama wote! Si basi akusubiri usiku umelala kama hadithi za popobawa?

Mostly wengi walidanganywa zinapelekwa Kongo kutengeneza madawa ya kinga, mvuto na utajiri.. Kongo kuna vita hivyo kuhitaji kupata nyeti za watu hakuhitaji mtu asafiri mpaka bongo

Hata hivyo kwenye uganga pia kuna vigezo na masharti.. Ndio maana mganga hutaka kuletewa vifaa vyenye mambo fulani.. Mano jasho la jogoo wa kijani na njano aliyetoka kula mdondo saa sita mchana!

Sasa vigezo vya hizo nyeti ni vipi?
Vibamia?
Nene?
Fupi?
Iliyopinda?
Mkono wa sweta?
Yenye busha?
Yenye kovu?
Iliyopita kwa ngariba bila ganzi?
Au iliyotutumka kama mashavu ya mtu mwenye safura?
Huu upuuzi umesababisha kadhia kubwa kwenye jamii
79660eeb-3bbb-4f90-b2d5-d6f6b94b5232.jpeg
 
sasa jamii yenyewe kama haihakiki mzigo wa anayelalamika hama haupo kweli wao wanaanza tu kumbonda anayetuhumiw na mpajka kumuua. mimi binafsi kwenye hilo ccm licha ya mapungufu yake ila sina cha kuwalaumu sana kwenye hilo , maana sisi wenyewe hata common sense za kawaida hatuna
 
sasa jamii yenyewe kama haihakiki mzigo wa anayelalamika hama haupo kweli wao wanaanza tu kumbonda anayetuhumiw na mpajka kumuua. mimi binafsi kwenye hilo ccm licha ya mapungufu yake ila sina cha kuwalaumu sana kwenye hilo , maana sisi wenyewe hata common sense za kawaida hatuna
Mtu anaye amini hana haja ya kutumia common sense mkuu
 
Ninakumbuka mkuu,
ukiwa unaenda kuzima taa anakwambia pumzika anaizima akiwa hapohapo kitandani.
Hizi imani toka nilipo anza kuzisikia nilikua na mashaka ni fix tu , kuna kijiji kimoja niliishi kulikua na uwanja wa mpira wa shule halafu chini ya uwanja kuna makaburi ya wakazi wa hapo kibao

Stories zikaanza ikifika saa 6 usiku ukipita hapa unaona watu wanacheza mpira wametokea makaburini , siku moja nikaenda hapo uwanjani ili nione nilikaa mpaka saa 9 hola , mbuu tu walinifaidi nikaona nisepe
 
We call it spinning.

Ila mpaka inatokea hali kama hiyo probably idadi ya wajinga ni kubwa sana .

Kuna watu wameuliwa , nakupata matatizo for this fake rumors.

Jamii yetu 85% ya watu wake ni uncivilized .

Kutokana na umasikini MTU akiamka atawaza kula, kufanya ngono na kulewa.

MTU kama huyu ukimletea habari kama hizi hatojipa muda wa kufikiri mara 2 but ata play any tune
 
Kwa Dunia ya Sasa ni hatari sana kuzungukwa na MTU au watu wasio na ELIMU ya kujitambua na ambao hawana hofu ya MUNGU.

Just imagine Hawa watu waliouliwa kisa huu uvumi walikuwa na kosa Gani ?

Watu waliokosa hofu ya MUNGU walileta taharuki na wajinga wanauana kwa kukosa ELIMU ya kujitambua.
 
Back
Top Bottom