Mkapa kaondoka, je nani atamfunga paka Kengele?

Mkapa kaondoka, je nani atamfunga paka Kengele?

Huwezi Iona thamani ya mtu angali bado anaishi Ila akishakufa ndo utajua thamani na umuhimu wake.

Ukweli nikwamba Taifa la Tanzania tumepoteza mtu mhimu Sana na hata CCM imepoteza mtu mhimu Sana ambae alikuwa yupo tayari alale njaa ili CCM ipate ushawishi na kura za kutosha kutoka kwa wananchi.
Kweli maana ya Zanzibar na Mwembechai si haba
 
Daah!!! Juzi wakati Magu anatoa taarifa ya msiba, alikua kanyong'onyea sana, nilihisi jambo kwake kama nilivosoma huu uzi. Magufuli sasa anahisi upweke sana, hii vita ni nzito ndani ya chama na nje ya chama
Jasiri muongoza njia ndio karesti ini pisi, mwamba aliumia sana alitoa taarifa kwa uchungu sana.
 
Hakika kuondoka kwa Mkapa c tu pigo kwa CCM bali pia kwa Taifa kwa ujumla.

Na hapo ndipo utajua kumbe Mzee Mkapa alikuwa na maono ya mbali kwa kuifanya CCM kucheza turufu dume.

Mwaka 2015, wakati wa chama tawala rushwa ikiwa imetamalaki na ilikuwa ndiyo agenda kuu ya wapinzani na kuwaaminisha watanzania kuwa CCM ni ile ile ya rushwa.

Hasa baada ya Rais alokuwepo kuwa na mtu wake alotaka ameithishe kijiti cha Urais kwa maana ya JK kumpa Membe.

Watu hawakuwa wanaona kama kuna mabadiliko yoyote zaidi ya kuendeleza miziz ya rushwa kwani membe na utawala ulokuwepo mi kiti kile kile.

Ndiposa Mzee akasema hapana, hapa kinachitakiwa na kuendelea kukilinda chama tuache sasa dhana ya mazoea na kuandaana badala yake tuweke mtu ambae watu wanamuelewa ana uwezo wa kukemea rushwa na asiye cheka na nyau.

Na kwakuwa sote tulishajua utendaji kazi wa Raisi wa sasa bac kwa sehemu kubwa ilisaidia CCM kurudi madarakani.

Na hasa ukizingatia mtu alokuwa anasimama kupeperusha bendera ya vyama vya upinzani alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa, Mzee EL.

Inapofikia hatua watu wakasema kwa hali ya rushwa ilivyotamalaki ndani ya chama ni bora tuweke jiwe likagombee na CCM kikubwa tu iondoke madarakani bac ujue mwisho ulikuwa unawadia kama yasingekuwa maono makubwa ya Hayati mzee Mkapa.

Hakika mzee huyu alikuwa nguzo muhimu ndani ya chama na kwa Taifa kwa ujumla. RIP mzee wetu.
 
Ngoja praise timu ije ihale uhalo kwenye thread yako iliyotukuka.
 
Duhh kwahiyo hapo unahisi nn braza kaka daah maneno yako mmmh!!!!! haya
 
Hayo mambo si ya wastaafu bali ni wananchi kuzuia au kutozuia wanaodhani wanamamlaka ya kufanya chochote wataujutia uamuzi wao mda ukifika
 
. Hata baadhi ya wazee (kina Kikwete) walikua wanamtumia yeye kuwasilisha madukuduku yao. Kama unakumbuka ile audio ya Kinana iliyovuja mtandaoni, Kinana alisikika akimwambia Nape kuwa Mkapa alitaka kumuona Magufuli kuongea nae kuhusu maswala ya Chama, ila Magufuli alikua anamkimbia. Hii ilidhiirisha influence ya Mkapa kwenye uRais wa Magufuli.
Duuuh . . . simulizi tamu kwelikweli maana imekua kama movie vile. Anyway, kuna ukweli kiasi kuhusu uliyoyaandika na kwa kweli hata sisi wananchi tuko puzzled tu hatujui nini itakua hatma hasa kwenye suala la ushauri na mshauri neutral ambaye atafuata kama alivyokuwa mzee Mkapa
 
Back
Top Bottom