FUTURE HUNTER
JF-Expert Member
- Apr 30, 2018
- 2,050
- 2,651
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] paka atakuwa huru kujitanua bila kidhibiti mabawa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Anaogopa jinsi ya kumfunga "pakashume" aka "kimbulu" kengele!😂😂😂😂Ninini kinamliza JK hapa!?[emoji848][emoji848][emoji848]
Hivi kwenye kile Kitabu alicho andika Marehemu aliwaomba msamaha wale aliowaita Malofa siku ile ya Kampeni pale Jangwani?.Muda wa kumfunga paka kengele haupo. Paka apigwe manati ya utosi
Pinda huyu alietoa pendekezo Magufuli aongezewa muda?? Kazi ipo kweli.amebaki mheshimiwa pinda tu ambae jiwe huwa anamsikiliza...hao wengine hakuna kitu.
"Ndoa" ya Magufuli na Makonda ilishaisha muda mrefu sanaaaa. Alishamtosa muda kweli, nashangaa kwanini watu bado wanadhani Makonda ana infuence yotote kwa jiwe.Naona Magufuli amteue Makonda azibe nafasi iliyoachwa wazi na Mkapa
Ataweza kuvaa viatu vya mkapa na kusema kweli pale ambapo hayaend sawaNinini kinamliza JK hapa!?[emoji848][emoji848][emoji848]
Kuna mtu alisema huwezi ogopa kinyago ulichochonga mwenyewe unless you are abnormalKweli kabisa BWM alikuwa hamuogopi JIWE.
Ni siri iliyo wazi kuwa Hayati Benjamin Mkapa alikuwa nguzo muhimu sana CCM haswa katika utawala huu wa Magufuli. Mkapa alikua mtu pekee ambae alikua haogopi kumpa Magufuli za uso. Magufuli mwenyewe alikua sio tu anamheshimu sana, bali alikua anamchukulia kama baba yake maana Mkapa ndiye aliyemsaidia kuingia kwenye ulingo wa siasa, na alichangia sana yeye kuwa Rais 2015.
Mkapa ndiye alimnadi Magufuli jukwaani 1995 wakati anaomba ubunge Chato ambao Magufuli alishinda. Akamteua kuwa Naibu Waziri na baadae kuwa Waziri kamili. Tunajua Mkapa alizungumza wazi uchapakazi wa Magufuli mpaka kumuita Askari wake wa Mwavuli, hali iliyosababishwa Magufuli kunyweshwa sumu na "watu" waliodhani anaandaliwa na Mkapa kuwa Rais 2005. Mkapa aliendelea kumlinda na hata kumpa ulinzi wa usalama wa taifa.
Mchakato wa Urais 2015
Tunajua Lowassa alikatwa 2015 sababu Kikwete alitaka Membe amrithi Urais. Vyanzo mbalimbali ndani ya chama vinasema Kamati ya Wazee, kwa ushawishi mkubwa wa Mzee Mkapa, vilionya Membe asingeweza kumshinda Lowassa sababu wananchi wangeona ni muendelezo wa miaka mitano wa Rais Kikwete. Ndipo jina la Magufuli likapendekezwa na Mkapa, na alitetea kuwa Magufuli ni mtu ambae amefanya kazi zake "consistently" na kuwa ni mtu ambae hana "roots" ndani ya chama hivyo itakua rahisi CCM kunadi sera za Rushwa ambayo ndio ilikua agenda kuu ya Upinzani. Kikwete ikabidi akubali, na kilichofuata ilikua tu itifaki ya kupitisha jina la mgombea.
Baada ya Urais 2015
Mkapa alifurahishwa na jinsi Magufuli alivokuwa anaendesha nchi mwanzoni, ila baada ya kama mwaka hivi, akaona jinsi mtu aliempigania alivokuwa ameaza kubadilika. Alikua ananadi mafanikio ya serikali kama ya kwake (Magufuli) binafsi na sio ya CCM. Pia, Magufuli, mara kadhaa alikua anaponda jinsi MaRais wezake walivyoendesha nchi na mida mengine aliponda sera za Mkapa za ubinafsishaji.
Hata hivyo, uhusiano kati ya hawa ulizorota sana kwa takribani mwaka hivi maana Magufuli aliona anamuingilia sana katika kazi zake. Mkapa akanawa mikono. Waliohudhuria mkutano wa Mkapa kule kigamboni 2018 mnajua alisema kuwa anaomba asihusihwe na mambo yanayoendelea nchini maana kama mstaafu amejaribu kwa nguvu zote kutoa mchango wake ila hausikilizwi.
Kwa mnaofuatilia kwa ukaribu sana siasa za nchi mtajua kuna wakati, Rais Mkapa alikuwa haonekani katika hafla za kitaifa, ni kwa sababu alikuwa anagomea mialiko. Magufuli, kuona mtu anaemuheshimu hampi support, alijirudi, akaongea nae na uhusiano wao ukaanza kurudi taratibu.
Baada ya hapo alikua moja wa watu wachache sana ambao Magufuli alikua anawasikiliza. Hata baadhi ya wazee (kina Kikwete) walikua wanamtumia yeye kuwasilisha madukuduku yao. Kama unakumbuka ile audio ya Kinana iliyovuja mtandaoni, Kinana alisikika akimwambia Nape kuwa Mkapa alitaka kumuona Magufuli kuongea nae kuhusu maswala ya Chama, ila Magufuli alikua anamkimbia. Hii ilidhiirisha influence ya Mkapa kwenye uRais wa Magufuli.
Nini sasa baada ya kifo?
Wastaafu waliobaki tunajua hawana nguvu kama aliyokuwa nayo mzee Mkapa kumshauri Magufuli kwenye maswala mbalimbali, Kikwete analinda maslai ya familia yake - mtoto na Mke wake waendelee kuwa Wabunge, na pia kulinda baadhi ya bishara zake. Mwinyi anataka mwanae awe Rais wa Zanzibar na pia ukweli ni kuwa amekua mzee sana na hata mawazo yake (kama lile la kutaka Magufuli apewe zawadi ya kuongezewa muda wa uongozi) hayachukuliwi kwa uzito.
Ndio maana Kikwete amesikitika sana, anajua jinsi huyo mzee alivokuwa na nguvu katika kutoa kauli ya wastaafu. Mkapa alikua moja ya watu wachache sana ambao walikua hawamwogopi Magufuli, and he spoke his mind whenever necessary.
Kwa hali ya siasa ilivyo nchini, kilichobaki ni kumuomba Mungu tu, maana kizingiti kikubwa kilichokuwa kimzuie Magufuli (kama alikua na mpango wa kubadilisha katiba atawale zaidi ya 2025) kimeondoka. Tuwaombee wastaafu waliobaki wasimame kwa umoja na nguvu moja kusemea maswala muhimu ya nchi, la sivyo tunapoelekea naona giza tu.
Kwakweli, baada ya Mzee Julius, alibaki huyu mwenye sauti ya kimamlaka na vision isiyoyumba kuhusu taifa hili.Huwezi Iona thamani ya mtu angali bado anaishi Ila akishakufa ndo utajua thamani na umuhimu wake.
Ukweli nikwamba Taifa la Tanzania tumepoteza mtu mhimu Sana na hata CCM imepoteza mtu mhimu Sana ambae alikuwa yupo tayari alale njaa ili CCM ipate ushawishi na kura za kutosha kutoka kwa wananchi.
Hakika kuondoka kwa Mkapa c tu pigo kwa CCM bali pia kwa Taifa kwa ujumla.
Na hapo ndipo utajua kumbe Mzee Mkapa alikuwa na maono ya mbali kwa kuifanya CCM kucheza turufu dume.
Mwaka 2015, wakati wa chama tawala rushwa ikiwa imetamalaki na ilikuwa ndiyo agenda kuu ya wapinzani na kuwaaminisha watanzania kuwa CCM ni ile ile ya rushwa.
Hasa baada ya Rais alokuwepo kuwa na mtu wake alotaka ameithishe kijiti cha Urais kwa maana ya JK kumpa Membe.
Watu hawakuwa wanaona kama kuna mabadiliko yoyote zaidi ya kuendeleza miziz ya rushwa kwani membe na utawala ulokuwepo mi kiti kile kile.
Ndiposa Mzee akasema hapana, hapa kinachitakiwa na kuendelea kukilinda chama tuache sasa dhana ya mazoea na kuandaana badala yake tuweke mtu ambae watu wanamuelewa ana uwezo wa kukemea rushwa na asiye cheka na nyau.
Na kwakuwa sote tulishajua utendaji kazi wa Raisi wa sasa bac kwa sehemu kubwa ilisaidia CCM kurudi madarakani.
Na hasa ukizingatia mtu alokuwa anasimama kupeperusha bendera ya vyama vya upinzani alikuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa, Mzee EL.
Inapofikia hatua watu wakasema kwa hali ya rushwa ilivyotamalaki ndani ya chama ni bora tuweke jiwe likagombee na CCM kikubwa tu iondoke madarakani bac ujue mwisho ulikuwa unawadia kama yasingekuwa maono makubwa ya Hayati mzee Mkapa.
Hakika mzee huyu alikuwa nguzo muhimu ndani ya chama na kwa Taifa kwa ujumla. RIP mzee wetu.