Mkapa kaondoka, je nani atamfunga paka Kengele?

Historia ina tabia ya kujirudia, alichofanya Raisi Magufuli kwa Mzee Mkapa ndicho alichokifanya Raisi Mkapa kwa Mzee Nyerere. Mwaka 1995 ulikuwa ni mwaka wa wakina Jakaya na Malecela lakini Mzee Nyerere akatumia nguvu zake za Ubaba wa Taifa kumfanya Mkapa awe Raisi. Mkapa alinadiwa kama Mr Clean huku Magufuli kama Tingatinga na Askari wa Mwamvuli.

Haukuvuka hata mwaka Raisi Mkapa akaanza kumkera sana Mzee Nyerere, basi watu wakawa wanapeleka malalamiko yao kwa Mzee Nyerere kwasababu wanamuogopa Mkapa. Baada ya mwaka 2015 watu walianza kupeleka malalamiko yao kwa Mzee Mkapa kisa wanamuogopa Magufuli. Yaani historia imejirudia vizuri sanaa!

Mzee Nyerere alikufa kwa majonzi baada ya kugeukwa na Mkapa,
Mzee Mkapa amekufa kwa majonzi baada ya kugeukwa na Magufuli.
Historia huwa ina tabia ya kujirudia rudia tu, hivyo tuwe tunatunza kumbukumbu zetu vizuri.

NB: Baada ya Mzee Nyerere kufariki hakukuwa na mtu wa kumfunga lijamu Mkapa, akaamua kutuuza wananchi wote kwa mabepari maana alifanya kila analotaka. Raisi Magufuli naye anaelekea kulekule kwenye "ABSOLUTE POWER" ambako Raisi Mkapa alielekea baada ya kifo cha Mzee Nyerere. Hatua stahiki zisipochukuliwa na watu wenye akili timamu tutakuja siku kuikumbuka hii miaka kwa majonzi sana.
 
We have 2 problems.
1.CCM
2.Ccm voters
 
Hapa ni kimoja tu wandugu tumpe Lissu huyu bwana ataokoa ya hovyo mengi ambayo yanakuja kuanzia 2021 hadi 2025, wengi watajuta hapa.
Kweli sauti ya mamlaka imeondoka
Wee unafikiri alivyokuwa ana mkaripia magu alifurahi moyoni wakati magu uwezo anao?
Umeongea jambo la maana sana
JPM kapata pigo kubwa sana…tumfariji
Muda wa kumfunga paka kengele haupo. Paka apigwe manati ya utosi
Wakati ni ukuta Mungu atotuacha yatima
 
Bila mtu wa kumdhibiti Magu, atatukaanga kwa mafuta ya mawese atutafune
 
Hapa ni kimoja tu wandugu tumpe Lissu huyu bwana ataokoa ya hovyo mengi ambayo yanakuja kuanzia 2021 hadi 2025, wengi watajuta hapa.

Lissu alijimaliza mwenyewe alipounga mkono ujio wael cdm. Haya mengine yote anayo ya fanya ni yale ya mfa maji. Dhambi ya ulaghai wao kwetu wananchi kamwe haita waacha salama. Wameanza kuvunjika/kuvunjwa miguu mwisho wake ni mioyo. Labda watubu kwa Mola wao wala si kushupaza shingo. Nikuulize siku hizi za karibu ulisha wasikia wakiongelea juu ya wale wahanga wa Arusha kati ya wengi walio waponza kwa kuwajaza ujinga? Wanachoongelea sasa ni kukumbatia ubeberu na ushoga maana ndiko ulaji uliko.
 
Hapa ni kimoja tu wandugu tumpe Lissu huyu bwana ataokoa ya hovyo mengi ambayo yanakuja kuanzia 2021 hadi 2025, wengi watajuta hapa.
Hali itakuwa mbaya zaidi Kama tukirudia makosa
 
hvi ni kweli haya maneno uliyoyaandika?
 
Uwiii sasa itakuwaje mi nahama nchi 😅🏃
 
Aisee..
Ngoja nikae kimya..
Huwenda Ricin imehusika kulingana na maelezo yako..
 
Huu ndio ukweli.Sio tu kuwa waliobaki hawawezi kumfunga gavana aliyeko kilingine, ila pia kwa sababu mbalimbali hawana msimamo wa kuwafanya wathubutu kumyooshea kidole ...
 
Kuwafundisha siyo hoja,
Hoja ni kauli yenye mamlaka
 
Watu wanamchukulia kikwete mwepesi sana lakini huyu mzee Ni mtu mzito sana sana sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oh basi sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…