Mkapa kaondoka, je nani atamfunga paka Kengele?


JK inabidi aibebe mikoba iliyoachwa na hayati Mkapa vilivyo.

Nafasi ya marais wastaafu katika nchi yoyote iliyostaarabika haiwezi kubezwa hata kidogo.

Ni kwa minajili hiyo nyuzi kama hizi zimewahi kuwepo:

Waraka wa wazi kwa Marais wetu Wastaafu kuhusiana na hali ya Corona nchini

Apumzike kwa amani mzee wetu rais mstaafu Mkapa.
 
Watu wanasahau mapema wakati mwl anafariki watu walikuwa na hofu nchi haitakuwa salama,sasa wamehamia kwa Mh Mkapa hii nchi itakuwa salama maana mifumo yetu ya usalama iko vizuri...ondoeni Shaka wanatanzania
kwakweli maana JK kamfundisha Mabeyo apo monduli
 
Mwinyi na Kikwete hawana influence yoyote kwa Marais wa nchi hii?
 
Hii ni uchambuzi tu, siyo FACT. Mengi niliyoandika nimetoa kwenye vyanzo mbalimbali ninavyoviamini, ni wewe mwenyewe kuchanganya na zako.
mi tangia juzi nilikuwa nawaza kuanzisha Uzi Kama huu sema we umeniwahi

Halina Ubishi kuwa aliyekuwa na uwezo wa kumzuia Magufuli ku extend zaidi ya 2025 Ni Mkapa

Yeye ndio Rais pekee aliyelipinga hili waziwazi zaidi ya Mara moja

Waliobakia hawajawahi kukemea, Mwinyi ndio alimuunga mkono na Kikwete hajawahi kulizungumzia

Mwinyi Ni bendera fuata upepo najiuliza sijui hata alikuwaje Rais
 
Mkapa mwenyewe hakuweza kumfunga paka kengele.

Tuache stories.
 

Mkuu umeongea ukweli 110%.

Ila Magufuli alichomfanyia Mkapa ni exactly Mkapa alichomfanyia Nyerere. What goes around comes around.
 
Alisahau, msamehe bule.. ila mwembe chai na pemba amejutia.
Hivi kwenye kile Kitabu alicho andika Marehemu aliwaomba msamaha wale aliowaita Malofa siku ile ya Kampeni pale Jangwani?.
 
Reform kubwa imefanyika
 
Kwa mliosikiliza speech ya Magufuli leo kwenye hafla ya kumuaga Mkapa, sasa mtakua kidogo mmeelewa huu uzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…