Mkasa wa Afande Mwasifiga alivyopoteza kazi baada ya kubishana na hayati Rais Magufuli

Mkasa wa Afande Mwasifiga alivyopoteza kazi baada ya kubishana na hayati Rais Magufuli

Sijachangia kimahaba!!

Kama mshindi ni afande, mbona hajarejeshwa kazini?

Amri ya magufuri bado ipo palepale pamoja na kua hatuko nae!!

Afande alikua na tuhuma za unyanyasaji lakini bado akaongea na mkuu wa nchi kama anaongea na mtoto au afande mwenzie walie lingana cheo!!

Toa mahaba mahaba halafu uniambie wewe na mwanao hamna mipaka ya mahusiano?

Boss wako tu hata kama ana miliki mashine moja tu ya kusaga nafaka, huwezi kumjibu kama unavyo jibizana na mshikaj wako mnaecheza na draft hapo mashinen. Leo ndio uje umjibu mkuu wa nchi kama unavyo jisikia?? Hata kama umemzidi umri bado boss ni boss tu utamwita baba/ mzee huku umekusanya mikono na kushusha kichwa chako chini.

SIKU NYINGINE UNAPO CHANGIA JITAIDI KUPUNGUZA MAHABA KUNA WEMGINE HATUFUNGAMANI NA UPANDE WOWOTE TUNAJIKITA KWENYE MAADA TU!
Bado mshindi ni Afande Mwasifiga!! Yule bwege wenu mlikuwa mnamuona kama mungu wenu. Lakini Afande Mwasifiga akamuona kama kinyago tu na ndiyo maana akamjibu kunya. Hiyo tu inatosha .
 
Leo nimekumbuka mkasa mmoja uliotokea enzi ya awamu ya tano!

Ilikuwa ni Julai 16 ya mwaka 2019 Jumanne tulivu tu ndani ya jiji la Mwanza, ghafla Gereza Kuu la Butimba likapata ugeni wa Amiri Jeshi Mkuu, Rais Magufuli.

Basi baada ya maofisa wa juu kutonywa kuwa Rais angeweza kufika pale, wakajipanga kumpokea.

Punde si punde, hayati Magufuli akawasili na bila kupoteza muda akaomba kuongea na wafungwa ili asikie matatizo yao kama ilivyoada yake.

Wafungwa walifurahi sana kumuona Rais, basi wakaambiwa watoe kero zao. Wakazungumza wengi mpaka ilipofika kwa mfungwa mmoja aliyeamua kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

Mmoja ya wafungwa waliopata nafasi ya kuongea na hayati Magufuli alikuwa ni Kalikenye Thomas Nyamboge, mfungwa mwenye ulemavu wa ngozi, aliyekuwa anatumikia kifungo cha Miaka 30 jela.

Mfungwa Kalikenye yeye akatoa kero yake kuhusu Afisa Usalama wa Gereza hilo, Afande Mwasifiga kuwa anashirikiana na wafungwa wengine kwa kuwapa simu waongee na watu wa nje ya Gereza kinyume na utaratibu uliowekwa lakini pia anashirikiana na baadhi ya wafungwa wenye hela kuingiza simu kwenye Gereza hilo la Butimba.

Mfungwa wa miaka 30 Jela, Bwana Thomas Kalikenye akaendelea kumsagia kunguni Afande kuwa, msako ukipita simu hazionekani na wao akina Thomas wasiohusika na kuingiza simu wanamwagiwa vitu vyao kama vile Karanga, Sukari, Sabuni na saa nyingine vinachukuliwa kwa nguvu na team ya Afande Mwasifiga.

Ghafla hayati Magufuli anabadilika na kuuliza yuko wapi huyo Afande Mwasifiga? Afande anatokea na kupiga saluti na kuanza kujibu shutuma.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Afande Mwasifiga anaanza kubishana na Rais Magufuli kuhusu suala la uwepo wa simu kwa wafungwa katika Gereza la Butimba.

Afande Mwasifiga katika ubishani wake akamuambia Rais Magufuli, “huyu alitaka kuniinua” Maneno hayo yalimchefua sana Rais.

Magufuli akamwambia afande kuwa”inaonekana una dharau sana wewe” akawa ameshakasirika huku wasaidizi wa Rais wakimtonya Afande Mwasifiga aombe msamaha kwa Rais. Kweli akaomba msamaha huku akipiga saluti, lakini haikusaidia kitu.

Kama utani Rais Magufuli akamwambia ninaweza nikang’oa hizo nyota zako hapo (huyu Afande alikuwa na nyota mbili).

Basi Rais akaachana nae akamalizia kuongea na wafungwa kama alivyopanga ana akatoa agizo kwa Mkuu wa Gereza la Butimba, ole wake mfungwa yoyote aliyetoa kero anyanyaswe, basi atachukua hatua mara moja. Akamaliza akaaga akaondoka zake.

Usiku wake, Afande Mwasifiga akapokea maelekezo kuwa ameondolewa Gereza la Butimba na kupewa uhamisho wa kwenda Ukerewe.

Sambamba na hilo, akavuliwa nyota yake moja alitoka kuipata siku chache kabla ya kubishana na Rais. Hivyo basi akabaki na nyota moja tu badala ya mbili kama hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi yake.

Kama haitoshi, baada ya miezi sita akiwa katika kituo chake kipya cha kazi, akastaafishwa kwa maslahi ya umma na utumishi wake ndani ya Jeshi la Magereza ukawa umefikia kikomo.

Ikumbukwe alipewa miaka mitano ya ziada jeshini baada ya kupewa nyota ya pili kabla ya kuipoteza nyota hiyo kutokana na kubishana na Rais.

Ukawa ndio mwisho wa Afande Mwasifiga, aliyepata kuwa Mkuu wa Usalama ndani ya Gereza la Butimba na waliopata kufanya nayr kazi wanakwambia alikuwa ni mjivuni, kiburi kwelikweli.

Kwasasa amerudi kwao Mbeya akiwa ni mkulima akiendeleza maisha baada ya kustaafishwa kwa maslahi ya Umma!View attachment 3164402
Upuuzi tu na huyu magufuli ni mpuuzi tu
 
Bado mshindi ni Afande Mwasifiga!! Yule bwege wenu mlikuwa mnamuona kama mungu wenu. Lakini Afande Mwasifiga akamuona kama kinyago tu na ndiyo maana akamjibu kunya. Hiyo tu inatosha .

Afande alisahau nani aliyeshika Mpini ,aliyepoteza hapo ni afande nina uhakika kuna baadhi ya maslahi yake yaliondolewa ,kustaafishwa kwa maslahi ya umma means kufukuzwa kazi.
 
Unaweza kujitapa sana kwamba unaweza kumvua mtu manyota wakati wowote lakini huyo unayemvua manyota akaendelea kuishi na wewe na tambo lako lote la kumvua manyota ukafa ukamuacha.

Cheo ni dhamana, tusipende sana kujimwambafy kwa dhamana ya cheo.

Magufuli angeweza kumsikiliza Afande na kuamua kesi kwa busara bila kujimwambafy kwamba anaweza kumvua manyota.
What if kama wote walikiwa na mihemko na msongo wa mawazo ?
Huyu msongo wa mawazo ya kuendesha nchi, huyuy mihemko na msongo wa mawazo wa kuchomwa utambi wa ugali wake na mfungwa?
 
Rais akisema mbona manyasi yameota sana
Hapo haulizi bali ni amri hayo manyasi yapaliliwe, Mpo hapo?

Aliposema naweza nikaziondoa hizo nyota maana yake ilikuwa ashushwe cheo
Daa naikumbuka hiyo ziara
Inategemea na sehemu!

Kuna siku Magu alimwambia aliyewahi kuwa Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jonh Mbungo,kwamba unajua naweza kung'oa hizo nyota zako!

Mkasa ulikua kwamba,Magu alipewa taarifa za ujenzi wa nyumba za TAKUKURU kuwa zipo chini ya kiwango,lakini Mkuu wa TAKUKURU hana taarifa na akawa anambishia Magu! Hadi Magu anafariki jamaa alikua bado Mkuu wa TAKUKURU na still alikua bado na cheo chake cha one star General
 
Mtu kama kabarikiwa jambo flani kwa nini ukweli usisemwe? Ww ambae haukuwehuka umelifanyia nini taifa hili..chuki zako binafsi kwa hayati usipandikize kwa wengine...
Kusema ukweli si kosa kosa ni kuusemea ukweli ambao uliaminishwa kuwa ni ukweli bila wewe kujiridhisha kwa kutumia akilizako kuwa ni kweli.
Vipi kuhusu alivyotembelea bandarini na kuokota vichwa vya treni ukweli wake ni upi?
Je ukweli wa makinikia yaliyozuiliwa bandarini ukweliwake uliishia wapi?
Sijawahi kuwa na chuki nae ila sipo kwenye kundi la watu ambao wanaamini mazingaombwe.
 
Inategemea na sehemu!

Kuna siku Magu alimwambia aliyewahi kuwa Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jonh Mbungo,kwamba unajua naweza kung'oa hizo nyota zako!

Mkasa ulikua kwamba,Magu alipewa taarifa za ujenzi wa nyumba za TAKUKURU kuwa zipo chini ya kiwango,lakini Mkuu wa TAKUKURU hana taarifa na akawa anambishia Magu! Hadi Magu anafariki jamaa alikua bado Mkuu wa TAKUKURU na still alikua bado na cheo chake cha one star General
Kuna vyeo ili vishuke vikao kama 30 lazima vikaliwe wacha hizo nyota mbili tena za magereza
 
Huu uzi una uongo mwingi hakuondolewa nyota moja ingawa alihamishiwa Ukerewe, hata kama angeondolewa nyota moja kisingelikuwa kigezo cha kustaafu maana umri wa kustaafu kwa nyota moja na mbili ni sawa.
Mwasifiga hakustaafishwa umri wake wa kustaafu ulikuwa umefika, alistaafu kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Lakini pia nitoe elimu kidogo juu ya Afisa usalama wa gereza, Afisa usalama ni mtu ambae huangalia usalama wa gereza na kuhakikisha gereza lipo salama muda wote, Kazi kubwa ni kuhakikisha vitu ambavyo haviruhusiwi kama simu, silaha na hata haviingii ndani gereza na hata vikiingia inabidi ahakikishe vinakamatwa.

Maafisa usalama ni maadui wa wafungwa na mahabusu, kwa sababu huwa wanahusika mara kwa mara kukamata mali zao, ndio maana walimsagia Mwasifiga kunguni kwa Magufuli.
Kama kweli Afande angelikuwa anayafanya yale aliyoyasema yule mfungwa hakuna mfungwa angelalamika, kilio cha wale wafungwa kilimaanisha wamebanwa haswa.

Mengineyo mkubwa hakosei.
 
Magufuli kajitapa kuvua watu manyota lakini na yeye kavuliwa uhai hakuweza kuzuia kuvuliwa uhai.

Cheo ni dhamana, usinyanyase watu kwa cheo.

Najua wewe ngumbaru huwezi kuelewa somo, uwezo huo wa juelewa huna kwa sababu wewe guluguja huna ubongo wala uti wa mgongo.

Ila kuna watu wataelewa.
Hapa ndipo nawaona Watu wanaokanusha uwepo wa Mungu ni Mtaahira wanaojaribu kuidanganya Akili Zao sasa huyu anasema Magufuli Amevuliwa Uhai na nani sasa huyo anayevua watu uhai?Hawa ni machizi wanaovaa suti.
 
Back
Top Bottom