Sema hizo codes umezificha ,ungetaja tu hata jina la kanisa but ndo hivo ukitaja hilo kanisa huyo jamaa atajulikana kwa story ilivyoenda.
Hapo kinachoonekana ni nguvu ya Mungu vs Nguvu za giza au nguvu za giza zinapambana zenyewe.
Huyo jamaa yako amekuwa mtu wa kuconnet dots either kwa hofu zake na hisia tu za kibinadamu lakini mambo kama hayo yapo tunakutana nayo na hatutulii akilini tunalindwa tu na ulinzi wa Mungu
♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
UPDATE 22/04/2020
1 SWITCH ZA TAA ZA PARKING KWENYE JENGO ANALOISHI KUTOKUWA ZIMEWASHWA KWA JUMAPILI MBILI MFULULIZO, UKIHUSIANISHA NA SWITCH ZA FENI ALIZOKUTA ZIKITEMBEA KANISANI, PAMOJA NA ASKARI WA SANITIZER
Ikumbukwe kuwa Jumapili (ya Pasaka) ya siku ambayo alikuta Kanisani kuna feni zinatembea halafu akaenda akazima switch zake, kule nyumbani alikotokea kwenyewe nako aliacha amewasha switch za kwenye parking, ambazo nazo alizikuta ziko OFF. Jumapili hiyo alihudumiwa sanitizer na Mlinzi A, na ilikuwa mara ya 3 mfululizo kupata huduma kutoka kwa mtu huyu, kwenye siku za Ibada kuu ukiongeza na zile za Ijumaa Kuu, na Jumapili ya wiki kabla ya Jumapili ya Pasaka
Lakini pia vilevlie, Jumapili hii iliyopita (wiki jana), switch za kwenye parking alizikuta tena zikiwa OFF, lakini safari hii hakuziwasha, aliziacha kama alivyozikuta. Alipofika Kanisani akapokelewa na Mlinzi mwingine nje ya gate, akiwa anajiandaa kumpulizia sanitizer na hatimaye malumbano kidogo baada ya kuingia ndani ya gate la Kanisa
Yeye hypothesis yake kwenye matukio haya anadai kuwa kama ifuatavyo:
Inaonyesha KAMA alivyoweka ON switchi za kwenye parking asubuhi ya Jumapili ya Pasaka, halafu tena akaenda akaweka OFF switch za feni kule Kanisani, ambazo kwa sasa yeye anadai kuwa ziliachwa ON makusudi, kitendo cha yeye kutorudia tena kuziweka ON switch za kwenye Parking ya jengo analoishi Jumapili ya wiki jana, ziliashiria kuwa inawezekana tayari ameshajenga dhana kuwa kitendo cha kuwa anakuta switch zimeachwa katika position ambayo siyo sahihi halafu unazirekebisha, ni kitendo malicious, na si cha bahati mbaya. Kwa hali hiyo siku ya Jumapili hiyo aliyoacha kuweka ON switch za kwenye parking, inaonyesha KAMA kuna information zilikuwa relayed kule alikokuwa anaelekea, yaani Kanisani, kwamba jamaa ameshastuka na issue ya switch. Na kwa sababu switch alizowasha Kanisani zilikuwa connected na issue ya Sanitizer, ikaonekana sasa kuwa kuna uwezekano asubuhi ile angeweza kutoa resistance namna ya kupokea huduma hiyo ya sanitizer, pindi atakapokuwa amefika Kanisani. Kwa hiyo mkakati ukapangwa sasa wakati akiwa bado yuko njiani kwamba:
Mlinizi A asitumike tena siku hiyo kumpa huduma ya sanitizer kwa sababu kuu mbili
- amekuwa akimpa kwa mara 3 mfululizo, na siku hiyo ingekuwa mara ya nne.
- kulikuwa na uwezekano wa mhudumiwa kutoa upinzani wa huduma hiyo, na kama mhudumu angekuwa yuleyule, pengine upinzani ungekuwa mkubwa zaidi ikiwa ni pamoja na maswali mengi
Kwa hiyo inaonyesha KAMA mamlaka zikawa zimeafiki mtu mwingine ajiandae kwa kumpa huduma ya Sanitizer na kwa kumfuata nje kabla hajaingia ndani ya gate ili kama pengine kutatokea mgogoro, umalizikie huko huko nje ili waliomo ndani ya gate wasije wakaunusa.
Mbali na hilo, kwenye sehemu ya parking ,hivi karibuni kumewekwa Kamera. Kwa hiyo inaonyesha pia KAMA mhudumu wa sanitizer alishauriwa hivyo ili kukwepa uwezekano wa tukio lake na mhudumiwa, kukamatwa kwenye Kamera, kwa sababu kama nilivyosema hapo awali kuwa, baada ya kuwa ameingia ndani, aligundua kuwa kulikuwa pia na ndoo ya maji yanayotiririka. Assuming angeingia ndani halafu tukio likawa limekamatwa kwenye Kamera, la mhudumu anampelekea mtu sanitizer halafu mhudumiwa anaanza kuuliza maswali ya kumhoji mhudumu, mojawapo likiwa tuseme KWA NINI KILA MARA MUNANILETEA SANITIZER WAKATI LEO YAPO PIA MAJI YANAYOTIRIRIKA? ,…., na maswali mengine ambayo yangeweza kufana na hayo
Kama hypothesis hii ya switch haitakuwa sahihi, uwezekano mwingine ni kuwa Jumapili ya wiki jana, switch ziliwekwa OFF ili kuwe na giza kwenye parking, kuruhusu ufunguaji wa kioo cha gari upande wa passenger seat, ambalo mhusika hakuwa ameliacha wazi. Uhakika alionao ni kuwa kioo hicho kilifunguliwa gari likiwa nyumbani, alfajiri ya Jumapili, na kwa sababu huwa anaondoka ikiwa bado giza kidogo, na pia Kanisani si mbali sana kiasi kwamba anaweza akahitaji kukimbia mwendo mkubwa, kioo hakukiona hadi anafika Kanisani na kupaki gari na kuiacha.
Alternatively, hypotheses zote mbili zinaweza pia ku-apply, kwamba mambo hayo yote mawili yanaweza kuwa yalikuwa yamekusudiwa kutendeka kwa pamoja.
2.
TRIP ZA KUTOKEA NYUMBANI NA ZILE ZA KUTOKEA OFISINI KUELEKEA KWENYE IBADA, NA UHUSIANO WAKE NA SANITIZER
Anadai kuwa amekuwa akipata huduma ya Sanitizer pindi anapokuwa anaelekea Kanisani kutokea nyumbani na kwa siku ambazo ni za Ibada Kuu tu. Hapati huduma hiyo akiwa anatokea ofisini kuelekea kwenye Ibada za katikati ya wiki ambazo huwa zina kawaida ya kuanza baada ya saa 10. Yeye hapa anadai kuwa kunaweza kukawa na mambo makuu mawili ambayo ni:
- Inaonyesha KAMA huwa anatoa upinzani mkubwa kwenye Ibada Kuu hasa zile zinazoanza asubuhi kwa sababu huwa anafika Ibadani asubuhi akiwa anatokea nyumbani, na akiwa haja-interact na mtu yeyote siku hiyo. Mbali na hivyo, huwa anaanza kwa maombi kwanza pamoja na kusoma maandiko matakatifu, alfajiri kabla hajanza safari ya kuelekea Kanisani. Kwa hiyo akiwa anatokea nyumbani kuelekea Ibadani, inalazimika afanyiwe udhibiti wa kipekee, na hivyo huduma ya sanitizer, anapokuwa tu amefika Ibadani akiwa anatokea nyumbani
- Inaonyesha pia KAMA huwa hatoi upinzani mkubwa kwenye Ibada za katikati ya wiki, anapokuwa ametokea ofisini, au kama anatoa basi bado kunakuwa na nafasi ya kuudhibiti kabla ya siku ya Ibada Kuu, yaani Jumapili. Aidha kunaweza pia kukawa na mtandao saidizi mwingine ofisini kwake ulio kinyume naye, ambao huwa unahakikisha kuwa umemdhibiti kabla muda wa Ibada kuwa umefikakiasi kwamba huwa anaondoka ofisini akiwa tayari hana ule upako wa kutoa upinzani unaoweza kuleta athari. Kwa hali hiyo kwa siku kama hizi, inakuwa hakuna haja ya kumpa huduma ya Sanitizer, itapelekea huduma hiyo iwe monotonous kwake halafu ipelekee aje aigomee kwenye siku ambayo ni ya muhimu huko mbele ya safari
3 COINCIDENCE INAYOMHUSU KIONGOZI ALIYESEMEKANA KUWA NI MHUSIKA WA MANUNUZI YA CORONA
- Mhusika anadai kuwa baada ya kupuliziwa Sanitizer kwa lazima, alipitiliza moja kwa moja mpaka men’s room, akanawa kwa sabuni na maji yanayotiririka. Kuna bomba moja tu la maji kwenye chumba hicho
- Baadaye alirudi ofisini kwa walinzi, akawa anahoji mawili matatu kuhusiana na baadhi ya mambo ambayo alikuwa anayaona hayaendi sawa, mojawapo ikiwa ni kujua kama Sanitizer hizo zimewekwa wakfu kwa ajili ya matumizi ya Kanisani
- Hatimaye mtu mmoja alijibu akasema muulize fulani (akamtaja kiongozi ambaye inaonyesha ndiyo mhusika wa manunuzi ya vifaa hivyo)
- Baadaye wakati Ibada inaendelea, mhusika alitoka tena kuelekea men’s room. Alipofika huko akamkuta mtu aliyetajwa kuwa mhusika wa manunuzi, men’s room, akiwa ananawa kwenye bomba la hilo la maji. Umbali kutoka pale lilipo bomba hilo na pale alipokuwa amekaa kiongozi mhusika wa manunuzi wakati wa Ibada, hauzidi mita kumi na tano, na umbali kutoka kule alikokuwa mhusika wa tukio hadi kufika kwenye bomba hilo, shortest distance inaweza kuwa mara 3 ya umbali huo, lakini pia ali-opt kutumia njia mbadala kukwepa kuwabughudi watu kwa sababu Ibada ilikuwa inandelea, na njia aliyotumia inaweza kuwa na urefu wa takribani mita 60
- Mhusika wakati anatoka men’s room, (kiongozi alikuwa tayari ameshaondoka) alirudi kwa kutumia njia ile ile aliyoijia. Njiani tena akakutana na binti wa karibu sana na kiongozi aliyetajwa, yeye naye alikuwa anaelekea kule alikokuwa anatoka mhusika. Configuration ya sehemu ile namna ilivyokaa ni uchochoro ambao uwezekano wa mtu mwingine kumuona mwenzake ni lazima uwe maeneo yale na si Kanisani au kwingine. Kwa hiyo hayupo mtu ambaye anaweza kuwa alituona wakati tunapishana, labda satellite iliyo juu!
Scenerio hii nayo ilionekana kama rare coincidence kwake, japo anakiri kuwa inaweza kuwa haina maana yoyote!
Nitarudi kwa ajili ya sehemu ya mwisho ambayo mojawapo ya habari zake ni hii hapa chini, mbarikiwe tena na Bwana
4.
MAMBO MENGINE AMBAYO HAYAHUSIANI MOJA KWA MOJA NA TUKIO LA MHUSIKA, LAKINI AMBAYO ANASHAURI KAMA KUNA UWEZEKANO, UONGOZI UWEZE
Anadai kuwa pembezoni mwa nyumba ya Ibada wanayoabudia kwa sasa kuna chamber za majitaka umbali wa si zaidi ya mita moja, upande wa kushoto wa Kanisa. Kanisa ni Banda ambalo halina kuta, na Kanisa jipya bado liko kwenye ujenzi. Chambre hizi zimekuwa zikiachwa zinafurika na kutoa nje maji yaliyochanganyikana na kinyesi, halafu maji hayo yanaanza kutirirka kupitia njia ambayo waumini huwa wanapita na watoto kucheza. Kwa mvua zilizonyesha hivi karibuni, anadai hakuona mafuriko hayo, ila pia hana taarifa kama chemba hizo zimefanyiwa kazi, ila pengie hazikuvuja tu kwa bahati nzuri. Pia anadai kuwa kuna mtu alimdokeza kuwa mapepo huwa yana uwezo wa kukaa hata kwenye harufu ya kitu tu, au kwenye kitu kinachotiririka, kama nilichokitaja
NITARUDI