MAELEZO MUHIMU SANA YANAYOHUSIANA NA MKASA UNAOWAHUSU WATU HAWA WAWILI AMBAO MHUSIKA AMEWAHI KUWAONGELEA PIA KWENYE POST HII HAPA #994
NI MAELEZO AMBAYO MHUSIKA ALIKUWA AMEAMUA KUTOKUYALETA HUMU JUKWAANI ISIPOKUWA HATIMAYE AMELAZIMIKA UKIZINGATIA MIENENDO YAO
Wa kwanza ambaye ni mrefu zaidi ni ndugu wa damu wa mhusika; binamu yake na mhusika; ni mtoto wa shagazi yake; huyu tumwite BNM. Yule mwingine
wa pili ni shemeji yake na mhusika; huyu tumwite SHMJ
BAADHI TU YA MATUKIO WALIYOWAHI KUHUSIKA HAWA WATU WAWILI NA AMBAYO MIONGO/ MIAKA MINGI NYUMA, MHUSIKA ALIWAHI KUYAONA YAKIWA KAMA NI MATUKIO YA KAWAIDA ILA KWA SASA ANA MTIZAMO TOFAUTI KABISA; BAADA YA KUWA AMESHUHUDIA MATUKIO MENGINE MUAMBATA NA HAYO
TRIGGER YA MATUKIO YOTE MUHIMU INAANZIA JUNE 1989 (MIKA 33 ILIYOPITA)
June 1989 binti ambaye ni dada yake na mhusika akarudi nyumbani likizo kutoka shule moja ya sekondari iliyoko Mororgoro
- Binti alikuwa anasoma sekondari kidato cha nne; kwa hiyo kufikia Novemba 1989 binti alikuwa anahitimu masomo ya kidato cha nne na kweli muda huo ulipotimu, alifanikiwa kuhitmu
- Kwenye shule hiyo hiyo aliyokuwa anasoma binti, alikuwepo pia binamu mwingine mdogo wake na BNM; huyu tumwite BNM-1
- Hawa BNM na BNM-1 wamezaliwa; wamezaliwa baba mmoja mama mmoja
- Mzazi wao na akina binamu hawa wanaotajwa humu ambaye ni shangazi yake na mhusika; mzazi huyu amezaliwa baba mmoja mama mmoja na baba yake mhusika au binti
- Tofauti ya umri kati ya BNM na BNM-1 mtu na mdogo wake ni exactly miaka 20
BAADA YA KUMALIZA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE; BINTI ARUDI NYUMBANI AKIWA NA UJAUZITO ULIOPELEKEA AJIFUNGUE MWISHONI MWA MWEZI WA TATU MWAKA 1990
Baada ya binti huyu kumaliza kufanya mitihani ya kumaliza kidato cha nne, binti alirudi nyumbani akiwa na ujauzito wa
si chini ya miezi sita na hivyo kufanikiwa kujifungua salama kitoto mwishoni kabisa mwa mwezi wa tatu mwaka 1990
Katika hali ya kawaida; kwa ujauzito mkubwa wa kiasi hiki, binti huyu wa sekondari alitakiwa kufukuzwa shule na asingefanikiwa kuhitimu masomo yake hiyo Novemba 1990. Hata hivyo kitu cha pekee kilichotokea ni kwamba alifanikiwa kuhitimu masomo yake pasipo tatizo lolote
Ujauzito huu ulitungwa mwishoni mwa mwezi wa 6, muda mfupi kabla binti hajaondoka kurejea masononi
Anachokielewa mhusika mpaka muda huu ni kwamba ujauzito huu uliopangwa makusudi utokee katika kipindi hicho ulichotokea, na mtandao wake ulikuwa unahusisha baadhi ya ndugu kutoka kwenye familia ya binti pamoja na mamlaka za shule ya sekondari aliyokuwa akisoma huyu binti
Hypothesis aliyonayo mhusika mpaka muda huu ni kwamba mtoto aliyezaliwa hakutakiwa kuishi ila kwa bahati nzuri yupo hadi leo na ana mke na watoto wawili
MAELEZO MAFUPI SANA YA UTANGULIZI KUHUSIANA NA MTOTO HUYU ALIYEZALIWA MWISHONI MWA MWEZI MARCH 1990
SABABU HASA ZINAZOPELEKEA MHUSIKA KULETA TAARIFA ZAKE HUMU JUKWAANI NA AMBAZO KWA KIASI KIKUBWA ZINAHUSIANA PIA NA BABA YAKE MZAZI (SHMJ) PAMOJA NA BNM
Sababu moja kubwa inayopelekea mhusika alete taarifa za mtoto huyu humu jukwaani muda huu ni kwamba mtoto huyu hakutakiwa kuwepo kwa sababu maisha yake yanabeba matukio ambayo hayakutakiwa kujulikana na watu wengine
Aidha mtoto huyu alitakiwa aishi ILA MHUSIKA ASIISHI kwa sababu ya ule uwezekano wa kwamba siku mhusika akija kugundua siri iliyobebwa na maisha ya mtoto huyu, siri hiyo itakuwa wazi na lazima kuna shida kubwa itatokea mahali
Kwa hiyo Plan A iliyokuwepo mwaka 1990 ilikuwa ni wote mhusika na mtoto wasiishi; na Plan B ilikuwa ni aidha mmoja wao tu aishi na si wote wawili
Kwa hiyo mimba hiyo ilitungwa kaika muda huo ili wakati fulani ije ilelewe kwenye muda na majira ambayo mhuska naye angekuwepo nyumbani kwa sababu yeye naye pia alihitimu kidato cha nne mwaka huo huo wa 1989
Kwa hiyo mhusika naye pia alikuwepo nyumbani kuanzia Novemba 1989 hadi mwanzoni mwa Julai 1990
Kwa bahati nzuri watu hawa wote wawili wapo isipokuwa yule mwingine AMETUMIA KARIBIA 90% YA MAISHA YAKE JELA NA MARA ZOTE IKIWA NI KWA MBARAKA MKUBWA KUTOKA KWA BABA YAKE MZAZI, YAANI SHMJ
Hivi karibuni APRIL 2022 alitakiwa pia kuwa ameshaenda JELA isipokuwa hekima ya Askari kwenye kituo kimojawapo cha Polisi jijini Mwanza kilimsadia abaki uraiani
Siyo kwamba mtoto hafanyi makosa, ni kweli wakati mwingine anafanya makosa isipokuwa kwa
zaidi ya 90% amekuwa akitengenezewa au kutegeshewa mazingira rutubishi ya kufanya makosa
Maelezo ya kina kuhusiana na mtoto huyu yatafuata baadaye.
Kwa sasa turudi kwanza kwa wanafunzi wawili mtu na binamu yake waliokuwa wanasoma shule moja huko Morogoro wakiwa wamefuatana madarasa
……………………….inaendelea