Life starts at 45
JF-Expert Member
- Sep 22, 2015
- 998
- 987
mkuu nipo naingojea hapa kabla ya kulalaPlease stay tuned for today's update
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mkuu nipo naingojea hapa kabla ya kulalaPlease stay tuned for today's update
kiongoz naanza hivyo kuisomaUPDATE THURSDAY 04/06/2020
RARE COINCIDENCE ILIYOTOKEA KATI YA SIKU ZA JUMAPILI YA TAREHE 24/05/2020 NA JUMATANO YA TAREHE 27/05/2020; NA AMBAYO INAMHUSISHA MR X TENA
Inaendelea………………..
MAELEZO KUHUSIANA NA MATUKIO YANAYOUNDA COINCIDENCE YENYEWE
Mhusika wakati anarudi kutoka duka kubwa pale Savei, alikuta watu wawili kwenye kituo cha daladala, karibu kabisa na pale alipokuwa amepaki gari lake
Hiyo siku ikapita, ambayo ilikuwa ni J2 ya tarehe 24/05/2020
- Walikuwa mama na mwana, na ambao anafahamiana nao wote kama alivyoeleza hapo juu
- Mara ya mwisho kumuona mwana ilikuwa mwaka 2004, na alikuwa mtoto mdogo asiyezidi miaka takriban mitano (5)
- Mhusika alikuwa pia rafiki wa binti huyu katika kipindi cha utoto wake
- Mknononi mwake, mhusika alikuwa amebeba mfuko ambao ndani yake kulikuwa na Soda pamoja na Biscuits, bidhaa ambazo alinunua kutoka duka kubwa siku hiyo ya J2
- Baada ya mhusika kuwauliza wanaelekea wapi, mama mtu alieleza kuwa wanaelekea Changanyikeni kupitia Utawala, UDSM
- Yaani wakifika utawala wanashuka, halafu wanapanda daladala nyingine tena kutokea pale kuelekea Changanyikeni
- Uelekeo wao ulikuwa ni sawa na ule wa mhusika, japo mhusika alikuwa karibu zaidi na nyumbani kwake
- Mhusika hakuona mantiki ya kuwachukua kwenye gari lake kwa sababu kwa ratiba aliyokuwa nayo siku hiyo, asingeweza kuwapeleka mpaka Changanyikeni
- Vilevile haikuwa na mantiki sana kuwachukua hadi Utawala halafu akawaacha pale ili wapande tena daladala za kwenda changanyikeni
- Kwa hiyo mhusika aliamua kuwaaga, akawaacha pale wakiwa wanasubiri daladala ambayo ilitarajiwa kwenda kuwaacha Utawala UDSM.
J3 kesho yake muda wa asubuhi, mhusika alibahatika kupishana kwenye korido na Mr X, ambaye alishukuru kwa zawadi.
Siku hiyo hiyo tena kwenye muda wa baada ya saa 10 jioni, mhusika akabahatika kumuona kwa mbali mke wa Mr X, yaani Mrs X akiwa anaingia ofisini kwa Mr X
Wakati anatoka ofisini, akawakuta wawili hao bado hawajaondoka, walikuwa wamepaki gari yao pembeni mwa gari la mhusika, upande wa dereva wa gari la mhusika, na Mrs X alikuwa amekaa mbele upande wa passenger seat ya gari lao. Alipofika aliwasalimia na hatimaye Mrs X naye alimshukura kwa zawadi za watoto. Baada ya hapo mhusika aliamua kumsimulia Mrs X kwa kifupi sana kilichopelekea anunue zawadi hizo.
- Huwa ni mara chache sana kwa Mrs X kuonekana ofisini kwa mumewe, na mhusika hakumbuki ni lini mara ya mwisho alimuona ndani ya jengo hilo
- Baada ya muda, mhusika aliwaona tena wawili hao wakitoka ofisini tayari kwa kuondoka, kuashiria kuwa siku ya kazi ilikuwa imeisha
- Mhusika naye pia alikuwa katika harakati hizo hizo za kuondoka, lakini yeye ilimchukua takribani dakika 15 mbele ya wawili hao, ndiyo akawa amekamilisha kila kitu na hatimaye kufunga ofisi na kuondoka
J3 hiyo (ambayo sasa ni wiki jana), mhusika alikuwa amepanga kuhudhuria Ibada ya maombi Kanisani, yaliyokuwa yanaanza saa 11:00 kamili na kuisha saa 1:00 kamili usiku. Hata hivyo, mhusika, alikuwa amepanga kuwa angeondoka Kanisani hapo saa 12:30 siku hiyo, yaani kabla ya Ibada kuisha. Hii ni kutokana na matatizo ya ki-usalama ambayo alishawahi kukumbana nayo Kanisani hapo kipindi cha nyuma, na ambayo yalimlazimu awe na ratiba ya kutokuendelea kukaa Kanisani hapo baada ya saa 12:30 kuanzia kipindi hali hiyo ilivyojitokeza, hadi leo (hili nalo ni swala jingine ambalo linahitaji maelezo ya kipekee, ila Kiongozi Mkuu analijua kwa kina kwa sababu waliwahi kuliongelea siku walipofanya mkutano wao ofisini kwa kiongozi huyo)
Kwa hali hiyo, kitendo cha wawili hao kuwakuta bado hawajaondoka kwenye parking, kilimsababisha mhusika aanze kurudi nyuma kuona kama kunaanza kujitokeza pattern yoyote ya matukio, na mambo kadhaa aliyoanza kuyajadili kwa haraka haraka kichwani ni kama yafuatayo
Kwa hiyo, kwa upande mwingine tena, ilionyesha pia kama wawili hao
- Ni mara chache mno kuwakuta Mr X na mhusika wamepaki gari zao ubavu ubavu, na inapotokea Mr X mwenyewe ameamua kufanya hivyo, basi MARA ZOTE lazima kuwe na jambo la kipekee. Hii inamanisha pia kuwa MARA ZOTE mhusika huwa anakwepa sana kupaki gari lake ubavuni mwa gari la Mr. X
- Mhusika alishamsoma vizuri sana Mr X. Kwa mfano ukiona umefanya kitu positive kwa Mr X ( au kwa Kiongozi Mkuu) na akawa ame-respond positively, na hatimaye kuanza kuonyesha dalili za kama anataka kuionyesha AUDIENCE kuwa ana ukaribu fulani wa kipekee na wewe, hapo sasa ndiyo unatakiwa uwe alert beyond 100%, kwa sababu ndiyo kipindi ambacho huwa anakitumia kwa ajli ya kupanga na kupata THE BEST STRIKE kwako. Sema tu WEAKNESS MOJA KUBWA SANA ya mhusika inayopelekea haya yote yatokee ni kwamba, ikitokea tuseme, hata umemtendea kitu cha ajabu sana muda huu ambacho walio wengi huwa hawawezi kukivumilia, tuseme baada ya dakika 5 akakuona uko na mtoto wako mdogo, na ukawa huna mpango wa kum-restrict namna ya kumu-access mtoto huyo; yeye kuanzia pale huwa hana tena kumbukumbu ya kilichotokea huko nyuma, anapenda watoto ni in-born. Na kwa hali hiyo basi, mtu yeyote akiwakuta mtu huyo na mhusika katika mazingira hayo, hawezi kujua kabisa kuwa dakika 5 zilizopita watu wale walikuwa wamefanyiana unyama.
- Kitu kingine pia ni kuwa muda waliopishana mhusika na wawili hao wakati wa kutoka ofisini, ulikuwa unatosha kabisa kuwafanya wasikutane kwenye parking. Muda huo ulikuwa unatosha kabisa kuwafanya Mr & Mrs X wawe wameondoka kiasi kwamba mhusika asingefanikiwa kuwakuta wakiwa bado wako kwenye pale
Baada ya mhusika kuwa ameyachuja haya yote, alibadilisha uamuzi na kuamua kutohudhuria Ibada siku hiyo. Mambo kadhaa yaliyopelekea uamuzi wake huo ni kama yafuatayo:
- Walikaa kwa makusudi na kwa muda wa kutosha wakiwa kwenye parking wakimsubiri mhusika
- Walikuwa wamepanga kwa makusudi kwamba, Mrs X afike kwa ajli ya kumshukuru mhusika katika mazingira ya ofisini ila si ofisini kwake. Hii ni kutokana na ukweli kwamba Mrs X angeweza kumshukuru mhusika kwa kutumia simu ya mumewe wakati wowote pindi wawili hao walipokuwa wapo nyumbani
- Walikuwa wamepanga kuja kumshukuru kenye mazingira ya ofisini kwake ILA NJE YA OFISI YAKE. Hii ni kwa sababu Mrs X alikuwa ofisini kwa mumewe, lakini mumewe hakuweza kumpeleka kwa mhusika kwenda kutoa shukrani hizo
- Hawakutaka kumpigia mhusika kumjulisha kuwa walifanikiwa kuchukua zawadi za watoto, kwa sababu kitendo hicho kingeondoa mantiki ya Mrs X kufika mazingira ya ofisini kwa mhusika na hatimaye naye kutoa shukrani zake kama alivyofanya
- Walikuwa wanakwepa kuonekana na mawasilano mengine ya simu na mhusika, isipokuwa yale tu ambayo mhusika aliyafanya kwa kumpigia Mr X siku ya Ijumaa, akimtaarifu juu ya uwepo wa zawadi za watoto rafiki zake
- Walitamani J2 apite dukani aliponunulia zawadi,kutaka kujua kama Mr X alichukua zawadi hizo
- Na kama walitaka apite Savei, je, vipi kuhusu wale watu wawili aliowakuta kwenye kituo cha daladala pale Savei wakati anataka kuondoka? Je ilikuwa coincidence?
Mambo haya machache ukiunganisha na fact kwamba siku chache sana nyuma mhusika alinunua zawadi kwa watoto,.yangeonyesha ukaribu wa pekee ambao ndiyo mara nyingi sana Mr X huwa anatumia kwa ajili ya kutafuta nafasi ya k u-STRIKE
- Wakiwa bado wako pale kwenye parking, mhusika hakuweza kujua Mr & Mrs X walikuwa wanaelekea wapi, lakini most likely ilikuwa ni Kanisani
- Wakati mhusika anatoka ofisini, kitendo cha wawili hao kuwakuta bado wapo nje kwenye parking, kwa mtu aliyewaona kwa haraka haraka wakiwa hapo nje, angeweza kudhani kuwa walikaa hapo wakiwa wanamsubiri mhusika ili waelekee wote Kanisani, possibly baada ya kuwa wamepanga hivyo pindi walipokuwa wapo ndani ya jengo, ndani ya ofisi zao. Zaidi ni kuwa mhusika alionekana akiongea nao kwa muda kidogo kwenye eneo hilo la parking, maongezi ambayo hayakuwa na uwezekano wa kusikika na mtu yeyote aliyekuwa pembezoni kwa sababu ya interference ya muungurumo wa gari la Mr X ambalo tayari lilikuwa linaunguruma
- Na kama wawili hao walikuwa wanaelekea Kanisani, basi mhusika angeweza kuambatana nao hadi Kanisani, na wangefika kanisani wakiwa wote watatu, hali ambayo ingeonyesha ukaribu wa namna ya kipekee
Mbali na hayo yanayowahusu wawili hawa, huko Kanisani nako kulikuwa na mambo kadhaa yaliyomlazimu aanze kuyachuja, nayo ni kama yafuatayo:
Mabadiliko haya aliyoyataja kwenye kipengele hiki cha mwisho, yakawa pia yamamkumbusha kwa mbali, mabadiliko ya ratiba ya Ibada ya harusi yaliyowahi kutangazwa na Kiongozi X.
- Kabla ya ugonjwa wa Corona, maombi kawaida yalikuwa yanafanyika kwa Ibada moja tu ya kuanzia saa 12:00 jioni mpaka saa 2:00 usiku
- Kwa hali hiyo, kutokana na sababu alizozigusia hapo juu, kawaida mhusika alikuwa ameshaacha tangu siku nyingi nyuma, kushiriki Ibada zozote zenye kuangukia katika muda huo
- Baada ya Corona, ratiba ya maombi ilibadilika na kuwa Ibada mbili, moja kuanzia saa 10:30 jioni mpaka saa 12:00 jioni na nyingine kuanzia 12:30 jioni mpaka saa 2:00 usiku
- Mhusika hapa alikuwa amechagua kuwa atakuwa anahudhuria ile ya kuanzia saa 10:30 jioni mpaka saa 12:00 jioni
- Lakin ghafla tena hivi majuzi, Ibada ya maombi ikabadilika na kuwa ni kuanzia saa 11:00 jioni mpaka saa 1:00 usiku
Kwa kifupi, maelezo haya aliyoyatoa hapa mhusika ndiyo yaliyopelekea sasa akaamua kuwa atakuwa anahudhuria Ibada kuanzia saa 11:00 jioni; na kuondoka Kanisani saa 12:30 kabla ya Ibada kuisha. Strategy aliyokuwa nayo ni kwamba atakuwa anahakikisha amepaki gari lake kwenye sehemu ambayo halitaweza kuzibwa na magari mengine pindi anapohitaji kutoka
Kwa hiyo vipengele tajwa hapo juu vikapelekea mhusika akiwa bado yupo pale kwenye parking, kulazimika kuahirisha kuhudhuria Ibada ya maombi siku hiyo, lakini akiwa pia na PLAN aliyohitaji aifanyie kazi, kichwani kwake
Baada ya kuachana na Mr & Mrs X, alirudi nyumbani na kwenda kutengeneza hiyo PLAN, akiwa sasa ana hamu ya kutaka kujua kama wale watu wawili aliowakuta kituo cha daladala pale Savei ilikuwa ni coincidence ama la
Kweli J5 alipotoka ofisini, alipitiliza mpaka Mawasiliano na wakati anarudi, aliamua kupaki tena Savei. Siku hiyo tena, alikutana na mtu ambaye kumbukumbu zake mhusika zinaonyesha kuwa walipotezana tangu mwaka 2004, na alikuwa mtu wa karibu sana naye. Mtu huyu naye pia alikuwa katika pilika pilika za kuelekea uelekeo ule ule ambao alikuwa anelekea mhusika, na katika mfanano kabisa sawa na wale watu wawili aliowakuta kwenye kituo cha daladala J2 pale Savei!
- Aliamua kutohudhuria kabisa maombi hayo kwa wiki yote nzima
- Aliamua kuwa ndani ya wiki hiyo, atajifanya kutoka halafu atarudi na kuja kupark tena gari Savei, sehemu ile ile aliyopark J2, halafu aone kama anaweza kuonana na mtu yote pale, na pia nini atasema mtu huyo
ITAENDELEA NA KUMALIZIKA KESHO!
Kwa aliyefanikiwa kufuatilia uzi huu kwa makini, mpaka muda atagundua kuwa mtu mmoja maarufu (RIP) hapa nchini ambaye alikuwa anapenda sana kuwekeza kwenye Oil na Gas lakini akawa anakumbana na vigingi, alikumbana na vigingi hivyo kwa sababu hakutakiwa kujua nini kilichokuwa nyuma yake. Kwa sababu kama angeruhusiwa, ingebidi apewe data kwa ajili ya utafiti huo, na kwa hali hiyo angelazimika kujua namna data hizo zinavyopatikana, kitu ambacho ndiyo alitakiwa asikijue. Kwa hiyo kilichotokea baada ya hapo ni dhihaka ya kuambiwa akawekeze kwenye juice na matunda na kwamba data hizo ni expensive muno hana uwezo wa kumudu kuzinunua, wakati data hizo ni za bure kwa wawekezaji wazawa, tunazo na mtu akizihitaji kwa kufuata utaratibu unaokubalika na kwa ridhaa ya Serikali, hata leo anazipata
Zaidi ni kuwa Wana Siasa wote waliokuwa wakipinga na wanaoendelea kupinga mradi wa umeme wa maji, walikuwa kwenye kundi hili la Oil and Gas ambalo limekuwa liki-simulate matetemeko. Wanachofanya ni ku-simulate matetemeko ili waweze kupata data za kuwa-convince wenye pesa kwamba data za Oil na Gas zipo, lakini pia kui-convince Serikali kwamba tuko kwenye ukanda wa matetemeko ili iweze kutoa back-up katika jitihada za utafiti wa matetemeko.
Halafu eti kuna watu kila siku humu wanawalalamikia TISS hawafanyi kazi; sijui wanataka wawe wanatoa press release ndiyo waridhike kuwa wanafanya kazi? Nahisi siku wakikosea wakafanya hivyo, kuna watu wanaweza wakatamani kuhamia Sayari ya Mars!
UPDATE FRIDAY 05/06/2020
Hii nchi hatari sana.....
Hamna kitu hana chochote, hafai TISS wala CIA. Bora kidogo hata mimi mwandishi wa stori ungeweza kunifagilia kidogo. Hamna kitu, mimi si namfahanu, wala siyo kwamba namuonea wivu! Isipokuwa......!Mhusika anafaa kufanya kazi na cia
Sawa, uko unamwandiko mzuri sana mkuu. Malizia hapo isipokuwa nini tena. Kwanza mhusika jana alienda church kukutana na mr x?Hamna kitu hana chochote, hafai TISS wala CIA. Bora kidogo hata mimi mwandishi wa stori ungeweza kunifagilia kidogo. Hamna kitu, mimi si namfahanu, wala siyo kwamba namuonea wivu! Isipokuwa......!
Nashukuru kwa compliments, sema tu sasa zinatakiwa zisinijaze kichwa! Mhusika anadai kuwa alienda ila hawakuonana na Mr X. Possibly walipishanaSawa, uko unamwandiko mzuri sana mkuu. Malizia hapo isipokuwa nini tena. Kwanza mhusika jana alienda church kukutana na mr x?
Sawa, uko unamwandiko mzuri sana mkuu. Malizia hapo isipokuwa nini tena. Kwanza mhusika jana alienda church kukutana na mr x?