Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama ana matatizo ya Kisaikolojia, atapata msaada unaohitajikaMhusika anashuku mambo mengi sana, inaelekea hana familia ya angalau kuiteka akili yake iachane na ya kudhani kila watu, mazingira na matukio, yakatokea kumuwinda yeye.
Hii diary yake unayoiandika itakuwa msaada mkubwa kwa psychologist ili asaidiwe.Kama ana matatizo ya Kisaikolojia, atapata msaada unaohitajika
R.i.p kwa mdogo wake na mhusika.UPDATE: TUESDAY 29 JULY 2020
NYONGEZA YA MUHIMU KUHUSIANA NA TUKIO LA MR Y ALILOWAHI KUILIELEZEA HUKO NYUMA
TUKIO JINGINE JIPYA NA LA KUSIKITISHA SANA LINALOFANANA NA LILE LA MR Y
Kwa taarifa za sasa hivi ni kuwa, siku ya leo Jumanne, tarehe 28/07/2020, mhusika amepatwa na tukio jingine kubwa, ambalo nalo linaelekea kufafana sana na lile la Mr Y
- Tukio la mwanzo ni lile ambalo mhusika alitakiwa asafiri kwenda kufanya kazi mkoani, pasipo kuwa amepata ruhusa ya mwajiri wake
- Kazi hiyo alitafutiwa na Mr Y
MAELEZO YA TUKIO HILI NI KAMA IFUATAVYO HAPA CHINI
MHUSIKA APATA TAARIFA ZA MSIBA WA GHAFLA WA MDOGO WAKE
Mdogo wake huyu ndiyo yule aliyewahi kuja nyumbani kwa mhusika August 2008 akiwa anahitaji matibabu, halafu ndiyo kipindi hicho Mr Y akamletea mhusika ofa ya kwenda kufanya kazi mkoani, kazi ambayo baadaye iliyeyuka ghafla
Hata hivyo si nia ya mhusika kuwa anaweka public kila tukio analokumbana nalo, lakini kwa hili inabidi aliweke hadharani kutokana na mfanano uliojitokeza
MHUSIKA APATA TAARIFA ZA MSIBA WA GHAFLA WA MDOGO WAKE
SHERIA YA UTUMISHI WA UMMA KUHUSIANA NA MASWALA YA MFANYAKAZI KUPEWA RUHUSA KWA AJILI YA KWENDA KUHANI MSIBA WA NDUGU ZAKE
- Hakuugua, amefariki ghafla tu usiku wa kuamkia leo
- Inasemekana amefariki saa saba za usiku wa kuamkia Jumanne ya tarehe 28/072020
- Mhusika alipata taarifa za msiba leo saa 2 asubuhi, baada ya kupigiwa simu na shemeji yake anayeishi Mwanza
- Chanzo cha kifo chake hakijajulikana vizuri ila kwa upande mwingine inaonyesha kama kuna uwezekano wa kuwekewa sumu kwenye kinywaji aina ya pombe
TUKIO JINGINE LA MSIBA LILILOWAHI KUMTOKEA MHUSIKA MWAKA 2006, NA LINALOSHAHIBIANA KIDOGO NA HILI HAPA JUU
- Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha utumishi wake, mhusika alipata tatizo la msiba wa Baba mlezi mwaka 2006
- Wakati huo sheria ya kwenda kuhani msiba ilikuwa inawatambua warihti tu walioko kwenye file ambao ni Baba/ Mlezi na Mama/ Mlezi
- Wengine wote hawakuwa wanahusika na kama mtumishi ataamua kwenda, basi si kwa ruhusa ya mwajiri na kwa hali hiyo atahesabiwa kuwa maetorka kazini
- UNLESS kama sheria hiyo imebadilika kwa sasa, ila kama siyo, basi itakuwa bado iko hivyo; inaendelea kutambua wazazi/ walezi tu
- Kwa hiyo, kwa namna ambavyo sheria ilivyo kwa sasa, tuseme kama mhuiska angeamua kuondoka leo Jumanne ili kuwahi mazishi kesho Jumatano, ilibidi atoroke kwa sababu aliyefariki ni mdogo wake wa tumbo moja na si mzazi au mlezi
- Zaidi ni kuwa mwanzoni mwa mwezi huu wa Julai 2020, mhusika alipata waraka kutoka mamlaka za juu ofisini kwake, uliomhitaji ku-update taarifa zake kwenye file lake, mojawapo ikiwa ni hiyo taarifa ya mrithi (Next of Kin), ambaye kawaida anakuwa ni mzazi/ mlezi
- Mhusika alijaza taarifa hizo kiwa usahihi na kuziwasilisha yeye mwenyewe kwa Katibu Muhtasi wa Idara Julai 2020, mrithi akiwa ameonyesha kuwa ni mama yake mzazi
- Msiba umetokea muda mfupi tu baada ya mhusika kuwasilisha taarifa hizi
HITIMISHO
- Mara ya kwanza na ya mwisho mhusika alijaza taarifa za warihti wake ilikuwa ni mwezi August/ Septemba 2006
- Alifanya hivyo pia baada ya kuwa kuwa ameombwa kufanya hivyo na mamlaka husika kupitia idarani kwake
- Baada ya kujaza taarifa hizo mwaka huo, Baba yake Mlezi alifariki dunia Septemba 2006, ikiwa ni siku chache tu baada ya kuwa amewasilisha taarifa hizi
- Baada ya msiba kutokea, alipigiwa simu ghafla na na pia kujulishwa kuwa inabidi awahi mazishi kwa sababu marehemu alikuwa ameusia kuwa asizikwe bila yeye mhusika kuwepo msibani
- Mhusika aliondoka ghafla kwa usafiri wa ndege na akafanikiwa kuwahi mazishi
- Hata hivyo baada ya siku nyingi kupita, ikabanika kuwa marehemu hakuwa ameusia hivyo bali mhusika alidanganywa
- Hatimaye kadri siku zilivyopita, alikuja kubaini kuwa BAADHI ya waliokuwepo huko msibani walikuwa wanamhitaji mhusika kwa sababu walizozijua wao, na hivyo njia pekee iliyokuwa bora ya wao kuhakikisha kuwa wanampata kama wanavyomhitaji, ilikuwa ni kumdanganya kuwa marehemu alisema asizikwe bila yeye (mhusika) kuwepo
Kwa kifupi tu ni kwamba, mara ya mwisho mhusika aliwahi kuwa huko ni mwaka 2009, na baada ya hapo hajawahi tena kurudi huko kutokana na matukio yaliyowahi kujitokeza pindi alipokuwa huko.
Zaidi ni kwamba tangu May 2012 hajawahi kufanya safari yoyote ile (ya kikazi au binafsi), nje ya mkoa wa Dar es salaam kutokana na sababu za kiusalama
Mbali na hayo yote ni kwamba kama mhusika angeamua kuchomoka na kuelekea uwanja wa ndege kuwahi mazishi Mwanza, wale ambao wangebahatika kumuona wangedhani anakwenda Airport kwa ajili ya msiba wetu huu mkubwa wa Kitaifa wa kuondokewa na Rais wetu mpendwa, BWM.
MwiH
elly obedy