UPDATE: THURSDAY 03 SEPTEMBER 2020
USHAURI JUU YA RATIBA ZA IBADA BAADA YA KIPINDI CHA KORONA KUWA KIMEPITA
Mhusika anapenda
kuwapa challenge Viongozi wote wa Kanisa A ila ambayo pia ni ushauri, kwamba kama kuna uwezekano, basi ratiba ya vipindi vya Ibada Kanisani hapo kama ilivyokuwa hapo awali kwamba:
- Somo la Uanafunzi na Maandiko lirudishwe sasa kwenye siku yake ya kawaida ya Jumapili kama ilivyokuwa kawaida siku zote hapo awali
- Safari hii, somo hili liwe linafundishwa mfululizo kila J2 pasipo kurukaruka
- Mafundisho ya Biblia ya siku za J3 nayo yarudi kama kawaida, na pia nayo yasirukwe rukwe
- Maombi ya Ijumaa nayo yaendelee kuwepo siku za Ijumaa, na yasiwe yanakuwa na kawaida ya kufuta vipindi vingine. Hii ni kwa sababu, ni kawaida sana siku hizi kuwa maombi badala ya kuwepo Ijumaa, yamekuwa mara kwa mara yakitengenezewa mazingira ya kuwepo hata siku za J5 na Alhamis, na hivyo kupelekea kutokuwepo kwa mafundisho ya J5 kwa kipindi kirefu sana
Mhusika hapa ametumia maneno kuwapa challenge
kuwapa challenge Viongozi wote wa Kanisa A kwa sababu mpaka muda huu yeye alishajiridhisha pasipo shaka kabisa kuwa:
- Kinachopendwa zaidi na Viongozi wa Kanisa A ni maombi ila si mafundisho
- Kwa hali hiyo, viongozi hawa huwa wanajitahidi kuhakikisha kuwa mafundisho yapo kwa kiwango kidogo sana halafu maombi ndiyo yanakuwa kwa wingi sana
- Wanasisitiza zaidi maombi hasa yale ya WATU KUNENA KWA LUGHA
- Maombi ya aina hii(ya kunena kwa lugha) ni mazuri muno na yana nguvu sana ila ikumbukwe kwa upande mwingine pia kuwa, yana uwezekano mkubwa sana wa kutoa mianya ya watu wasiokuwa waumini, kushiriki kwenye maombi hayo kwa nia isiyokuwa njema kwa sababu hata wao nao wana uwezo wa kunena kwa lugha ila kwa njia ya mapepo
- Vile vile watu hawa ndiyo wanaoweza kutumika kuita mapepo kwa lugha ngeni na kusababisha yaendelee kuwepo kwenye nyumba za Ibada
- Kwa upande mwingine, ukisema kuwa maombi yawe ni yale ya kutumia lugha ya kawaida, hii itatoa mwanya pia wa mtu asiyekuwa muumini, kujulikana na waumini wenye nia njema ambao huwa wanahudhuria maombi hayo
- Ni kwa sababu asiyekuwa muumini aliyevamia maombi kwa nia isiyokuwa njema, pamoja na kuonekana na ile hali yake ya ugeni, bado pia hawezi kuwa yuko fluent katika kutamka maneno kwa njia ambyao ni ya ki-Biblia, hali inayoweza kupelekea kwa urahisi sana, waumini wazoefu wenye nia njema kumtambua kuwa huyo siyo mwenzao ila amevamia maombi yao.
- Kwa upande mwingine, mtu ambaye ni mgeni na amevamia maombi akiwa hana nia njema, lakini naye ananena kwa lughahuwa siyo rahisi kumgundua. Ni kwa sababu naye pia huwa anakuwa ananena kwa lugha
- Mtu kama huyu waumini wenye nia njema hawawezi kumgundua kirahisi kwa sababu sura wataiona ngeni kweli, lakini sasa je, si ananena kwa lugha?
- Baada ya hapo waumini watajua ni mshiriki tu kutoka Kanisa jingine amekuja kwa ajili ya maombi kanisani hapo kwa siku hiyo kumbe hapana, ……..is an invader from outside
- Halii kama hii inapokuwa imetokea, lazima itapelekea kutoweza kabisa kumgundua mtu mgeni na asiyekuwa muumini, ambaye amekuja kujiunga na maombi hayo, na ambaye si mshiriki wala muminini ila tu naye ananena kwa lugha lakini ile ambayo ni ya mapepo
Zaidi ni kuwa kabla ya Corona na pia kipindi kirefu nyuma kabla ya hapo, Somo la uanafunzi na maandiko limekuwa likikwepeshwa kuwepo na pale inapotokea kuwa lipo, lina kuwa na mazagazaga ya nyongeza ambayo hayatakiwi kuwepo, likiwemo swala la baadhi ya waumini kuambiwa wakae mbali na mahali somo linapofundishwa, badala ya kuhamasishwa kushiriki kwenye somo hilo. Mengi yapo kuhusiana na somo hili. Mafundisho ya J5 nayo pia yamekuwa na visingizio vingi sana vya kutokuwepo mara kwa mara, ila si maombi. Na mara nyingi sana, maombi yamekuwa yakifuta mafundisho ya J5. Hapo kabla, mhusika hakuwa amewahi kabisa kuona maombi yanageuka kuwa mafundisho,
ila KWA MARA YA KWANZA kabisa, tukio hilo lilitukia wiki jana ambapo maombi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika yaliahirishwa na kuwa mafundisho
Mhusika mpaka sasa yeye anaamini kuwa:
- Uwepo wa maombi ya kunena kwa lugha ukichukulia hatua sahihi za kiroho Kanisa A, kuna uwezekano wa mapepo kutokuwepo kabisa Kanisani hapo
- Viongozi wa Kanisa A wakijitahidi kufuata kwa usahahihi ratiba ya vipindi vya masomo yote ndani ya wiki na pia siku za J2, kuna uwezekano wa mapepo kutokuwepo kabisa Kanisani hapo
- Ratiba ya vipindi ikirudi na kuwa kama ilivyokuwa hapo awali, yaani mafundisho ya J5 yarudi kama kawaida na yasiwe yanabadilishwa badilishwa na kuwa maombi. kuna uwezekano wa mapepo kutokuwepo kabisa Kanisani hapo
- Somo la uanafunzi na maandiko likirudishwa J2 na kuwa linafundishwa bila kurukwa rukwa kwa visingizio visivyokuwa vya msingi, kuna uwezekano wa mapepo kutokuwepo kabisa Kanisani hapo
Mhusika yeye mpaka muda huu anaamini kuwa “idle “ time” ambayo huwa inakuwepo Kanisani hapo siku za J2 kutokana na kutokuwepo kwa Somo la uanafunzi na maandiko, huwa inatengeneza mwanya wa watu wasiokuwa waumini na wasio na nia njema, kuwepo Kanisani hapo bila waumini halisi kujua kuna watu kama hao
Mfano halisi tu ni kuwa mwaka 2011, mhusika alikuwa na kawaida ya kuhudhuria maombezi ambayo mara zote huwa yanafanyika mara baada ya Ibada ya pili ya kila J2. Mwanzoni, maombi hayo yalikuwa yanafanyika juu ghorofani, lakin baada ya siku kadhaa, yalihamishiwa karibu na gate la kuingilia Kanisani hapo, kwenye banda la Ibada za watoto. Maombi hayo baada ya kuwa yanafanyikia nje kwenye banda hilo, ghafla kukatokea watu amabo si waumini wakawa wanakuja kujiunga na maombi hayo ili kuyazimisha, na kuna mtu ambaye ni muumini wa pale Kanisani, alikuwa ana-coordinate kazi hiyo, maana wengine walikuwa wanakuja wakiwa kwenye Taxi. Jambo hili mhusika aliwahi kulifikisha kwa mmojawapo wa mashemasi, pia aliwahi kulieleza kwa
Kiongozi Mkuu siku walipokutana kwa ajili ya maongezi ofisini kwa kiongozi huyo, sema tu hajawahi kuwatajia mtu aliyekuwa ana-coordinate mpango.huo ila nii binti ambaye mpaka sasa yupo na kama watahitaji kumjua, mhusika yuko tayari kumtaja. Binti huyu pia huwa ni mhusika kwenye kundi la watu wa Ibada ya Sifa na Kuabudu
MUBARIKIWE TENA NA BWANA
WAEBRANIA 6:4-6 SUV
Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu kwa mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri.
MwiH
elly obedy