……………………….inaendelea
TAARIFA ZA MABADILIKO YA MUUNDO WA TAASISI AMBAZO UMMA BADO HAUJAJULISHWA
Mambo kadhaa yafuatayo bado hayajulikani
- Anayekaimu ukuu wa Idara wa UNIT-A kwa sasa anajulikana Idarani tu isipokuwa hakuna taarifa rasmi kwa umma iliyotolewa kuonyesha kuwa huyo ndiyo Kaimu MWI
- Mbali na hilo, kwa taarifa zilizopo wanazoendelea kubadilishana watu kwa sasa kwenye mazingira ya ofisini, ni kwamba kuna unit zngine kadhaa zilizo ndani ya mazingira ya Taasisi mama (tuziite kwa ujumla wake UNIT-B) ambazo baadaye zitakuja kuungana na UNIT-A, pamoja na UNIT-G na UNIT-H zilizoko Dodoma na Nzega
- Baada ya hapo unit zote hizi kwa ujumla wake ndiyo zitaunda MAJOR UNIT-B, iliyopelekea UNIT-A kuhama kutoka MAJOR UNIT-A ilikokuwa zamani
Hizi units zote zilizotajwa hapa zipo na zote ni sehemu muafaka kabisa ya Taasisi mama. Kitu pekee ambacho mpaka muda huu bado hakijasemwa ni huo muunganiko ambao watu wa ngazi za chini wanaendelea kuuongelea huku mamlaka za juu zikiwa bado hazitamka lolote
Kwa hiyo yote yaliyotajwa hapo bado hayajawa rasmi mpaka pale mamlaka husika zitakapokuwa zimechukua hatua ya kuujulisha umma kuwa zimeamua kufanya hivyo
TURUDI SASA KWENYE BARUA TATU ZA MHUSIKA TUKIZIHUSIANISHA NA MABADILIKO HAYA YA MUUNDO WA TAASISI MAMA
Kati ya barua hizi tatu ambazo mhusika ameshaziongelea leo:
- Mbili aliziandika yeye zikielekea mamlaka za juu, wakati moja aliipata ikiwa imetoka mamlaka za juu kuja kwake
- Kati ya zile mbili alizoandika, moja ililfika na nyingine haikufika
MKONDO WA MAWASILIANO WA BARUA ZA MHUSIKA KWENDA NGAZI ZA JUU, NDANI YA TAASISI MAMA
A: MKONDO KAMA ULIVYOKUWA ZAMANI
Mkondo wa zamani wa mawasilIano ya barua za mhusika kwenda ngazi za juu ulikuwa kama ifuatavyo
UNIT-A⟹⟹
MAJOR UNIT-A⟹⟹NGAZI ZA JUU
Kwa hiyo barua zake zote zilikuwa zinapitia kwenye MAJOR UNIT-A kabla ya kuwa zimepokelewa na ofisi husika ngazi za juu
B: MKONDO KAMA ULIVYO SASA
UNIT-A⟹⟹
MAJOR UNIT-B⟹⟹NGAZI ZA JUU
Mpaka hapa, msomaji inabidi arejee mambo kdahaayafuatayo
- Barua aliyoipata mhusika tarehe 27 JANUARY 2021, ikiwa imetoka mamlaka za juu, na iliyoandikwa tarehe 21 JANUARY 2021, ilitumia MKONDO WA ZAMANI
- Mhusika naye pia aliijibu barua hiyo kwa kutumia MKONDO HUO HUO WA ZAMANI, na barua hiyo ya majibu ilifika kule ilikokuwa imekusudiwa
- Vile vile, barua aliyoandika mhusika tarehe 21 JANUARY 2021, ikiwa inaelekea mamlaka za juu, mwanzoni aliiandika AKIWA MEKUSUDIA ITUMIE MKONDO WA ZAMANI
- Hata hivyo, baadaye alishauriwa na KMH kuwa inabidi atumie mkondo mpya na alifanya hivyo
Baada ya kuwa ametumia MKONDO MPYA kwa mawasiliano na kama alivyoshauriwa na KMH, barua hii ya mhusika haikuweza tena kufika ngazi za juu kule ilikokuwa imekusudiwa kufika
BARUA NYINGINE ALIYOIANDIKA MHUSIKA BAADA YA TAREHE 27 JANUARY 2021 KWA KUPITIAMKONDO WA ZAMANI
Baada ya kupata barua kutoka mamlaka za juu ikiwa imepitia kwenye mkondo wa zamani, mhusika alibadilisha mawazo na kudhani kuwa pengine ushaurri wa KMH kwa barua yake ile ya mwanzo haukuwa sahihi
- Mhusika aliamua kutoa nakala barua nyingine, sawa na ile ya tarehe 21/01/2021 na kuiwasilisha idarani ili iende ngazi za juu, kwa kupitia MKONDO WA ZAMANI
- Hata hivyo, barua hiyo ilirudishwa na Mkuu wa MAJOR UNIT-A (hii ni unit kule ambako UNIT-A wamehama) ikiwa na ki-note cha kikimshauri MHUSIKA APITISHIE BARUA ZAKE KWENYE MKONDO MPYA
Ikumbukwe kuwa mpaka hapa, mhusika alikuwa tayari ameshapata barua kwa kutumia mkondo wa zamani, na hatimaye naye kuijibu kwa kutmia mkondo huohuo
Baada ya hali hii kujitokeza, mhusika hatimaye aliitwa na Kaimu MWI mwingine mpya (Kaimu wa siku zote yule ambaye bado hajatangazwa, alikuwa safarini) ofisini kwa MWI kujadili swala hilo na baada ya maongezi yao, hatimaye mhusika aliamua apumzike kwanza na swala la barua hizi. Hiyo sasa ilikuwa ni J3 ya tarehe 07 Februari 2021 na kweli kuanzia pale alipumzika
- Ni kwa sababu barua hizo alikuwa akiziandika na hatimaye zingine kuwapa nakala baadhi ya wakuu wengine ndani ya taasisi hiyo
- Mhusika alihofia kuwa nakala za barua hizo hatimaye zingeweza kuwachanganya, na possibly kupelekea kumuona yeye kama mtu aliyechanganyikiwa
Hata hivyo, kwa wakati huo, jibu lililokuwa amelipata kwa ki-note kutoka kwa Mkuu wa MAJOR UNIT-A, baada ya kutokuipitisha barua yake, lilimthibitishia kuwa mkondo ule alioutumia kwa barua yake ya kwanza ya tarehe 21/01/2021 na kwa ushauri wa KMH, ulikuwa sahihi na hivyo akawa ana imani kua barua hiyo ya kwanza kabisa itakuwa ilishapokelewa na mamlaka husika
HITIMISHO
Baada ya mkanganyiko huu kujitokeza, mhusika aliamua kusitisha kwanza zoezi la barua hizi, na ndipo J2 ya wiki hii tarehe 02 MARCH 2021 ziilipoanza kujitokeza
“movements” zilizosababisha kumuweka kwenye tahadhari kubwa
Baada ya hapo jana Alhamis tarehe 04 MARCH 2021 aliamua afuatilie kwenye ofisi husika alikokuwa ameelekeza barua yake ili kuona kama kuna kitu tayari kinaendelea ndiyo akautana na situation ya HOLAAAAA, vijana wa mtaani huwa wanasema. Baruahiyo haikufika huko
Kwa hiyo mpaka muda huu, situation ya mawasiliano ya barua za mhusika ni kwamba
- Akiandika barua kupitia mkondo wa zamani, barua hizo zinarudishwa kwake
- Aakiandika barua kupitia mkondo huu wa sasa, barua hizo hazifiki kule zinakotakiwa kwenda, nadhani zinapotelea njiani
Na kwa sasa hivi, huyu Kaimu MWI wa siku zote (ambaye hajatangazwa) hayupo, yuko safarini.
Vile vile wakati ule wa pilikapilka ukiwemo ushauri wa barua kubadilishwa mkondo wa mawasiliano, na hatimaye zingine kuwa zinakwenda na kurudi, napo pia vile vile hakuwepo
Actually, barua zilizowahi kurudishwa na Mkuu wa MAJOR UNIT-A ni mbili, isipokuwa mwandishi hakuona mantiki ya kuziongelea zote mbili. kwa sababu moja tu ilikuwa inatosha kama sample
MUBARIKIWE TENA NA BWANA