#COVID19 Mkasa wa kipekee kuhusu pilikapilika za kujikinga na COVID-19

#COVID19 Mkasa wa kipekee kuhusu pilikapilika za kujikinga na COVID-19

……………………….inaendelea

TAARIFA ZA MABADILIKO YA MUUNDO WA TAASISI AMBAZO UMMA BADO HAUJAJULISHWA


Mambo kadhaa yafuatayo bado hayajulikani

  • Anayekaimu ukuu wa Idara wa UNIT-A kwa sasa anajulikana Idarani tu isipokuwa hakuna taarifa rasmi kwa umma iliyotolewa kuonyesha kuwa huyo ndiyo Kaimu MWI
  • Mbali na hilo, kwa taarifa zilizopo wanazoendelea kubadilishana watu kwa sasa kwenye mazingira ya ofisini, ni kwamba kuna unit zngine kadhaa zilizo ndani ya mazingira ya Taasisi mama (tuziite kwa ujumla wake UNIT-B) ambazo baadaye zitakuja kuungana na UNIT-A, pamoja na UNIT-G na UNIT-H zilizoko Dodoma na Nzega
  • Baada ya hapo unit zote hizi kwa ujumla wake ndiyo zitaunda MAJOR UNIT-B, iliyopelekea UNIT-A kuhama kutoka MAJOR UNIT-A ilikokuwa zamani
Hizi units zote zilizotajwa hapa zipo na zote ni sehemu muafaka kabisa ya Taasisi mama. Kitu pekee ambacho mpaka muda huu bado hakijasemwa ni huo muunganiko ambao watu wa ngazi za chini wanaendelea kuuongelea huku mamlaka za juu zikiwa bado hazitamka lolote

Kwa hiyo yote yaliyotajwa hapo bado hayajawa rasmi mpaka pale mamlaka husika zitakapokuwa zimechukua hatua ya kuujulisha umma kuwa zimeamua kufanya hivyo



TURUDI SASA KWENYE BARUA TATU ZA MHUSIKA TUKIZIHUSIANISHA NA MABADILIKO HAYA YA MUUNDO WA TAASISI MAMA

Kati ya barua hizi tatu ambazo mhusika ameshaziongelea leo:

  • Mbili aliziandika yeye zikielekea mamlaka za juu, wakati moja aliipata ikiwa imetoka mamlaka za juu kuja kwake
  • Kati ya zile mbili alizoandika, moja ililfika na nyingine haikufika

MKONDO WA MAWASILIANO WA BARUA ZA MHUSIKA KWENDA NGAZI ZA JUU, NDANI YA TAASISI MAMA

A: MKONDO KAMA ULIVYOKUWA ZAMANI


Mkondo wa zamani wa mawasilIano ya barua za mhusika kwenda ngazi za juu ulikuwa kama ifuatavyo

UNIT-A⟹⟹MAJOR UNIT-A⟹⟹NGAZI ZA JUU

Kwa hiyo barua zake zote zilikuwa zinapitia kwenye MAJOR UNIT-A kabla ya kuwa zimepokelewa na ofisi husika ngazi za juu



B: MKONDO KAMA ULIVYO SASA

UNIT-A⟹⟹MAJOR UNIT-B⟹⟹NGAZI ZA JUU

Mpaka hapa, msomaji inabidi arejee mambo kdahaayafuatayo

  • Barua aliyoipata mhusika tarehe 27 JANUARY 2021, ikiwa imetoka mamlaka za juu, na iliyoandikwa tarehe 21 JANUARY 2021, ilitumia MKONDO WA ZAMANI
  • Mhusika naye pia aliijibu barua hiyo kwa kutumia MKONDO HUO HUO WA ZAMANI, na barua hiyo ya majibu ilifika kule ilikokuwa imekusudiwa
  • Vile vile, barua aliyoandika mhusika tarehe 21 JANUARY 2021, ikiwa inaelekea mamlaka za juu, mwanzoni aliiandika AKIWA MEKUSUDIA ITUMIE MKONDO WA ZAMANI
  • Hata hivyo, baadaye alishauriwa na KMH kuwa inabidi atumie mkondo mpya na alifanya hivyo
Baada ya kuwa ametumia MKONDO MPYA kwa mawasiliano na kama alivyoshauriwa na KMH, barua hii ya mhusika haikuweza tena kufika ngazi za juu kule ilikokuwa imekusudiwa kufika



BARUA NYINGINE ALIYOIANDIKA MHUSIKA BAADA YA TAREHE 27 JANUARY 2021 KWA KUPITIAMKONDO WA ZAMANI


Baada ya kupata barua kutoka mamlaka za juu ikiwa imepitia kwenye mkondo wa zamani, mhusika alibadilisha mawazo na kudhani kuwa pengine ushaurri wa KMH kwa barua yake ile ya mwanzo haukuwa sahihi

  • Mhusika aliamua kutoa nakala barua nyingine, sawa na ile ya tarehe 21/01/2021 na kuiwasilisha idarani ili iende ngazi za juu, kwa kupitia MKONDO WA ZAMANI
  • Hata hivyo, barua hiyo ilirudishwa na Mkuu wa MAJOR UNIT-A (hii ni unit kule ambako UNIT-A wamehama) ikiwa na ki-note cha kikimshauri MHUSIKA APITISHIE BARUA ZAKE KWENYE MKONDO MPYA
Ikumbukwe kuwa mpaka hapa, mhusika alikuwa tayari ameshapata barua kwa kutumia mkondo wa zamani, na hatimaye naye kuijibu kwa kutmia mkondo huohuo

Baada ya hali hii kujitokeza, mhusika hatimaye aliitwa na Kaimu MWI mwingine mpya (Kaimu wa siku zote yule ambaye bado hajatangazwa, alikuwa safarini) ofisini kwa MWI kujadili swala hilo na baada ya maongezi yao, hatimaye mhusika aliamua apumzike kwanza na swala la barua hizi. Hiyo sasa ilikuwa ni J3 ya tarehe 07 Februari 2021 na kweli kuanzia pale alipumzika

  • Ni kwa sababu barua hizo alikuwa akiziandika na hatimaye zingine kuwapa nakala baadhi ya wakuu wengine ndani ya taasisi hiyo
  • Mhusika alihofia kuwa nakala za barua hizo hatimaye zingeweza kuwachanganya, na possibly kupelekea kumuona yeye kama mtu aliyechanganyikiwa
Hata hivyo, kwa wakati huo, jibu lililokuwa amelipata kwa ki-note kutoka kwa Mkuu wa MAJOR UNIT-A, baada ya kutokuipitisha barua yake, lilimthibitishia kuwa mkondo ule alioutumia kwa barua yake ya kwanza ya tarehe 21/01/2021 na kwa ushauri wa KMH, ulikuwa sahihi na hivyo akawa ana imani kua barua hiyo ya kwanza kabisa itakuwa ilishapokelewa na mamlaka husika



HITIMISHO

Baada ya mkanganyiko huu kujitokeza, mhusika aliamua kusitisha kwanza zoezi la barua hizi, na ndipo J2 ya wiki hii tarehe 02 MARCH 2021 ziilipoanza kujitokeza “movements” zilizosababisha kumuweka kwenye tahadhari kubwa

Baada ya hapo jana Alhamis tarehe 04 MARCH 2021 aliamua afuatilie kwenye ofisi husika alikokuwa ameelekeza barua yake ili kuona kama kuna kitu tayari kinaendelea ndiyo akautana na situation ya HOLAAAAA, vijana wa mtaani huwa wanasema. Baruahiyo haikufika huko

Kwa hiyo mpaka muda huu, situation ya mawasiliano ya barua za mhusika ni kwamba

  • Akiandika barua kupitia mkondo wa zamani, barua hizo zinarudishwa kwake
  • Aakiandika barua kupitia mkondo huu wa sasa, barua hizo hazifiki kule zinakotakiwa kwenda, nadhani zinapotelea njiani
Na kwa sasa hivi, huyu Kaimu MWI wa siku zote (ambaye hajatangazwa) hayupo, yuko safarini.
Vile vile wakati ule wa pilikapilka ukiwemo ushauri wa barua kubadilishwa mkondo wa mawasiliano, na hatimaye zingine kuwa zinakwenda na kurudi, napo pia vile vile hakuwepo

Actually, barua zilizowahi kurudishwa na Mkuu wa MAJOR UNIT-A ni mbili, isipokuwa mwandishi hakuona mantiki ya kuziongelea zote mbili. kwa sababu moja tu ilikuwa inatosha kama sample

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
Code ni nyingi
 
NEXT:
MHUSIKA AWASHAURI (NI USHAURI, SIYO AGIZO) VIONGOZ WOTE KANISA A

  • Waombe msamaha kwa Mungu, iwapo tu wanaona ndani ya roho na nafsi zao kuwa kuna mahali wamemkosea Mungu katika haya yanayoendelea kuandikwa humu
  • Vile vile wawaombe msamaha waumini wa kanisa A, kila kiongozi mmoja kwa wakati wake
Vinginevyo, WASIMAME MADHABAHUNI MMOJA MMOJA na kukanusha haya yanayoandikwa humu, MBELE YA MACHO YA WAUMINI WOTE WA KANISA A

Hitaji hili la viongozi hawa kuomba toba na rehema kwa Mungu, halimhusu Kiongozi mmoja tu ambaye amekuwa masomoni katika kipindi chote ambacho mambo haya yaliyopinda panda yamekuwa yakiendela Kanisa A

Mhusika ataleta orodha ya mambo ambayo kwayo viongozi hawa inabidi waombe toba na rehema kwa Mungu, ikiwa ni pamoja na kuomba msamaha mbele ya waumini wa Kanisa A

Ikumbukwe kuwa utakuwa ni ushauri, na si agizo; ushauri ambao wanaweza kuufuata au kutokuufuata
 
Wakati mhusika anaongea na MR X wakiwa ofisini J3 ya tarehe 08/03/2021. mhusika alijaribu kumuuliza MR X kuwa binti yake anaenda lini kwenye mkutano wa injili. MR X alijibu kuwa ni wiki ijayo, wakati binti mwenyewe alikuwa ameshasema kuwa ni J5 ya wiki hiyo. Hata hivyo kupishana kwao huku ni kwa kawaida sana iwapo tu safari hiyo waliwahi kuiongelea kipindi kirefu huko nyuma na baada ya hapo, hawakuwahi kuiongelea tena

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
Je mhusika haoni kuwa kupishana huku kwa majibu baina ya Mr X na bintie kunaweza kuwa na sababu maalumu??
Ni nadra sana mtoto kuwa na safari halafu mzazi asijue wakati wanaishi nyumba moja,
Kwahiyo huenda Mr X amemtajia siku fake mhusika kwa sababu, au binti amempa mhusika siku fake kwa sababu zake pia
 
UPDATE: SUNDAY 04 APRIL 2021

KUHUSIANA NA GARI LA MHUSIKA AMBALO BETRI ZAKE ZIMEKUWA ZIKIPIGWA SHOTI YA UMEME


Gari hili alilinunua kutoka Japan mnamo Julai 2013, baada ya kuwa amedhulumika lile la kwanza alilokuwa nalo. Wasomaji wa siku zote wa uzi huu watakumbuka namna ambavyo gari la kwanza aliwahi kulipoteza hali iliyopelekea anunue hili la pli. Ilimchukua takriban miaka mitatu tangu apoteze garii la kwanza hadi kufikia kununua hii la pili .
  • Gari hili la pili liliwekwa wakfu na viongozi wafuatao, chini ya ushauri wa MAMA WA KIROHO:Hawa ni Kiongozi Mkuu wa Kanisa A (KM-A), Kiongozi X na kiongozi mhubiri wa uzinzi
  • Hawa ndiyo watu pekee walioweka wakfu gari hilo la mhusika
  • Baadhi ya waumini wengine wachache nao pia walikuwepo Kanisani siku hiyo lakini hawakukaribishwa kuhusika kwenye Ibada hiyo, kitu ambacho si cha kawaida sana
  • Kawaida Ibada ya namna hii huwa iko wazi kwa kila muumini yeyote yule aliyepo Kanisani muda huo
  • Wakati wa kuwekwa wakfu gari hilo, kiongozi mhubiri wa uzinzi alimuomba mhusika afungue boneti la gari, kitu ambacho alifanya
  • Kitendo hiki nacho kinaweza kikawa si cha kawaida sana, kwa sababu yeye mwenyewe hakuwa amewahi kukiona hapo kabla
  • Vile vile, siku amekwenda nalo gari hilo ofisini kwa mara ya kwanza, kuna mtu mwingine naye pia huko ofisini,alimuomba mhusika afungue boneti
  • Huyu ni rafiki yake wa karibu sana na SENIIOR MSTAAFU WA KIUME na wanakaa ofisi jirani
Gari liliwekwa wakfu kwenye siku ya katikati ya wiki na si Jumapili, baada ya MAMA WA KIROHO kuwa ameshauri hivyo
Maelezo mengine ya nyongeza kuhusiana na uwekwaji wakfu gari hili yatafuata baadaye

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPDATE-2: SUNDAY 04 APRIL 2021

NYONGEZA MUHIMU SANA
KUHISIANA NA MATUKIO YA KUPIGWA SHOTI ZA UMEME BETRI ZA GARI LA MHUSIKA

Kwa mara mbili za mwisho
, matukio haya ya kupigwa shoti za umeme betri za gari la mhusika yamekuwa yakitukia J3 ambayo J2 yake, mhubiri aliyekuwa amesimama madhabahuni kwa ajili ya kufundisha neno la Mungu, ni huyu KIONGOZI JUNIOR ambaye J2 iliyopita alitumwa kuja kutoa tangazo la Sadaka ya mjane
  • Na ndiye yule yule ambaye alisimama madhabahuni J2 ya leo akiwa na ujumbe uliokuwa unamwelezea Yesu kuwa ALIFANYIKA DHAMBI
  • Vile vile huko nyuma kwenye mojawapo ya J2 ambazo aliwahi kusimama na baadaye Betri ya Gari la mhusika kupigwa shoti ya umeme, JUNIOR huyu huyu aliwahi pia kusimama akiwa na ujumbe huo huo wa YESU KUFANYIKA DHAMBI, sawa na ule alioukuwa nao leo
Ni kijana ambaye anaibukia kwa kasi sana na anafuata sawia kabisa nyayo za Kiongozi Mkuu, kiasi kwamba anaonekana kuwa atakuja kuwa qualified zaidi kwenye haya maswala ya uchakachuaji, possibly kuwazidi hata hawa wanaomfanyia training hiyo

Hata hivyo mhusika anampenda sana kijana huyu kutokana na jambo moja kubwa sana kwamba yeye ndiye yule aliyewahi kutumiwa KWENYE ULIMWENGU WA ROHO, ku-leakisha SECRET CODE YA UZINZI kwa mhusika, ambayo nayo hatimaye tena, ilipelekea kujulikana kwa secret code zingine kama ile ya “JENGO JIPYA”

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
Kuna 10,000 cash zawadi kwa ataenipa summary ya huu uzi hasa baada ya majonzi haya ya JPM.
Ahsante
 
UPDATE: MONDAY 05 APRIL 2021

TATIZO LA MWISHO LA SHOTI YA UMEME KWENYE BETRI YA GARI LA MHUSIKA AMBALO KIONGOZI MKUU WA KANISA A (KM-A ALIHUSIKAA


Hili ni tatizo pekee ambalo betri ya gari ya mhusika iliwahi kupata shoti ya umeme na kwa bahati nzuri, safari hii haikuungua
  • Tatizo hili lilitokea siku ya J2 ya tarehe 01/03/2020 (mwaka jana)
  • Lilitokea muda mfupi tu mara baada ya mhusika kuwa ametoka Kanisani siku ya J2 hiyo
  • Mhubiri wa J2 hiyo alikuwa ndiye huyu huyu KIONGOZI JUNIOR aliyehudumu siku ya J2 ya wiki jana
  • Ndani ya wiki hiyo kabla ya J2 hiyo kuwadia, mhusika alikuwa ametoa FEDHA YA MCHANGO KWA AJILI YA HARUSI YA MTOTO WA KIONGOZI MKUU (KM-A)
  • Harusi hiyo ilifaanyika siku ya J2 hiyo hiyo kwenye Ibada ya pili
Kwa hiyo J2 hiyo mhusika alihudhuria Ibada ya kwanza, kukwepa harusi iliyokuwa inafanyika Ibada ya pili.

Baada ya kuwa ametoka Kanisani, alipitia Shell kwa ajili ya kufanya Service ya gari lake, na baada ya kumaliza Service, ndiyo betri ikaaanza kuleta shida na ilibidi awapigie mafundi wake waliokuwa mbali na hapo ili waje kutoa msaada, na walikuja
  • Mafundi hao walifika hapo baada ya muda kidogo, walikuwa mbali na pale alipokuwa mhusika J2 hiyo
  • Ndiyo tatizo la shoti ya umeme la mwisho na la pekee kabisa ambalo betri ya gari la mhusika iliwahi kupata na ikanusrika kutokuungua
HITIMISHO

Kiongozi Mkuu wa Kanisa A (KM-A) pamoja na MR X, wanao utaalamu huo wa kupiga shoti vifaa vya umeme kwa kutumia procedures za kwenye ulimwengu war roho iikiwa ni pamoja na fedha.


Fedha hii ambayo huwa wanaipata bure, huwa ndiyo wanaitumia kama sadaka kwenye madhabahu za ulimwengu wa giza

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
Kwa hiyo inaonyesha kama linapofikia swala la kupiga shoti vifaa vya umeme, KM-A na MR X huwa wanamshirkisha pia KIONGOZI JUNIOR (KJ). Role ya KJ yeye inaonekana ni kusimama madhabahuni wakati mchakato ukiwa unaendelea
 
UPDATE 08 APRIL 2021

KIONGOZI MKUU WA KANISA A (KM-A) NA MAOMBI YA WIKI TATU (3) YALIYOTANGAZWA NA MAMLAKA ZA JUU KWA AJILI YA WIMBI LA PILI LA MAAMBUKIZI YA CORONA


Kwenye wimbi hili la pili la maambukizi ya Covid-19, baada ya Hayati JPM kuomba waumini na watu wengine pia waliombee Taifa, mamlaka za juu kitaifa za Kanisa A zilitangaza maombi ya wiki tatu mfululizo. Hata hivyo maombi hayo hayakufanyika Kanisa A na sababu kubwa ya kutokufanyika kwake inaweza kuwa ni KM-A hakuridhia maombi hayo kufanyika

Iwapo ni kweli kuwa KM-A hakuridhia maombi hayo kufanyika, basi kutakuwa kulikuwa na sababu ya msingi sana ya yeye kufanya hivyo, na itakuwa ni mara ya kwanza kwake kukiuka agizo kutoka mamlaka za juu. Hii ni kutokana na ukweli kuwa

  • KM-A anapenda sana maombi, na kawaida yeye huwa anaishi si kwa mkate tu bali pia kwa maombi
  • KM-A huwa hapendi kabisa mafundisho ya maandiko matakatifu, anapenda maombi
Kwa wasomaji wa siku zote wa uzi huu, watakumbuka kuwa mhusika amekuwa akilalamika sana kuhusiana na ratiba za maombi na/ au semina za Kanisa A. Hii ni kutokana na ukweli kuwa kwenye wiki ambazo huwa kunakuwa na program za namna hiyo kanisani (maombi na/ au semina) mara nyingi ndiyo wiki ambazo majanga mengi ya ajabu yamekuwa yakimpata mhusika. Hii pia inaashiria kuwa si mhusika tu ambaye amekuwa akipatwa na majanga, possibly na kuna watu wengine pia ambao wao huwa wako kimya siku zote

HITIMISHO

Kwa hiyo yaweza kuwa KM-A aliamua kuahirisha maombi hayo kwa kuwa alijua kuwa maombi hayo yangeweza kuja kumletea maswali mengi badaaye mbele ya safari

KM-A aliahirisha maombi hayo kimya kimya, hakutoa tangazo lolote kuwa yamefutwa

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPDATE 12 APRIL 2021

Today’s is SOKOINE DAY. Hayati Edward Moringe Sokoine alifariki tarehe ya leo, mwaka 1984

Coming up next………..


YANAYOJIRI KANISA A CHINI YA KIONGOZI MKUU WA KANISA A (KM-A) BAADA YA MHUSIKA KUONGELEA MAMBO MAKUU MAWILI AMBAYO NI:

  • Shoti za umeme kadhaa kwenye betri za gari lake mhusika, wahusika wakuu wa shoti hizo akiwataja kuwa ni Kiongozi Mkuu wa Kanisa A (KM-A) pamoja na MR X
  • USHAURI kwamba viongozi wote wa Kanisa A wanatakiwa kufanya toba na kuomba rehema kwa Mungu iwapo tu wanaona kuwa kuna mahali wamemkosea Mungu
Muhimu sana: Taarifa zitakazofuata kwenye post zitakazokuja leo kwenye uzi huu zinawafaa zaidi wale ambao tu wanapenda kuchambua mambo kwa kina
 
Muhimu sana: Taarifa zifuatazo zinawafaa zaidi wale ambao tu wanapenda kuchambua mambo kwa kina

MAELEZO YA UTANGULIZI

MAZINGIRA YA KANISANI SIKU YA IBADA YA IJUMAA KUU YA TAREHE 02/04/2021


Mhusika alifika Kanisa A dakika kadhaa kabla ya saa 10. Kulikuwa na Ibada iliyokuwa imepangwa kufanyika siku hiyo kuanzia saa 10 kamili. Hata hivyo Ibada hiyo haikuwepo tena kutokana na tatizo la msingi lililokuwa limejitokeza na lililowahusu waumini wote wa Kanisa A. Ibada hiyo ilikuwa imehamishiwa kule ambako tatizo hilo lilikuwa limejitokeza na si Kanisani tena
  • Mhusika hakuwa amepata taarifa za tatizo hilo, nadhani mashemasi wake walikuwa wamepitiwa kumjulisha
  • Kawaida kama kuna chochote kile ambacho kimejitokeza, kiwe ni cha dhraura au cha kawaida, mara zote huwa mashemasi wake huwa wanamjulisha kwa kumpigia simu
Mara ya mwisho mhusika aliongea na mmojawapo wa mashemasi wake wawili kwa simu ilikuwa ni January/ February 2020
  • Kilikuwa ni kipindi kile cha maandalizi ya Harusi ya mtoto wa KM-A
  • Shemasi aliongea na mhusika akimjulisha mhusika juu ya umuhimu wake kushiriki katika kufanikisha shughuli hiyo
Baada ya maongezi hayo ya mhusika na shemansi wake, mhusika alishiriki kwenye shughuli hiyo sawsawa kabisa kama shemasi huyo alivyokuwa amesahuri

Baada ya kukuta Kanisani hakuna Ibada siku hiyo, mhsuika aliamua kunyoosha njia kurudi nyumbani. Siku hiyo ya Ijumaa Kuu ikawa imepita

SIKU YA IBADA YA JUMAPILI YA PASAKA YA TAREHE 04/04/2021

Mhusika alifika Kanisani Ibada ya pili ikiwa tayari imeshaanza. Baada ya kupaki gari, aliharakisha kuelekea Ibadani na kwenda kukaa kwenye viti safu ya nyuma na ya mwisho kabisa, kwenye eneo lile lile ambalo amezoea kukaa siku zote

Baada ya Ibada ya Kusifu na Kuabudu kuisha na watu wote kuwa wameketi chini, muda si mrefu alitokea mtu mmpja mgeni, mwanamme wa makamo, mzee kama miaka 65 hivi.

Tukirudi nyuma kidogo, kipindi Ibada ya kusifu na kuabudud ikiwa bado inaendelea, na kabla muumini mgeni huyu hajaja, mhusika alikuwa amechukua viti viwili na kutengeneza safu nyingine ya viti viwili tu, nyuma ya ile safu ya mwisho aliyokuwa ameikuta hapo awali.
  • Ni mara nyingi huwa anafanya hivi, huwa hapendelei sana kukaa kwenye viti vilivyobanana banana, pale tu viti hivyo vinapokuwa havijajazwa na watu na pale tu inapokuwa imetokea kuwa kuna nafasi nyingine ya kutosha nyuma ya viti hivyo vilivyopangwa kwa kubanana banana,
  • Mbali na hilo, mhisika vile vile wakati mwingine huwa anapenda kuabdud akiwa anatembea tembea wakati wa Ibada ya Kusifu na Kuabdu, na hivyo pale imapotokea kuwa kuna viti vimebanana na havina watu, viti hivyo huwa anavitenganisha ili apate nafasi ya kuwa anatembea tembea bila bughudha
Kwa hiyo J2 ya Pasaka mazingira ya kwenye viti vya nyuma yalikuwa hivyo, possibly kutokana na ukweli kuwa waumini walio wengi walipendelea zaidi kuhudhuria Ibada ya kwanza kwa sababu ilikuwa ni sikukukuu na hivyo kupelekea Ibada ya pili kutokuwa na waumini kwa idadi ile iliyo ya kawaida kwa siku zote

Kwa hiyo mhusika akiwa ameweka mazingira ya namna hiyo kwenye sehemu ile ambayo amezoea kukaa siku zote, muumini mgeni na ambaye sura yake likuwa ngeni kabisa machoni pa mhusika, aliingia Kanisani na kwenda kukaa kwenye mojawwpo ya viti alivyokuwa mhusika amevinyofoa kutoka kwenye safu ya viti iambyao kwa sasa ilikuwa mbele yake mhusika, ila ambayo hapo awali wakati mhusika anaingia Kanisani hapo, aliikuta ikiwa ni ndiyo ya safu ya mwisho ya viti. Kwa hiyo mhusika alipotengeneza safu ya viti vingine viwili, safu hiyo mpya ya viti hivyo viwili ndiyo ikawa ya mwisho, na ile aliyoikuta hapo awali, ikawa ni ya pili kutoka mwisho

Hivyo basi, muumini huyu mgeni aliingia Kanisani hapo na kukaa kwenye kiti cha pili kilichokuwa kimebaki, na ambacho ni mhusika alikuwa amekiweka mahali pale, hali iliyopelekea wakawa waumini wawili tu waliokaa kwenye safu hiyo, yaani mgeni pamoja na mhusika mwenyewe


……………………inaendelea
 
……….inaendelea

WAUMINI WAWILI WALIOKAA SAFU YA MWISHO NA YENYE VITI VIWILI TU

  • Mmojawapo wa waumini hawa wawili alikuwa ni mhusika
  • Muumni mwingine alikuwa ni mgeni aliyeingia Ibadani baada ya Ibada ya Kufifu na Kuabdu kuwa imeisha
  • Waumini hawa hawafahamiani na wala hawakusalimiana
  • Mhusika alikuwa amevaa suti ya mikono mifupi
BAADA YA KUPITA TAKRIBANI DAKIKA 15 HIVI:

Muumini mgeni alimsogelea mhusIka na bila kumsalimia, alimmnong’oneza maneno akimuuliza swali “HAPA LEO KUNA MEZA YA BWANA?’

Mhusika alimijibu ‘HAPANA”, na maongezi yao yaliishia pale

Baada ya takribani kama dakika 5 hivi zingine mbele, muumini mgeni alinyanyuka kwenye kiti na kuanza kutembea taratibu akiondoka mahali pale
  • Muumini huyu hakumuaga mhusika, na mhusika naye pia kwa wakati huo, hakujua kuwa ndiyo alikuwa anaondioka
  • Mhusika alikuja kujua kuwa muumini huyu aliondoka baada ya muda mrefu kupita na hatimaye Ibada kuisha na pasipo kumuona tena muumini yule Kanisani
Baada ya muumini huyu mgeni kuondoka Kanisani pale, mhusika hakunyanyuka tena kwenye kiti alichokuwa amekaa, hadi Ibada ilipoisha. Baada ya Ibada kuisha alisalimiana na watu kadhaa na hatimaye kuelekea moja kwa moja kwenye parking, akawasha gari lake na kuondoka kurudi nyumbani

Hiyo siku nayo ikawa imepita, yaani Jumapili ya Pasaka

SIKU YA IBADA YA JUMAPILI YA TAREHE 11/04/2021 (JANA)


……………….inaendelea
 
……………….inaendelea

SIKU YA IBADA YA JUMAPILI YA TAREHE 11/04/2021 (JANA)


Mhusika alifika kanisani dakika chache baada ya saa 4 kamili na kupaki gari lake nje kwa muda akisubiri watu wa Ibada ya kwanza watoke kwanza halafu ndiyo naye aingize gari lake ndani

Kwenye mida ya kama saa tano kasorobo, mhusika aliamua kulifuata gari lake nje ili aliingize ndani. Ibada ya pili ilikuwa inatarajiwa kuanza saa 5:00 kamili

Akiwa anatoka nje, pale getini walipishana na kusalimiana na mmoja wa mashemasi wake, shemasi akiwa anaingia, mhusika akiwa anatoka. Vile vile kipindi anaingia Kanisani Ibada ya kwanza ikiwa inaelekea mwisho, alibahatika kuonana na kusalimiana na Mama wa Kiroho akiwa ameambatana na mjukuu wake, ambaye pia (mjukuu) ni swahiba wa karibu sana na mhusika

NAMNA MCHAKATO WA KUINGIZA NDANI GARI LA MHUSIKA ULIVYOKUWA J2 HIYO (JANA)

Akiwa kwenye gari, wakati anaingiza gari ndani
  • Pale karibu kabisa na geti kushoto ilichomoka ghafla gari nyingine kutoka kwenye parking, ikiwa inataka kutoka nje.
  • Wakati huo huo, mhusika alikuwa ameruhusiwa kuingiza ndani gari baada ya gari zote zilizokuwa zinatakiwa kutoka nje na kuzipisha zingine, kuwa zimetoka
  • Gari hii ilibidi apishane nayo mhusika kwa ungalifu mkubwa vinginevyo ingeweaa kupelekea hata kukwanguana
  • Ilikuwa ni rahisi zaidi kwa gari hii ikabaki kwenye parking halafu mhusika akapita kwanza, halafu na yenyewe ndiyo ikatoka kwenye parking na kutoka nje baada ya hapo
  • Hicho kitu hakikufanyika na ilionekana kama ilikuwa inamsubiria atokeze getini mlangoni halafu na yenyewe ndiyo ianze mchakatto wake wa kutoka nje
  • Vinginevyo mhusika alitakiwa arudi tena nje kinyumenyume, aipishe kwanza gari hiyo itoke halafu ndiyo aanze tena kuingia
Mara baada ya kuwa amepishana na gari hiyo……………..
  • Mbele kidogo alibahatika kupokea maelekezo ya Shemasi ambaye mara zote huwa anashirikiana na Asakri katika kupanga na kuhakikisha usalama wa magari Kanisani hapo
  • Shemasi alimwelekeza mhusika apaki kushoto ambako kulikuwa na nafasi, ila mhusika yeye wakati huo alikuwa ameona nafasi nyingine mbele kabisa ambayo haikuwa inahitaji ku-manouvre ili mtu aweze kupaki
  • Hii nyingine aliyokuwa akielekezwa na shemasi ilikuwa inahitaji manouvring na ilikuwa na usumbufu kwa wale waliokuwa wanakuja kwa kumfuata nyuma yake mhusika
Kwa hiyo mhusika alinyoosha moja kwa moja na kwenda kupaki sehemu ya mbele kabisa, gari lake likawa ni la kwanza na mbele yake kuna dead-end ambayo magari hayawezi kupita tena isipokuwa binadamu tu
  • Baada ya kupaki, akiwa anataka kushuka kuna mtu asiyemfahamu alimsogelea na kumuomba asogeze mbele kidogo gari aache nafasi nyuma kwa sababu kuna kitu walikuwa wanataka kufanya
  • Mhusika alikubali kusogeza gari mbele na hivyo kupelekea kuwa mshazari na gari nyingine iliyoikuta ikiwa tayari imepaki kulia kwake mhusika
  • Gari hizi mbili sasa zikawa zimepaki katika namna ambayo gari ya mhusika iliiziba gari ile nyingine na zote mbili zikawa zimepaki kwa kutengeneza umbo la namba saba (7)
Mara tu baada ya mhusika kuwa amepaki gari lake na kushuka chini, muda huo huo tena kuna gari nyingine ilikuja kupaki nyuma yake. Gari hii ilipaki pale ambapo mhusika aliambiwa apahame asogee mbele kidogo kwa sababu kulikuwa na shughuli maalumu iliyokuwa inatarajiwa kufanyika mahali pale

Baada ya kushuka kwenye gari, akiwa anaelekea ndani Kanisani akirudi kupitia njia ambayo alikuja nayo wakati akiwa anaingiza gari (kuna njia nyingine ya pili ya kupitia uchochoroni kule ambako njia ni dead end kwa magari isispokuwa kwa binadamu tu),

  • Si mbali na hapo njiani, alikutana tena na shemasi yule aliyemwelekeza kupaki mwanzoni mwa parkng halafu yeye akaghairi na kwenda kupaki mbele
  • Shemasi alimweleza mhusika kuwa amepaki mahali ambapo kuna gari ambayo bado haijatoka ila inatarajiwa kutoka, na mwenye gari hiyo hakuwapo mahali hapo kwa wakati huo
  • Waakati huo huo, na kwa muda huo huo, mhusika naye alikuwa tena tayari ameshazibwa na gari nyingine nyuma yake (Nissan X-trail ya Blue)
  • Na ili mhusika aweze kuipisha gari iliyokuwa inahitaji kutoka, na ambayo kwa sasa mwenyewe hakuwepo mahali pale, ilikuwa inabdi mwenye X-trail ampishe kwanza mhusika, halafu mhusika naye ndiyo ampishe mwenye gari hiyo iliyokuwa inatarajiwa kutoka
  • Vile vile huyu mwenye gari X-Trail iliyokuja na kupaki ghafla nyuma ya gari ya mhusika, tayari alikuwa ameshatoka kwenye gari,hakuwamo kwenye gari hiyo wakati Shemasi anaongea na mhusika juu ya swala la kuipisha gari nyingine
Grari hiyo iliyokuwa inasemekena kuwa itatoka, ndiyo ile ambayo mhusika alienda akaiziba ikiwa kushoto kwake hali iliyopelekea kutengeneza umbo la namba saba (7). Ilikuwa ni baada ya kuombwa asogeze mbele kidogo gari yake

Mhusika na Shemasi waliachana kwa kukubaliana kuwa mwenye gari atakapohitaji kutoka, basi Shemasi atakuja kumuita mhusika kwenye Ibada. Mhusika kwa wakati huo alikuwa haamini kama kweli kuna mtu alikuwa bado anahitaji kutoka na ambaye hakuwa ametoka katika kipindi chote ambacho magari yalikuwa yameombwa na pia kuruhuhusiwa kutoka nje, alichelea kwa kudhani kuwa pengine ni utani tu

Hata hivyo mara tu baada ya Ibada kuanza, Shemasi alikuja kumuita mhusika na kumweleza kuwa muda umefika wa kumpisha yule mtu aliyekuwa anataka kutoka. Mhusika alitoka Ibadani na kuelekea kwenye parking na kumpisha mtu aliyekuwa anahitaji kutoka.

Wakati huo gari X-Trail haikuwepo tena maeneo yale, na possibly ilikuwa imetoka kabisa nje ya ukumbi wa Kanisa

Kuanzia muda ule mhusika alipokaki gari hadi kuja kuitwa tena na Shemasi ili ampishe mtu, haukuzidi muda wa dakika 15


……………..inaendelea
 
……………….inaendelea

AKIWA ANATOKA KWENYE IBADA KUELEKEA KWENYE PARKING KWA AJILI YA KUMPISHA MTU MWEYE GARI ILILOKUWA LINAHITAJI KUTOKA NJE


Kwenye uchochoro ambapo huwa yamepaki malori pamoja na mabasi, alipishana na kusalimiana na wanandoa wawili
  • Walipishana kwa ghafula mno kiasi kwamba hakuna mtu mwingine aliyeweza kuwaona, unless awe ni mtu aliyekuwa ameambatana nao
  • Hawa ni wale ambao waliwahi kuzua mtafaruku Kanisani hapo baada ya kuwa wamewakaribisha waumini kwenye hafla yao na waumini kukumbana na matukio ambayo hayakuwafurahisha sana
Baada ya kuwa amefika sehemu ile aliyokuwa amepaki, alimfahamu mtu aliyekuwa anatakiwa kumpisha, ni mumumin swahiba wake wa karibu
  • Hawakuongea kwa sababu tayari swahiba wake huyo alikuwa ndani ya gari, na mhusika naye alikuwa na haraka ya kurudi kwenye Ibada
  • Mhusika alimpisha mtu huyu na kutoka, na hatimaye akarudi kuendelea na Ibada
Mhusika alirudi kwa kutumia njia ile ile ya mwanzo na si ile ya mbele ambako ni dead end kwa magari isipokuwa kwa binadamu tu.

Alipofika sehemu aliyokuwa amekaa, aliwakuta wanandoa nao pia wako mahali pale. Baada ya kumuona amerudi, waliamua kuhama na kwanda kukaa sehemu mbele kidogo, kulia kabisa mwa Kanisa

Mara baada ya Ibada ya Kusifu na Kuabdu, mtu aliyepishwa na mhusika alikuwa tayari amesharudi tena Kanisani.
  • Alionekana madhabahuni akimkaribisha mhudumu wa Ibada ya siku hiyo.
  • Baada ya Ibada kuisha, mhusika alipofika kwenye parking, alikuta gari la “mpishwa” limepaki usawa ule ule ambao mhusika aliombwa apapishe kutokana na kuwa kulikuwa na kazi maalumu iliyotakiwa kufanyika pale
HITIMISHO

Alichokiona yeye kwenye hizi pilika pilika za kupaki magari, na kutokana na uzoefu wake wa miaka takribani kumi sasa, ni kwamba mhusika alitakiwa apaki kwenye parking ile ya kwanza aliyokuwa ameelekezwa na shemansi. Pale ndiyo mazingira ya kupaki gari lake yalikuwa yameandaliwa zikiwemo gari maarufu ambazo mara nyingi huwa anatakiwa apaki amepakana nazo

Hata hivyo, baada ya mhusika kuwa ameamua vinginevyo:
  • Akawa amevuruga plan ile ya awali na hivyo kupelekea kubuniwa kwa plan nyingine mpya ya mpangilio wa magari mengine aliyotakiwa kupakana nayo siku hiyo Ibada ikiwa inaendelea
  • Vile vile ulikuwa unatafutwa uwezekano possibly wa yeye kupita kwenye njia ile ya uchochoroni, ukizingatia kuwa J2 ile iliyokuwa imepita nyuma yake, yaani ile ya Pasaka, mhusika aliwahi kuonekana ananong'onezana kitu na mtu mgeni na ambaye hatimaye mgeni huyo aliondoka Kanisani kabla ya Ibada kuisha
  • Mhusika pia alimtayarishia kiti mgeni huyu siku hiyo kabla hajafika kwenye Ibada. Ni kwa sababu alikuwa anamtarajia
Jumapili hii vile vile (jana) mhusika hakuweza tena kutoka kwenye Ibada kwenda sehemu nyingine yoyote ile. Ibada iliisha saa 8 mchana na baada ya hapo mhusika alisalimiana na watu kadhaa na hatimaye kunyoosha moja kwa moja kuelekea kwenye parking akawasha gari lake na kurudi nyumbani

Mhusika pia alikuwa amevaa koti la mikono mirefu siku hiyo kutokana na hali ya hewa iliyokuwapo

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
KUHUSIANA NA HAWA WANANDOA WAPYA

KITENDO CHA WANANDOA HAWA WAPYA KUKUTANA NA MHUSIKA KWENYE UCHOCHORO WA PARKING YA MALORI NA MABASI, ALIPOKUWA AKIELEKEA KWENYE PARKING KWA AJILI YA KUMPISHA MTU AMBAYE ALITAKIWA KUTOKA NA GARI


Inaonyesha kama wanandoa wawili hawa, walitarajia kupishana na mhusika kwenye sehemu hiyo ambapo huwa yanapaki malori na mabasi na hivyo tukio hilo lilikuwa limepangwa

Kwa hiyo, inaonyesjha kama:
  • Iwapo mhusika asingefanikiwa kurudi kutoka kule alikokuwa ameelekea, wanandoa hawa wasingehama kwenye viti pale alipowakuta mhusika wakati anarudi kutoka kwenye kumpisha mtu aliyekuwa anatoka na gari
  • Wangeendelea kukaa pale kama mashahidi wa kushuhudia kuwa “sisi tumepishana naye pale kwenye parking ya malori na mabasi akiwa yuko hai hai”
Hata hivyo, baada ya mhusika kufanikiwa kurudi, kukawa hakuhitajiki tena ushuhuda wa aina yoyote ilee na hivyo kupelekea wawili hao kuhama na kwenda kukaa sehemu nyingine ya mbali, pengine ili kukwepa kujulikana na mhusika vile ambavyo waliikuwa wanadhani vina uwezekano wa kutokujulikana

MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
UPADATE: TUESDAY 13 APRIL 2021

TAARIFA MUHIMU YA NYONGEZA INAYOHUSIANA NA PILIKA PILKA ZA MHUSIKA KUINGIZA GARI NDANI YA UZIO WA KANISA JUMAPILI YA TAREHE 11 APRIL 2021


Ni kwamba hizi faulo za mhusika kukumbana na vitimbi vingi Kanisani siku za J2 pindi anapokuwa anaingiza gari lake ndani ya uzio wa Kanisa, ni za siku zote na mhusika alishazizoea kwa sababu zimekuwa zikifanywa kwake mara kwa mara, na engineer mkubwa wa pilika pilika hizi huwa ni Kiongozi Mkuu wa Kanisa A (KM-A)
  • Mara kwa mara amekuwa akifanyiwa hivi katika namna ambayo mhusika huwa anajikuta amepaki karibu na gari ya KM-A yenye usajiji li wa namba TXXX ACR
  • KM-A ana gari mbili lakini mara zote huwa anapenda kuitumia hiyo yenye namba hizo ambayo huwa haina parking maalum
  • Zipo na gari zingine pia mabzo mhusika asingependa kuongelea details zake humu
  • Kwa hiyo wapo na waumini wengine pia amabao huwa anashirikiana nao, waumini wa kawaida ikiwa ni pamoja na viongozi, akiwemo kiongozi mhubiri wa uzinzi
  • Viongozi hawa wawili ndiyo huwa wamo kwenye program hii
  • Mama wa kiroho naye pia huwa yumo kwenye program hii, tena siti ya mbele kabisa
Kiongozi X pamoja na wengine ambao hajawataja hapa mhusika, wao huwa hawahusiki sana kwenye project hii. Ni mtindo ambao umekuwa ukifanyika kipindi kirefu nyuma na wahusika wake anawajua wote isipokuwa muda wa kutoa details za vitu vingine ambavyo ni marginals huwa anakosa.

KILICHOPELEKEA ATOE DETAILS ZA J2 ILIYOPITA

Mhusika amelazimika kutoa details za pilika pilika hizi za J2 iliyopita zake kwa sababu zenyewe ziliambatan na kitu kingine kikubwa cha nyongeza kama ambavyo ameshatoa maelezo hapo juu

NEXT:


Mazingira ya wiki ambazo mhusika huwa anapata mashambulizi kutokea Kanisani mara nyingi huwa ni kwenye wiki ambazo huwa zinaanza kwa maombi halafu baadaye inafuata Semina, ndani ya wiki hiyo hiyo moja.

Kwa safari hii, version ya mlolongo wa program hii ya Kanisani imebadilika kidogo. Mhusika atauongelea utofauti wa “version” wake na namna ulivyojitokeza
 
“VERSION MPYA” KUHUSIANA NA MLOLONGO WA MATUKIO YA KANISANI J2 ILIYOPITA KANISANI

Ni kwamba J2 ya Pasaka ya tarehe 04/04/2021 lilitoka tangazo la program ya wiki iliyokuwa inafuata kuwa kutakuwa na maombi ya siku tatu (3) kuanzia J5 hadi Ijumaa, kwa ajili ya mikutano ya Injili. Tangazo hilo halikugusia chochote kuhusiana na uwepo wa proram maalumu Jumapili inayofuata ya wiki ya tangazo hilo husIka, yaani J2 ya tarehe 11/04/2021

  • Kwa hiyo pamoja na uwepo wa maombi kwa siku za J5 hadi Ijumaa, tangazo hilo lilionyesha kuwa J2 inayofuata itakuwa ni ya Ibada za kawaida sawa tu na zilivyo J2 zingine siku zote, kwamba hapatakuwa na program yoyote special
  • Kwa hali hiyo, tangazo hilo halikuonyesha kuwa kuna kitu kingine cha ziada kitafuata kuanzia J2 ya wiki itakayofuata
SEMINA YA WIKI NZIMA YATANGAZWA SIKU HIYO HIYO KUANZIA J2 YA TAREHE 11/04/2021 HAD J2 NYINGINE YA TAREHE 18/04/2021

J2 ya tarehe 11/04/2021 mhusika alifika Kanisani akiwa anajua kuwa ni J2 ya Ibada ya kawaida tu. Hata hivyo, baada ya pilika pilika alizozieleza hapo awali, na hatimaye kuwa ame-settle kwenye Ibada, na mara baada ya Ibada ya Kusifu na Kuabudu kuwa imeisha ndiyo pale lilipotolewa tangazo kuwa kuanzia J2 hiyo kutakuwa na Semina ya wiki nzima hadi J2 nyingine inayofauata, yaani J2 ya tarehe 18/04/2021
  • Kama mhusika alivyosema awali, J2 iliyokuwa imepita nyuma yake, yaani ile ya tarehe 04/04/2021, tangazo la Semina hii halikuwahi kutolewa
  • Mhusika alishangaa kidogo kwa nini tangaoz la Semina hiyo lilitolewa papo kwa papo na kwa siku hiyo hiyo
HITIMISHO

Huwezi kujua pengine labda ilidhaniwa kuwa kama tangazo la Semina hiyo lingetolewa J2 ile ya tarehe 04/04/2021, kungekuwa na uwezekano wa mhusika ku-connect dots kwamba kuna maombi ya siku tatu yanaanza halafu baada ya hapo tena yanafuatiwa na Semina ya wiki nzima, kitu ambacho kingeweza kupelekea kumuweka kwenye tahadhari kubwa kwa sababu ameshabaini pasipo shaka kuwa mara zote huwa anapata mashambulizi pale tu inapotokea kuwa kuna maombi yanayofuatiwa na Semina, ila ndani ya wiki hiyo hiyo moja

Pamoja na kwamba version ya kipindi hiki imebadilika kwamba maombi ya siku tatu yanaungana na siku moja tu ya Semina halafu siku zingine za Semina hiyo zinakuwa kwenye wiki nyingine, possibly mhusika angeweza kujua kuwa kuna trick imefanyika na hivyo kumpelekea kuchukua tahadhari

Kwa hiyo inaonyesha kama mhusika alitakiwa asiwe na tahadhari, na hivyo uwepo wa Semina alikuja kuufahamu baada ya pilika pilika zote zilizokuwa zimekusudiwa kwake J2 hiyo kuwa zimekamilika

Mbali na KM-A kutangaza semina hiyo, muumini mwingine naye pia alipanda madhabahuni kupigilia msumari wa uwepo wa Semina hiyo,, kitu ambacho hakikuwa cha kawaida na si cha lazima sana. KM-A tayari alikuwa ameshatangaza kuwa kuna semina na hiyo peke yake ilikuwa inatosha. Hapakuwa na haja tena ya ku-overemphasize juu ya uwepo wa Semina hiyo kwa sababu hapakuwa na muumini yoyote aliyekuwa ame-doubt au kuhoji uwepo wake

Muumini huyu aliyesimamama madhabahuni kupigilia msumari wa uwepo wa Semina hiyo ndiyo yule ambaye mhusika alikuja kutolewa Ibadani na Shemasi, ili akaipishe gari ya muumnin huyo ambayo mhusika alikuwa ameiziba. Gari hiyo ilikuwa ni ya huyu muumini ambaye naye alilazimika pia kusimama madhabahuni kutangaza Semina hiyo J2 hiyo


MUBARIKIWE TENA NA BWANA
 
Back
Top Bottom