SEHEMU YA TATU (03)
SASA ENDELEA; baba alikuja bila hata kuambiwa, na mambo yote nilikua nayaona lakini sikua na uwezo wa kusema yaani kwa kifupi nilikua kwenye ulimwengu mwingine kabisa ambao niliweza kuona kila jambo linaloendelea lakini sikua na uwezo wa kufanya kuongea jambo lolote.
Nikiwa katika ulimwengu huo nilimuona mwalimu chimota akiwa buheri wa afya tena akiwa amesimama eneo lile lile la shule ambako paredi ya wanafunzi ilikuwepo.
Nilitaka kujaribu kama nina guvu ya kifanya jambo lolote, niliinuka pale nilipolala na kisha nikaanza kuzipiga hatua zangu, lakini nishangazwa na hatua zangu kuwa ndefu sana yaani hatua moja ilikua ni sawa na hatua mia moja za kawaida.
Wazo langu lilikua moja tu, nipate kujua mwili wa mwalimu chimota ulipo ikiwa nafsi yake niliiona mahali tulipokusanyika.
Nilipowaza hivyo tu, ghafla nilijikuta pembeni kidogo ya shule, nyuma ya vyoo vya wasichana na chini ulikuepo mwili wa mwalimu chimota ukiwa unatoa machozi hakika niliona huruma sana nami nilijikuta nikidondosha machozi kisha nikawaza kurudi ilipokua paredi ya wanafunzi.
Nilifika na kumkuta baba akiwa kashafika, na tayari niliona kachanganyikiwa kabisa kwani ilionesha nimepoteza maisha.
Hakika nilimuonea huruma sana baba nami nilijikuta nikilia katika ulimwengu huo, lakini nilishangaa kuona mwili wangu nao ukitoa machozi ambapo baba aliyafuta kupitia kitambaa chake.
Macho yangu yaliangaza huku na kule na hapo nilimuona mwalmu chimota, nililikuta nikimfuata mwalimu chimota lakini kadiri nilipomkaribia ndivyo nae alizidi kunikimbia, name niliongeza mwendo nae aliongeza mwendo vivyo hivyo.
Nilipomkaribia nilianza kusikia makelele ya mwalimu chimota akilalamika kwamba anaungua, na nilipojiangalia niliona kweli nilikua nawaka moto.
Nami sikusita kumuamuru arudi kwenye mwili wake na apate kuamka.
Katika hali isiyo ya kawaida mwalimu chimota alitii, na baada ya muda aliinuka akiwa uchi wa mnyama na kuanza safari ya kwenda kwenye paredi.
Kisha akili yangu ikanituma nirudi tena, maeneo ya paredi ambapo sikuweza kuuona mwili wangu, wala baba yangu hakuwepo hakika nilichanganyikiwa sana na kisha nilianza kukimbia kwa nguvu na nilikua sikanyagi chini.
Nilifika nyumbani na kumkuta baba yangu akiwa kwenye chumba maalum ambacho hakumruhusu mtu yoyote kuingia.
Nilishangaa sana kukutana na mafuvu mengi na mifupa ya watu kutoka sehemu tofauti tofauti, ac ha hivyo vyote ndani humo mlikua na vibuyu vingi sana ambayo sikuelewa baba aivitumia kwa kazi gani.
Baba alikua amekaa chini na pembeni ulikuepo mwili wangi, hapo nilimuona akiwasha udi pamoja na kufukizia ubani,.
Taratibu niliona nikianza kupoteza nguvu na kichwa change kilianza kuona marue rue tu. Nilipata wazo la kutoka nje ya nyumba ambako nilishangaa kumuona asia akiwa na kibuyu cheusi ambacho mara nyingi kinanitokea kwenye ndoto.
Hakika nilipata hasira sana kisha nilimsogelea asia ambaye aliponiona alistuka sana na nilimuona akitetemeka kisha akaninyooshea kibuyu cheusi lakini alishangaa kuona nikimfuata bila kumuogopa.
Taratibu nilimuona asia akianza kurudi nyuma na kisha kuanza kukimbia kuelekea porini. Hakika sikutaka kumuacha asia nilitaka kuhakikisha ananipa siri ya kibuyu kile na kwanini kila siku kinitokee ndotoni.
Taratibu nilianza kumuona asia akichoka na kisha alibadilika na kuwa popo mkubwa na alipotea kwenye upeo wa macho yangu.
Niliamua kurudi na kumkuta baba akiwa anaendelea na zoezi lake hukua akiongea maneno ambayo sikuweza kuyaelewa.
Nilisogea ulipo mwili wangu na kulala juu yake ambapo nilianza kupiga chafya nyingi mfululizo na kisha kufungua macho yangu, baada ya kuyafikicha kwa muda.
Hakina nilijiona ni mchovu sana na kwa mara ya kwanza niliongea na baba
“baba nasikia kiu naomba maji”.Niliongea
ambapo baba aimuita mama ambaye mara ya mwisho nilimuona akiwa ameshika tama sebuleni.
Haukupita muda mama alikuja na jagi la maji pamoja na kikombe name sikusita kunywa maji yote ambayo yaikua ni lita mbili mpaka wazazi wangu walishangaa.
Kisha niliketi na kuegamia ukuta, nilikua kimya kabisa na wazazi wangu walinitazama tu bila kusema chochote.
“nadhani sasa umeshatambua kwanini nilikua nakukataza kuwa karibu na asia tena ushukuru nyota yako inang’aa na kuwafanya wachawi wakuone unawaka moto, hio ndiyo pona pona yako”. Alianza kuongea baba na kunifanya niwe makini kumsikiliza na alipomaliza nilianza kumuhoji.
“kwahio asia ni mchawi? Na mwalimu chimota je”. Nilihoji swali hilo ambapo baba aliguna kabla ya kulijibu
Je nini kilifuata