SEHEMU YA TANO (05)
ENDELEA; “SHIKAMOO!” nilimsalimu mwalimu chimota naye alijibu bila wasi huku akiingia kwenye gari lake.
“marahaba dogo hujambo”. Alijibu
“sijambo tu mwalimu”.
Baada ya salamu mwalimu chimota aliondoa gari maeneo ya nyumbani na safari yake iliishia kwa mzee simfukwe aliyekua akisifika kwa ufugaji wa kuku kijijini pale.
Alifika na kukaribishwa mpaka ndani nae hakusita kuingia na kumuelekeza kuwa alikua na shida ya kuku, jogoo mweupe na tetea mweusi.
“wapo wengi tu unataka wangapi?” alihoji mzee simfukwe
“nataka kuku wawili tu, jogoo mweupe na tetea mweusi”. Aliongea mwalimu chimota
“kuku wameshatoka nje, naomba jioni uje wajukuu zangu watakukamatia”. Aliongea mzee simfukwe
Mzee wa makamo anaeendesha maisha yake kwa ufugaji wa kuku pamoja na kilimo.
Bada ya makubaliano hayo mwalimu chimota hakuweza kukaa tena nyumbani kwa mzee huyo zaidi aliacha pesa na kuwasha gari kisha kuondoka kwenda nyumbani kwake ambako ndiko shule ya wasa sekondari ilipo.
Alifika na kuwakuta wanafunzi wakiwa paredi, lakini kwa mbali aliweza kumuona kiumbe akiwa mrefu kuliko wanafunzi wote huku akipitiliza hata jengo la ofisi ya walimu.
Hakika walimu chimota alistuka sana na almanusura angonge ukuta wa darasa, mwalimu chimota alienda moja kwa moja nyumbani ambapo alifika na kukuta nyumba yake ikiwa chafu na yenye matakataka mengi nje.
Aliyapuuzia kwani alitambua huenda takataka zile zimeletwa na kimbunga ukizingatia yalikua ni majira ya kiangazi, alizipiga hatua zake kuelekea ulipo mlango wa kuingilia ndani, alipofika mlangoni alishangaa kukutana na ujumbe ulioandikwa kwenye karatasi nyeupe na ilionesha dhahiri iliandikwa kwa damu.
Hakika maneno yaliyoandikwa kwenye karatasi ile ilikua na maneno mazito ambapo hata ungelikua wewe ungetetemeka baada ya kuyasoma.
“maandishi haya nimeyaandika kwa damu yako mwenyewe, achana na jambo hili kabisa la sivyo nitakumaliza na hilii ni onyo la mwisho kabisa”.
Chimota alistuka sana mstuko alioupata hauwezi kulinganisha na kitu chochote kwani almanusura azimie, tumbo la kuhara lilimpata ghafla na alijikuta akitamani kwenda uwani kwaajili ya kujisaidia.
Haraka alichota maji kwenye bomba lililokua pembeni ya nyumba yake na moja kwa moja kwenda maliwatoni, alistuka sana pindi alipoingia maliwatoni baada ya kuona moshi mweusi wenye harufu kali ukitoka kwenye tundu la shimo la choo.
Moshi ule ni kama ulikua na sumu kwani mwalimu chimota alizimia na kuanguka chooni punde tu baada ya kuivuta hewa ile.
Chimota alizinduka na kujikuta akiwa chooni majira ya jioni, viungo vilimuuma sana pia harufu mbaya ya kinyesi ndiyo ilimchefua kwani kila mahala alipoenda nzi walimfuata.
Alipokumbuka masheriti aliyopewa ya kutokuoga alichoka sana, kwani aliwaza angewezaje kufika siku ya kesho pasina kuoga wala kubadili nguo?
Akili yake ilimtuma kuangalia dawa aliyoiweka mfukoni, na alipopapasa tu hakuiona, na hakuishia hapo bali aliingiza mkono mfukoni na alikuta ujumbe badala ya ile dawa.
“huwezi zima moto kwa moto zaidi utachochea moto uwake na ukolee zaidi, chimota ni lazima ufe”.
Moyo wa chimota ulipasuka paaaaah! Kwani alijiona kwamba tayari ameshakufa japo yapo alikua buheri wa afya.
Mikono yake ilitetemeka kwa wasiwasi, mdomo wake pia ulianza kutetemeka kama mtu anayesikia baridi kali sana.
Chimota hakutaka kulala tena nyumbani kwake na aliamua kupiga simu kwa mganga, ambapo simu iliita na kisha kupokelewa.
“kosa ulilolifanya ni kupita kwa yule mzee”. Aliongea mganga kabla hata ya salamu kisha kukata simu na kumuacha chimota akiwa kwenye hali ya sintofahamu .
………………………………………………………………………………………………………………………………………………....................
“karibu sana justice simangwa kwenye
ulimwengu huu jisikie uko nyumbani na haujapotea njia kabisa”.
Ilisikika sauti ya mzee mmoja wa makamo ambaye nilimfahamu kabisa na alikua wa pale pale mtaani
“baba yako amenieleza kila kitu kuhusu wewe, name nitakupa nguvu ya kuweza kuangamiza uchawi mweusi ambao unatufanya wachawi wote tuonekane wabaya”.
Aliongea mzee huyo wakati huo mimi nikiwa kimya kabisa, mazingira tuliyokuepo niliyafahamu kwamba ni ya uwanja wa shule ya wasa.
Niliona aibu sana na muda mwingi nilikua nikificha jogoo wangu kwani tulikua uchi wa mnyama lakini hakukua na mtu aliyeonekana kujali mambo ya mwenzake.
Baada ya kusema maneno hayo mzee Yule alichukua usinga wake na kuanza kuupepeza kisha ghafla kilitokea kibuyu chenye angi ya njano kilichonakshiwa na shanga nyeusi.
Mzee Yule alinisogelea mimi na kuniamuru nisimame name nilitii, kisha akaanza kuupepeza usinga wake kwenye paji langu la uso huku akiongea maneno ambayo sikuyaelewa kabisa.
Alipomaliza kuyasema maneno hayo, alinyoosha mkono wake juu na kisha kikatokea chungu cheusi ambacho ndani kilikua na damu kisha akaniamuru ninywe.
Hakika ulikua ni mtihani mgumu sana, kabla ya kufanya jambo lolote nilimtazama baba yangu ,ambaye alinipa ishara ya kwamba ninywe na nisimuangushe.
Nilipiga moyo konde na kuinywa damu iliyokua kwenye chungu kile ambapo baada ya kumaliza, shangwe zilisikika si kina mama wala kina baba wote walishangilia kwa nguvu na ngoma zilipigwa.
“hatimaye tumekamilisha zoezi la kumpokea mwanachama mpya katika chama chetu cha uchawi, tutajipongeza kwa kula nyama na mwisho kila mmoja ataenda kwake”.
Baaada ya kusema maneno hayo moto mkali uliwaka na kisha kina mama wawili waliokua ndani ya vazi la kaniki walisogea mbele wakiwa wamebeba miili miwili ambayo sikuelewa ni ya kina nani lakini ilionesha ni maiti mbili za kiume.
Kisha bila huruma walikata vipande vipande na kila mmoja alokua eneo lile alipanga foleni kwaajili ya kupata kipande cha nyama.
Mzee Yule mwenye ndevu nyingi na mvi nyeupe aliniamuru niwe wa kwanza kupata kipande cha nyama.
ambapo nilisogea pia baba alifuata na alikua nyuma yangu alihakikisha nafanya kila jambo linalotakiwa kwa usahihi.
Baada ya kupokea kipande cha nyama nilikaa pembeni nikisubiri kuelekezwa ijapokua nilijua kabisa kinachofuata ni kula nyama ile ya binadamu mwenzangu.
Je nini kilifuata