Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,931
- 24,816
Wawili nimesha waadhibu akiwemo umugaka mwenyewe nimemshusha kabusha kadogo tu siku mbili tatu kamsumbue ili arudishe heshima. Alianza jisahau sana yule dogo. Sasa wanaonitishia maisha nimewaonya tu wasifikiri mi wa mchezo.😃😃😃Sasa ya nn kutishiahiana maisha
Mimi ni novel author. Kuhusu kisa ni Cha kweli haya mambo yapoe na yalishatokeaUmejitahidi kwenye kiswahili si kibaya. ila hii si story ya kweli. Si lazima ukitunga story useme ya kweli humu watu wanakuja kuburudika tu kisha wanashika hamsini zao. So haina haja kusema story ya kweli n.k pia usiifanye iwe ya kufikirika saaaaaana.
🤔🤔Ulimfanyia kama yule mfanyakazi wa kazini kwako😱😱Wawili nimesha waadhibu akiwemo umugaka mwenyewe nimemshusha kabusha kadogo tu siku mbili tatu kamsumbue ili arudishe heshima. Alianza jisahau sana yule dogo. Sasa wanaonitishia maisha nimewaonya tu wasifikiri mi wa mchezo.
Yes....kidogo tu. Yeye anacheza na sisi wapemba.🤔🤔Ulimfanyia kama yule mfanyakazi wa kazini kwako😱😱
Haya mengine nisiseme sana maana mshasema tunatumia majini n.k ila dogo nimempokea mimi town na kumfundisha anakuja kuponda huku JF?ambako nlimuingiza mimi mwenyewe.Au wewe ndo bwana ally mpemba
Asante mkuu nimesikia nimefikia
Kuna mengi yamejificha kwenye ule Uzi, ngoja tuone Hadi mwisho😃😃Haya mengine nisiseme sana maana mshasema tunatumia majini n.k ila dogo nimempokea mimi town na kumfundisha anakuja kuponda huku JF?ambako nlimuingiza mimi mwenyewe.
Kumbe wewe ni mpemba Ndiomana ulimvaaa Umughaka kweli lol! Kwani nawewe ni mutu ya shirki mkuu??? Au wapenda wote ni watu wa shirki???Ndani ya nyumba. Jamaa wataku mind sana kwa nini umeniita.....😂
Nisiseme mengiKumbe wewe ni mpemba Ndiomana ulimvaaa Umughaka kweli lol! Kwani nawewe ni mutu ya shirki mkuu??? Au wapenda wote ni watu wa shirki???
Nimeuliza tu natanguliza samawani
Juzi Jana na Leo,...... Nipo Mwalimu,
Tupo mkuuInvite watu kadhaa wajumuike katika huu Uzi.
GoPPiii.Kwanza nianze Kwa kutoa disclaimer kisa hiki ni Cha kweli majina yaliyotumika hapa ni ya kweli bila kubadili chochote ilirekodiwa NAMI nikaihamisha kimaandishi kama ilivyo.
MWANZO
Kwa majina naitwa justice simangwa mkazi wa mkoa wa songwe katika wilaya ya mbozi kijiji cha msia, nilizaliwa katika familia ambayo naweza kusema ni masikini ijapokua tulikua na uhakika wa kupata chakula na kula milo mitatu kabisa.
Suala la kula halikua tatizo kwani kwa maisha ya kijijini ukikosa chakula basi wewe ni mzembe kupitiliza, yaani hata kula kwa jirani umeshindwa.
Kijumba cha nyasi cha vyumba vitatu ndicho kilichonikuza hadi kufikia umri wa miaka kumi na tano na hapo nilianza kujiona ni mkubwa kwani hata shuleni tulifundishwa kwamba unapoanza kubalehe basi ndio dalili ya kuuanza ukubwa.
“hivi utakua lini wewe”. Ni sauti ya baba akiongea kwa ukali na kunifanya nikasirike sana, kwani kila siku baba huniambia mimi ni mtoto ilhali nilijiona nimeshakua sasa
“kwani nimefanyeje baba?” nilihoji kwa mshangao kwani sikuona sababu ya baba kunikoromea kiasi kile na ukizingatia ndio nikwanza nilikua narudi kutoka shuleni.
“hivi ni mara ngapi nakukanya kuhusu kuongea na asia, Yule binti wa mzee mwashilindi?” aliongea baba na safari hii macho yake yalishaanza kuwa mekundu ma ishipa yake ilimtoka kuashiria amekasirika sana na hapendi mambo ninayoyafana.
Kwa vile, namtambua baba akiwa amekasirika, sikutaka kuendelea na majibizano zaidi nilikua mpole kama nimenyeshewa na mvua kisha nikachukua begi langu na kwenda chumbani moja kwa moja.
Ambapo nilifika na kulirusha kitandani na kisha nami nilifuata na haukupita muda tangu nilipouweka mgongo wangu juu ya kitanda usingizi ulinipitia, hii ni kutokana na kuchoka na umbali kati ya shule ya sekondari wasa na makazi yetu yalipo.
Nishituka baada ya kuhisi nimeguswa na kitu Fulani, na nilipofungua macho yangu tayari nilikutana na baba ambaye aliniamuru niamke haraka kwani kulikua na kazi ya kuhamisha vitu kutoka kwenye nyumba ya nyasi na kuvipeleka kwenye nyumba yetu mpya.
Sikua na namna na nilipoangalia nje kulikua kweusi lakini giza lilikua halijatanda kabisa, na kwa kukadiria ilikua ni saa moja usiku.
Nilijiuliza sana kwanini baba hakusiema tuhamishe vitu mchana mpaka aseme tuhamishe muda ule, maswali yangu hayakuweza kuishia moyoni tu na moja kwa moja niliamua kumuuliza baba swali hilo ambaye alinikata jicho kali hadi niliogopa.
Baba hakunijibu hilo swali wala mimi sikuhitaji tena jibu la swali lile kwani nilishatambua kuwa baba hapendi.
Baada ya kumaliza kazi hio ya kuhamisha vitu mama alipika chakula na kisha tulikula, name baada ya kula nilienda chumbani na kuchukua madaftari yangu kwa lengo la kujisomea , lakini nilishangazwa na uvivu niliokua nao siku hio, niliposhika daftari nilisinzia lakini nilipoliachia nilijiona nisie na uchovu wowote.
Niliamua kupuuzia hali hio na kuyarudisha madaftari yangu kwenye begi kisha kulivuta blanketi langu tayari kwa kulala tena na nilipanga ningeamka kusoma usiku wa manane kwani huo ndio muda akili inakua imetulia na kunakua hakuna vurugu.
Majira ya saa nane usiku nilistuka ghafla kutokana na bati za nyumba kupiga makelele sana kutokana na mvua kubwa iliyokua ikinyesha usiku huo.
Hakika mvua ile ilinishangaza sana, kwani ilikua ni majira ya kiangazi, sasa inakuaje mvua kubwa kiasi kile inyeshe majira ya kiangazi.
Nikiendelea kuwaza hayo nilishikia kishindo kikubwa maeneo ya sebleni, hakika kishindo hiki kilipelekea moyo wangu upasuke paa!
Kisha mapigo yangu ya moyo kuanza kudunda kwa kasi, kabla sijakaa sawa niliaza kusikia bati zikigonga gonga kana kwamba kuna vitu vilikua vikicheza.
Nilipata ujasiri kisha haraka niliinuka na kutoka kuelekea sebleni ambapo katika hali ya kustaajabisha niliona kibuyu cheusi chenye shanga zinazowaka kama taa na kukifanya king’ae.
Macho yangu yalinitoka pima na kisha kibuyu kile kikapotea, baada ya hapo kila kitu kilikoma, hata mvua iliyokua ikinyesha iliacha na kukawa swari kabisa.
Sikua na budi kurudi chumbani kwa hofu sana kwani nilichokiona yalikua ni maajabu kwa upande wangu na moyo wangu haukua na amani hata kidogo.
Nilifika na kuvuta shuka
langu na kujifunika gubi gubi nikiwa na hofu sana yote hii ni kuufanya usingizi uwahi kunichukua.
Baada ya kupitiwa na usingizi nilikuaja kuzinduka majira ya alfajiri kama ilivyokua kawaida yangu kuwahi kuamka kabla ya wote na kuandaa kifungua kinywa kabisa kisha kuwahi shuleni.
Na wiki hio ilikua ni ya mwalimu mkali kuliko wote pale shuleni.
Nilijinyoosha na kisha kutoka nje kwa lengo la kuwasha moto lakini nilishangaa sana baada ya kukuta nyumba yetu ya zamani ikiwa imeanguka, haraka niliingia ndani na kumgongea baba ambaye alitoka na kuangalia hali halisi lakini hakuonesha kustuka na chochote.
“tukiwaambia mnakua wabishi”.
Aliongea baba na kisha kuingia ndani akiniacha na maswali mengi sana
Je nini kilifuata
Duh hii ni balaaSEHEMU YA TANO (05)
ENDELEA; “SHIKAMOO!” nilimsalimu mwalimu chimota naye alijibu bila wasi huku akiingia kwenye gari lake.
“marahaba dogo hujambo”. Alijibu
“sijambo tu mwalimu”.
Baada ya salamu mwalimu chimota aliondoa gari maeneo ya nyumbani na safari yake iliishia kwa mzee simfukwe aliyekua akisifika kwa ufugaji wa kuku kijijini pale.
Alifika na kukaribishwa mpaka ndani nae hakusita kuingia na kumuelekeza kuwa alikua na shida ya kuku, jogoo mweupe na tetea mweusi.
“wapo wengi tu unataka wangapi?” alihoji mzee simfukwe
“nataka kuku wawili tu, jogoo mweupe na tetea mweusi”. Aliongea mwalimu chimota
“kuku wameshatoka nje, naomba jioni uje wajukuu zangu watakukamatia”. Aliongea mzee simfukwe
Mzee wa makamo anaeendesha maisha yake kwa ufugaji wa kuku pamoja na kilimo.
Bada ya makubaliano hayo mwalimu chimota hakuweza kukaa tena nyumbani kwa mzee huyo zaidi aliacha pesa na kuwasha gari kisha kuondoka kwenda nyumbani kwake ambako ndiko shule ya wasa sekondari ilipo.
Alifika na kuwakuta wanafunzi wakiwa paredi, lakini kwa mbali aliweza kumuona kiumbe akiwa mrefu kuliko wanafunzi wote huku akipitiliza hata jengo la ofisi ya walimu.
Hakika walimu chimota alistuka sana na almanusura angonge ukuta wa darasa, mwalimu chimota alienda moja kwa moja nyumbani ambapo alifika na kukuta nyumba yake ikiwa chafu na yenye matakataka mengi nje.
Aliyapuuzia kwani alitambua huenda takataka zile zimeletwa na kimbunga ukizingatia yalikua ni majira ya kiangazi, alizipiga hatua zake kuelekea ulipo mlango wa kuingilia ndani, alipofika mlangoni alishangaa kukutana na ujumbe ulioandikwa kwenye karatasi nyeupe na ilionesha dhahiri iliandikwa kwa damu.
Hakika maneno yaliyoandikwa kwenye karatasi ile ilikua na maneno mazito ambapo hata ungelikua wewe ungetetemeka baada ya kuyasoma.
“maandishi haya nimeyaandika kwa damu yako mwenyewe, achana na jambo hili kabisa la sivyo nitakumaliza na hilii ni onyo la mwisho kabisa”.
Chimota alistuka sana mstuko alioupata hauwezi kulinganisha na kitu chochote kwani almanusura azimie, tumbo la kuhara lilimpata ghafla na alijikuta akitamani kwenda uwani kwaajili ya kujisaidia.
Haraka alichota maji kwenye bomba lililokua pembeni ya nyumba yake na moja kwa moja kwenda maliwatoni, alistuka sana pindi alipoingia maliwatoni baada ya kuona moshi mweusi wenye harufu kali ukitoka kwenye tundu la shimo la choo.
Moshi ule ni kama ulikua na sumu kwani mwalimu chimota alizimia na kuanguka chooni punde tu baada ya kuivuta hewa ile.
Chimota alizinduka na kujikuta akiwa chooni majira ya jioni, viungo vilimuuma sana pia harufu mbaya ya kinyesi ndiyo ilimchefua kwani kila mahala alipoenda nzi walimfuata.
Alipokumbuka masheriti aliyopewa ya kutokuoga alichoka sana, kwani aliwaza angewezaje kufika siku ya kesho pasina kuoga wala kubadili nguo?
Akili yake ilimtuma kuangalia dawa aliyoiweka mfukoni, na alipopapasa tu hakuiona, na hakuishia hapo bali aliingiza mkono mfukoni na alikuta ujumbe badala ya ile dawa.
“huwezi zima moto kwa moto zaidi utachochea moto uwake na ukolee zaidi, chimota ni lazima ufe”.
Moyo wa chimota ulipasuka paaaaah! Kwani alijiona kwamba tayari ameshakufa japo yapo alikua buheri wa afya.
Mikono yake ilitetemeka kwa wasiwasi, mdomo wake pia ulianza kutetemeka kama mtu anayesikia baridi kali sana.
Chimota hakutaka kulala tena nyumbani kwake na aliamua kupiga simu kwa mganga, ambapo simu iliita na kisha kupokelewa.
“kosa ulilolifanya ni kupita kwa yule mzee”. Aliongea mganga kabla hata ya salamu kisha kukata simu na kumuacha chimota akiwa kwenye hali ya sintofahamu .
………………………………………………………………………………………………………………………………………………....................
“karibu sana justice simangwa kwenye
ulimwengu huu jisikie uko nyumbani na haujapotea njia kabisa”.
Ilisikika sauti ya mzee mmoja wa makamo ambaye nilimfahamu kabisa na alikua wa pale pale mtaani
“baba yako amenieleza kila kitu kuhusu wewe, name nitakupa nguvu ya kuweza kuangamiza uchawi mweusi ambao unatufanya wachawi wote tuonekane wabaya”.
Aliongea mzee huyo wakati huo mimi nikiwa kimya kabisa, mazingira tuliyokuepo niliyafahamu kwamba ni ya uwanja wa shule ya wasa.
Niliona aibu sana na muda mwingi nilikua nikificha jogoo wangu kwani tulikua uchi wa mnyama lakini hakukua na mtu aliyeonekana kujali mambo ya mwenzake.
Baada ya kusema maneno hayo mzee Yule alichukua usinga wake na kuanza kuupepeza kisha ghafla kilitokea kibuyu chenye angi ya njano kilichonakshiwa na shanga nyeusi.
Mzee Yule alinisogelea mimi na kuniamuru nisimame name nilitii, kisha akaanza kuupepeza usinga wake kwenye paji langu la uso huku akiongea maneno ambayo sikuyaelewa kabisa.
Alipomaliza kuyasema maneno hayo, alinyoosha mkono wake juu na kisha kikatokea chungu cheusi ambacho ndani kilikua na damu kisha akaniamuru ninywe.
Hakika ulikua ni mtihani mgumu sana, kabla ya kufanya jambo lolote nilimtazama baba yangu ,ambaye alinipa ishara ya kwamba ninywe na nisimuangushe.
Nilipiga moyo konde na kuinywa damu iliyokua kwenye chungu kile ambapo baada ya kumaliza, shangwe zilisikika si kina mama wala kina baba wote walishangilia kwa nguvu na ngoma zilipigwa.
“hatimaye tumekamilisha zoezi la kumpokea mwanachama mpya katika chama chetu cha uchawi, tutajipongeza kwa kula nyama na mwisho kila mmoja ataenda kwake”.
Baaada ya kusema maneno hayo moto mkali uliwaka na kisha kina mama wawili waliokua ndani ya vazi la kaniki walisogea mbele wakiwa wamebeba miili miwili ambayo sikuelewa ni ya kina nani lakini ilionesha ni maiti mbili za kiume.
Kisha bila huruma walikata vipande vipande na kila mmoja alokua eneo lile alipanga foleni kwaajili ya kupata kipande cha nyama.
Mzee Yule mwenye ndevu nyingi na mvi nyeupe aliniamuru niwe wa kwanza kupata kipande cha nyama.
ambapo nilisogea pia baba alifuata na alikua nyuma yangu alihakikisha nafanya kila jambo linalotakiwa kwa usahihi.
Baada ya kupokea kipande cha nyama nilikaa pembeni nikisubiri kuelekezwa ijapokua nilijua kabisa kinachofuata ni kula nyama ile ya binadamu mwenzangu.
Je nini kilifuata