MKASA WA KWELI: Ni bora ubaki na umaskini kuliko utajiri wa pesa za "ndagu" au majini

MKASA WA KWELI: Ni bora ubaki na umaskini kuliko utajiri wa pesa za "ndagu" au majini

utajiri wa ndago upo sana..

mm kipindi nakua kuna mzee mmoja hv ni mchaga..jina lake linafanana na mwanamuziki mmoja hvi ambae wameshirikiana sana na chege chigunda kutoa pini nyingi kali(ana majigambo sana)

huyu mzee alikuwa na uwezo wa kawaida sana miaka hiyo ya late 90's...ghafla akaja kuzishika hela nyingi hatari na mpk sa hv yupo vzr sana..ana sheli c chini ya 4 nnazozijua

aliporomosha mjengo mmoja wa maana sana na baadae akajenga Sheli hapo hapo kwenye mjengo wake ukiwa unaenda MOSHI BAR(Ingawa kwa sasa hakai hapo)

Familia yake yote imeparanganyika..za chin chin ni kwamba alimtoa mama ake kafara(alimchizisha)
 
utajiri wa ndago upo sana..

mm kipindi nakua kuna mzee mmoja hv ni mchaga..jina lake linafanana na mwanamuziki mmoja hvi ambae wameshirikiana sana na chege chigunda kutoa pini nyingi kali(ana majigambo sana)

huyu mzee alikuwa na uwezo wa kawaida sana miaka hiyo ya late 90's...ghafla akaja kuzishika hela nyingi hatari na mpk sa hv yupo vzr sana..ana sheli c chini ya 4 nnazozijua

aliporomosha mjengo mmoja wa maana sana na baadae akajenga Sheli hapo hapo kwenye mjengo wake ukiwa unaenda MOSHI BAR(Ingawa kwa sasa hakai hapo)

Familia yake yote imeparanganyika..za chin chin ni kwamba alimtoa mama ake kafara(alimchizisha)
😳😳😳 Mama?
 
INAENDELEA:

Gado alimfata mzee mmoja pale kijijini na akamuelezea dhamira yake ya kutaka utajiri huu wa NDAGU na akamueleza anataka iwe Siri, yule mzee alikuwa ni mtu anaefahamu sana waganga na alikuwa anajua dawa nyingi za kutibu kienyeji, wakapotea na Gado kwenye vijiji vya mbali huko usukumani na baada ya wiki kadhaa wakarejea pale kijijini kwetu na Gado akarudi Arusha.

Kwenda kwa waganga kwa maisha ya kijijini ni jambo la kawaida lakini hakuna mtu aliyefikiria Gado ameenda kutafuta Utajiri huu wa kishetani. Mimi nikiwa nimemaliza mitihani yangu ya S/M najiandaa kwenda kidato cha kwanza shule niliyopangiwa huko mikoa ya mbali. Kabla ya X-Mass ilikuwa December Gado akaja tena kijijini kusalimia na wakapotea tena na yule mzee kwa wiki kadhaaa kabla ya kurudi na kuondoka tena.

Mimi nikaondoka Pale kijijini nikaenda masomoni sikuwa na simu wala mawasiliano na watu au ndugu wa pale kijijini kwetu zaidi ya wazazi wangu nikawa narudi likizo tu baada ya miezi 6.

Likizo ya 2006 narudi pale kijijini nasikia stori za Gado ni tofauti kabisa Jamaa alikuwa tajiri wa kutisha pale kijijini, alijenga nyumba nzuri kabisa na ya kisasa pale nyumbani kwa mama yake ukiachana na ile aliyojenga kaka yake. Kijijini kwetu kulikuwa hamna umeme.

Umeme ulikuwa mbali zaidi ya 50km huyu mwamba akawafuata tanesco akawaambia wampigie mahesabu ya nguzo na gharama ya Transformer ili kuutoa umeme umbali huo mpaka nyumbani kwao TANESCO chapchap wakafanya hii kazi umeme ukaingia Hadi kwao na akanunua transformer kwa pesa zake ambapo mpaka leo ndiyo inayotumika pale kijijini, na kwa mara ya kwanza kijijini kwetu kukawa na umeme na nyumba ya kisasa kabisa Kama zilizoko mjini.

Huyu mwamba alikuwa na pesa sana, pale kijijini Kuna jamaa alikuwa ndio anaonekana tajiri alikuwa na ng'ombe zaidi ya 600, siku moja wakatofautiana kimaongezi na huyu jamaa akaenda mnadani alinunua zaidi ya ng'ombe 400 katika minada tofauti tofauti akaziweka pale kwao akaona haitoshi akaenda kununua zingine minada mingine akawa anaweka kwa rafiki zake.

Baba yake tayari alikuwa ameshahamishia makazi kwenye nyumba kubwa ambapo ni kwao kwa mama yake. Mzee alikuwa anapanda ndege kwenda mikoani kufanyiwa checkup za kiafya Kama daladala vile. Story ikawa ni GADO pale kijijini. Alipokuwa anakuja pale kijijini wazee walikuwa wanampisha kiti akae wao wanasimama au wanachuchumaa hata pale jamaa alipokuwa anakataa Hawa wazee wakawa hawataki. Cha kushangaza huyu jamaa sio mkubwa kiumri amezaliwa 1980's. Pesa si mchezo aisee.

Gado akawa ananunua VX na V8 Kama Sasa tunavyonunua IST marafiki zake wakawa ni watu wazito Ma-RPC, wakubwa wengi wakati jamaa hata elimu hana na hata pale alipokuwa anakuja kijijini baadhi alikuwa anakuja nao.

Alijenga ghotofa 3 za maana Arusha na nyumba nyingi sana.
-------
Mwaka 2007 kama sikosei mme wa Sarah akawa anapigiwa simu sana na Gado ahamie Arusha na yeye atamtafutia kazi alimshawishi sana na kupitia mke wake pia akawa anamsihi waende kwa kaka yao awatafutafutie kazi maana tayari kaka yao ameshakuwa na pesa kidogo.

Sasa huyu mume wa Sarah ikabidi amshirikishe mdogo wake ambaye ndio huyo Kiringo anaefanya kazi hapo udsm,Kiringo akamkatalia akamsihi kaka yake abaki na yeye atamtafutia hiyo kazi, Lakini ushawishi wa mwanamke ukawa juu zaidi hali iliyopelekea kumjibu vibaya mdogo wake na kweli wakaondoka kwenda Arusha na mkeww

Kumbe kuna mipango ya Siri ilikuwa imesukwa kati ya Gado, mdogo wake Sarah na mama yao mzazi. Mpaka kipindi hiki wanatoka wanaenda Arusha Sarah alikuwa na mumewe walikuwa na mtoto mmoja wa kike.

Walipofika kule haikukaa mda mume wa Sarah aliumwa usiku ghafla na akafa.
-------
Kwa mujibu wa watu hapa kijijini hakuna mtu yeyote aliyehusisha ule msiba na dhana potofu ilionekana Kama vifo vingine vya kawaida.

Mambo yakaendelea kuwa mazuri zaidi kwa Gado, nakumbuka mwaka mmoja alikuja pale kijijini na Mimi nilikuwepo likizo nilishuhudia anafanya operation ya kuondoa vitanda vyote vya ngozi ama vile vya spring vilivyokuwa vinatumika sana kule kijijini kwenye nyumba za ndugu, jamaa na marafiki zake walikuwa ni wengi akawawekea vitanda vipya vya mbao na magodoro.

Huyu mwamba nadhani alijifunza kutokana na makosa ya Kaka yake, alikuwa hatoi pesa taslimu yeye alikuwa anawanunulia ndugu vitu au anampa pesa mtu mwingine akupe.

Kulingana na ukwasi aliokuwa nao akaoa Traffic mmoja wa kichaga hukohuko Arusha hiyo Harusi yao ilikuwa ni balaa madon na viongozi wa huko Arusha asilimia kubwa walikuwepo, mwamba akapewa jina la Kikwete wa pale kijijini.

Sasa pamoja na huyu jamaa kusaidia sana wazazi na ndugu wengine lakini akawa hasaidii kabisa mdogo wake huyu Sarah na kaka yake mkubwa aliyefirisika Joseph..yaani ukawa ni uhasama kwa huyu kaka mpaka mama yao mzazi anafikia hatua anasema nyumba iliyojengwa na Joseph ni takataka.

Maisha yalimpiga Sarah baada ya kifo cha mumeme ikabidi shemeji mtu (Kiringo) awe anaradhimika kumpa msaada kila mwezi ili ajikimu yeye na mtoto wake.

Hili suala likawa linamuuza sana sarah na istoshe kisa na mume wake kufa ni huyo Kaka yake Gado na alimshirikisha namna ya kufanikisha hilo zoezi kwa ahadi nyingi na yeye akalifanya kwa ustadi mkubwa mpaka kuwezesha mume wake kufa.

Ikafika kipindi Gado akawa hataki kumuona kabisa huyu mdogo wake Sarah yaani akipita njiani kuelekea kwake lazma akutane na Dada yake akichoma mahindi pembenzoni mwa barabara. Jamaa alichokuwa akifanya anafunga vioo vyake vya V8 yake then anapita Kama hamuoni hata salamu alikuwa hataki.
------
Pale kijijini ikawa ni kikwete, Kikwete, Kikwete ndilo jina pekee vijana walikuwa wakilihusudu kulingana na ukwasi aliokuwa nao, vijana nao wakaanza kutafuta waganga wawe Kama Kikwete, wengine walipitia Mikasa ya ajabu sana na hawakufanikisha japo Kuna wengine walifanikiwa leo sitaki kuwazungumia hao.

Huyu jamaa alizidi kuchanua kipesa toka 2005 mpaka namaliza chuo bado jamaa Yuko juu...alikuwa na magari hayahesabiki...mama yake akahimishia makazi Arusha lakini bahati mbaya hawakuwezana na mke wake hivyo akajengewa nyumba nyingine ya ghorofa huko huko Arusha.

Cha kushangaza huyu mama akawa anaona binti yake anateseka na anaishi kwa kuchoma mahindi Wala yeye hakujali. Sarah akachukia hii hali sana.

Sasa ilikuwa kama miaka ya 201... Siku moja Sarah akapata taarifa Kikwete (Gado) ameenda kwa mama yake kumsalimia nae akaenda kwa kushtukiza...na kukawa na baadhi ya watu wa kule kijijini akiwemo mfanyakazi wa ndani alitolewa huko kijijini kwetu. Binti Sarah alifika pale amefura mno.

Mkononi alikuwa ameshika ukuni wa mbao..moja kwa moja kwa mama yake piga bao la kwanza kichwani ile watu kuhamaki akampa la pili wakamshika akiwa anahema Kama mtu anaetaka kuzimia...pale ndani pakawa ni patashika wageni walipkuwepo wanashangaa nini hiki.
-----
Watu wakawa wanashangaa mbona Sarah anajikulia laana ya kumpiga mama yake, lakini kila mtu akataka kufahamu Kuna nini hasa.

Baada ya mda Sarah akawa vizuri akaanza kutukana mama yake na huyu Kikwete watu wakiwa bado wako midomo wazi na hapa ndipo alipotoa siri.

Kumbe walipanga mume wake Sarah atolewe kafara ili Gado awe tajiri zaidi na Gado na mama yake ndiyo walimshawishi Sarah kuhusu hili na Sarah akaahidiwa atajengewa nyumba nzuri ya ghorofa, gari nzuri pamoja na biashara, Sarah alishiriki kikamilifu kutoa baadhi ya vitu kutoka kwa mumewe vilivyokuwa vinahitajika kwa mganga ili kufanikisha kumuua mume wake na ile mbinu ya kumshawishi ahamie Arusha akatafutiwe kazi nzuri zaidi ilikuwa ni kumsogeza karibu na wasuka mipango

Sasa kibaya zaidi Gado alipopeleka vile Vifaa alivyoagizwa na mganga akapewa masharti na mojawapo ya hayo masharti ni kutokusaidia kabisa baadhi ya watu Sarah nae alikuwemo kwenye hiyo list.

Hizi habari zikazaagaa Kama upepo pale kijijini, mashemeji wa upande wa pili nao wakazipata habari za undani wa kifo cha mtoto wao hawakuwa na jinsi zaidi ya kuhuzunika ikizingatiwa wao wako kwenye misingi ya kiimani zaidi.

Huyu Bwana Kiringo alimfuata mtoto wa kaka yake akarudi nae Dar ili amsomeshe na hakukuwa na pingamizi kwenye hili maana tayari Sarah hakuwa na msaada.

Pamoja na hayo Kikwete Wala hakutishika alizidi kuchanua tu japo kukawa na bifu na Sarah pamoja na Joseph.
------
Huyu Gado akaendelea kuwa tajiri sana mwenye ukwasi wa kufa mtu, nakumbuka mwaka 2015 alimuita ndugu yangu mmoja hotelini pale Musoma mjini baada ya kuja kusalimia kijijini Hawa walikuwa hawajaonana siku nyingi katika maongezi yao aligusia kwamba kwa mda ule alikuwa na akiba bank kama 400m hivi.

Jamaa akawa anaogolea kwenye ukwasi na pale kijijini akawa anaheshimika sana na akawa tayari amepata watoto wawili na yule mkewe traffic. Kitu nilichogundua ukiwa na pesa hata watu wakijua ni za madhara bado watakuheshimu na kukunyekea tu yaani huyu jamaa alikuwa ananyenyekewa pale kijijini utafikiri mfalme.

Kuna mwaka, mama mkwe wa Wasosi ambaye Sasa ni shemeji yake na huyu Gado maana Kaka yake ni yule aliyetolewa kafara akafariki pale kijijini na Mimi Kama kijana nikaenda kushiriki ule msiba, Cha kushangaza Gado sijui alipata wapi Ujasiri akafunga safari kuja msibani.

Pale Msibani alikuwepo mama yake Wasosi pia, wakawa wamepata taarifa za ujio wake huyu mwamba msibani jamaa alipofika na mkewe lile gari tu kuingia yule mama yake Wasosi alipiga ukunga ambao sijawahi uona Aisee huku akilalamika kwa uchungu na kutukana..nanukuu baadhi ya maneno ninayayakumbuka..." Uwiiiiiiiiiii mbwa wewe, Shetani mkubwa umemuua mwanangu Sasa wewe unafurahia na maisha, umeuua mwananangu, kweli umeuua mwananangu au hiyo gari ndio mwanangu" huyu mama alikiwa akiongea haya huku akionekana kuishiwa nguvu.

Wabibi wenzake wakawa wanamtuliza na baadhi ya wazeee lakini hali ya pale Msibani ikawa sio nzuri japo jamaa hakuonekana kujali kabisa..na baada ya kuzika yeye akaondoka.

Mimi nilikuja kuondoka pale kijijini nikaendelea na harakati za kutafuta maisha mikoani, mwaka juzi nikapata habari za huyu mwamba kwamba ameanza kufirisika ..kweli mpaka nakuja Arusha huyu Gado amebaki na Ghorofa moja tu zingine zote ameshauza na hata gari Hana..mke alishamkimbia nadhani hata hii ghorofa itauzwa mda si mrefu sijui alikosea wapi kwenye masharti yake huyu mwamba.

Mishe zimemgomea kabisa, Hana pesa tena.

Kibaya zaidi familia imeshaparanganika baba yao alishafariki.., watoto wote na mama hawaaminiani tena na hata upendo kati yao haupo kabisa yaani wanapitana Kama unavyompita mtu njiani..wanaishi kwa kuviziana sana.

Huyu mkubwa Joseph kwa Sasa ni Dereva Merelani hapo na afadhari amerudi kupatapata vipesa yuko njema kiasi chake kwa Sasa.

Yule mtoto wa Sarah, kwa Sasa ni binti mkubwa yuko vidato kadhaa na anajua kila kitu kuhusu stori ya kifo Cha baba yake, binti ana kisasi sana na Hawa ndugu ndugu zake.

kupitia kwa watu na hata Joseph mwenyewe anasema binti amesema hawatambui akiwemo mama yake mzazi Sarah na hajawahi hata kwenda kuwasalimia hata kwenye simu.

Maisha yao yamegeuzwa kuwa Arusha japo kwa Sasa yamekuwa magumu sana wanaona soni kurudi pale kijijini tena na pale Kijijini Kuna miamba mipya iliyofuata nyayo za Gado imeibuka ndio inatawala sasa.

Sarah kachoka sana hadi anatia huruma.

.................................................

Hiki kisa ni cha kweli na hakijatokea miaka mingi. Ukiwa unatoka mwanza au Bunda na unaenda Musoma mjini au Tarime shuka hapo sabasaba mbele ya kiabakari na Mazami. Hapohapo barabara kuu ya Musoma ulizia kwa mzee Nyanda au uliza mtu yeyote hii stori ukifika sabasaba.

Kwa mlioko mjini unaweza kumuona huyo Kiringo hapo udsm na atakupa huu mkasa uliochukua maisha ya kaka yake.

Poleni kwa uandishi wangu mbovu.

Niko zangu sitimbi now mapumziko naangalia madon wapya walioibuka.
Kiufupi nimekuelewa,coz mm ni mkazi wa. Bunda nimefuatilia hii story ni kweri
 
utajiri wa ndago upo sana..

mm kipindi nakua kuna mzee mmoja hv ni mchaga..jina lake linafanana na mwanamuziki mmoja hvi ambae wameshirikiana sana na chege chigunda kutoa pini nyingi kali(ana majigambo sana)

huyu mzee alikuwa na uwezo wa kawaida sana miaka hiyo ya late 90's...ghafla akaja kuzishika hela nyingi hatari na mpk sa hv yupo vzr sana..ana sheli c chini ya 4 nnazozijua

aliporomosha mjengo mmoja wa maana sana na baadae akajenga Sheli hapo hapo kwenye mjengo wake ukiwa unaenda MOSHI BAR(Ingawa kwa sasa hakai hapo)

Familia yake yote imeparanganyika..za chin chin ni kwamba alimtoa mama ake kafara(alimchizisha)
Jamaa Hana familia kwa Sasa?
 
Back
Top Bottom