Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Je hizo dini nyingine au madhehebu mengine yanazo miundombinu kama ya hao walalamikiwa? Je wanayo hospitali kama Bugando au KCMC? Je wanavyo vyuo vikuu kama Tumaini au SAUT au ST Johns?GT,
..at first nilibabaika na nikaona serikali inajitumbukiza ktk masuala ya kidini.
..lakini baada ya kutulia na kutafakari nadhani hii MOU haina matatizo.
..hata mataifa makubwa kama MAREKANI yana ushirikiano kati ya SERIKALI na FAITH BASED organisations.
..sidhani kama hiyo MOU inaelekeza serikali ktk kusaidia Kanisa ktk shughuli zake za kiroho.
..kwa mazingira yetu Tanzania serikali inapaswa kushirikiana na mashirika ya kidini ktk urahisishaji wa utoaji wa huduma za kijamii kama elimu, afya, maji,mazingira etc.
..kama taasisi ya kidini imejenga hospitali na inatoa madawa na chakula sioni ubaya wa serikali kuwasaidia ktk kutoa waganga na wauguzi na kuwalipa mishahara. ushirikiano wa minajili hiyo nadhani ndiyo unaoelekezwa na MOU hiyo.
..pia tangu kusainiwa kwa MOU hiyo sijaona dalili zozote zile za serikali kuipendelea dini moja dhidi ya nyingine.
..tumeshuhudia serikali ikifadhili mkutano wa Bakwata, ikitoa majengo kwa chuo cha Kiislamu, na kusaidia kutatua ile sakata ya mahujaji kukwama kwenda hijja. pia tumeona serikali ikirudisha shule za kanisa zilizokuwa zimetaifishwa, tumeona viongozi wakuu wakishiriki fundraising za ujenzi wa shule za kanisa etc etc. vilevile kiongozi wa mabohora ametembelea nchini na kupokewa kwa heshima zinazostahili.
..badala ya kukaa pembeni na kulalamika labda madhehebu mengine nayo yachukue initiative na kusaini MOU na serikali kama ambavyo makanisa yamefanya. lakini with or without MOU sidhani kama serikali ina nia ya kubagua madhehebu yoyote ya dini.
Mara nyingine kuzidi kulumbana nao ni kuwapa umaarufu wasiokuwa nao. Wao utasikia kwenye kujiunga na Al Shabab, Kupokea tende za msaada na kutaka Mahakama ya Kadhi na mashindano ya kuhifadhi Quran tu. Hawajui mambo ya msingi ambayo jamii inahitaji