Mkataba wa Bandari: Mbunge Aida Khenani akiri kupelekwa Dubai, lakini mpaka wanarudi hakujua walikwenda kufanya nini

Aida kasema neno muhimu sana ,kuwa taharuki hii inatokana na Hofu tuliyonayo kutokana na uzoefu wa mikataba kadhaa ambayo tumeingi huko nyuma ambayo Watanzania tumepigwa na imeonekana haina maslahi kwa Taifa.

Hoja hi ni ya msingi.sana.

Na m,zee mboe yeye katahadharisha kuwa hili suala ni la Kimuungano, kwa nini bandari za Zanzibar hazimo?
Ukweli ni kuwa Waziri alijibu kuwa Mkataba huu unaihusu bandari ya Dar es salaam tuu.

Ila ikonekana kuna ufanisi tunaweza kungia kwenye mikataba ya nyongeza huko mbeleni .

Ama hili la Kimuungano kuwa Bandari ni za Muungano kweli limo ndani a Katiba, ya 1977. lakini ukweli ni kuwa katiba hii haitumiki tena tanzania, Serikali ya CCM inatuma Akili na uzoefu tuu.
Tazama hapo chini:
_________
NYONGEZA YA KWANZA
_________
(Imetajwa katika ibara ya 4)
Mambo ya Muungano
1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
2. Mambo ya Nchi za Nje.
3. Ulinzi na Usalama.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje.
9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
10.Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,
ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa
nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.

11.Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na
simu.

12.Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya
malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja
mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;
fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika
na fedha za kigeni.
13.Leseni ya viwanda na takwimu.
14.Elimu ya juu.
15.Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya
motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo za
mafuta au bidhaa, na gesi asilia.

16.Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote
yanayohusika na kazi za Baraza hilo.

17.Usafiri na usafirishaji wa anga.
18.Utafiti.
19.Utafiti wa hali ya hewa.
20.Takwimu.
21.Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
22.Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengine
yanayohusiana navyo.

Article nilizo tia Rangi zina utata mkubwa , CCM wenyewe upande wa ZNZ na Tanganyika hawakubaliani ,
Zanzibar wan baraza lao la Mitiani,
Zanzibar wanakusanya kodi kwa idara yao inayoitwa ZRB(zamani) /(sasa ZRA)
zanzibar wana simamia Bandari yao wenyewe (ZPA) iko chini ya SMZ
Zanzibar inapata shida sana kukopa , ndo maana inataka itolewe kwenye Muungano suala la Mikopo.
Zanzibar imekwama kwa kushindwa kutowa leseni za Viwanda, Kila kiwanda kinapoanzishwa Zanzibar Tanganyika inadai Haki ya Kutoa leseni na Kupata Mrejesho wa Kodi, Kiwanda kinakufa au kufungwa.


Mh.Mbowe hapa ndipo alipolenga na kuonesha Mgogoro tulionao kitaifa.


Ama Upande wa Jamuhuri ya Muungano imeshindwa hadi leo Kufungua Account Ya pamoja ya Muungano ambayo imo ndani ya Katiba.Imeshindwa kutekelezwa na kuisababaishia Zanzibar kukosa stahiki yake katika Mgao wa Muungano.
Hili likoUpande wa Tanganyika nalolimekwama.

Tanganyika lazima Irudi na Zanzibar ipewe mamlaka kamili.
 
Tuungane na wabunge kufanya maandamo ya Amani kuupinga huu utumwa.
 
Kipengele gani ch mkataba kimesema rasilimali zimeuzwa?
Ukodishwaji wa bandari itahusisha bandari zote za maziwa, bahari na mito. Mwisho wa mkataba ni mpaka shughuli za.bandari zitakapokoma. Itakuwa wanamaanisha mwisho wa dunia. Kipengele hicho hapo. Kasome mkataba wewe sasa utuambie kama hakipo
 
Baada ya Hii ziara ilitakiwa wapelekwe Wataalamu wetu wa bandari wajue huo mfumo na uanze mchakato wa kuupata. Tunacho Chuo cha Bandari kiwezeshwe kututengenezee Wataalamu wakuwezesha efficiency!
Unaambiwa mkataba ulishasainiwa a year before
 
Mazingira ya watu kulamba asali yapo wazi kabisa, na hili ni jambo baya sana kwa uongozi wa nchi ukichukulia unyeti wa swala lenyewe, umiliki na udhibiti wa mipaka ikiwemo bandari.
Kulamba asali sio dhambi ikiwa huyo mwekezaji anayekuja anaongeza ufanisi na faida kwa maana ya pato la taifa linakwenda kuongezeka maradufu.

Kulamba asali hakuwi ni tatizo iwapo kinachokwenda kufanyika kinakuwa na tija pana ya kiuchumi kwa nchi yetu.
 
Article 23 inazungumzia Duration and Termination. Muda wa Mkataba na Kusitishwa kwake na kimeelezea mazingira ya usitishwaji/ kukoma. Kwangu naona mazingira yote yako sawa na maslahi ya Taifa yamezingatiwa. Wewe shida yako ni nini?
Jioni njema
 
Mazingira ya watu kulamba asali yapo wazi kabisa, na hili ni jambo baya sana kwa uongozi wa nchi ukichukulia unyeti wa swala lenyewe, umiliki na udhibiti wa mipaka ikiwemo bandari.
Very bad indeed.

Ishu hii imewavua nguo kabisa viongozi wa serikali yetu hii ya ajabu.

Rais Samia S. Hassan na Wana CCM wenzake badala wachutame ili kuficha tupu zao, Lakini cha ajabu wanaendelea kukata mbuga hivyo huku wakiwa uchi!

Yaani hawaioni kabisa hatari ya jambo hili na kwamba litawaangusha Kwa kishindo kikuu ajabu.

Ama kweli rushwa hupofusha fikra na ufahamu wa mtu
 
Point ni kwamba tuna viongozi wajinga , ujinga huzalisha hayo mengine ,
 
Sipingi huja ya mbunge lkn Kuna shida nyingine naiona kwa sisi wa bongo.
Hivi mbunge atoke Tanzania hadi Dubai hajui alienda kufanya nn? Hatupo serious kiasi hiki kweli?

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Umesikiliza kuanzia dk ya 7?ninyi ndiyo mkisikia watu wanasema ukweli kuhusu viongozi wa nchi hii huwa mnakimbilia hoja za kijinga kama za kidini na za vyama hamsikilizi mkaelewa yanayotendeka.

Yeye anasema japo hakuambiwa anaenda kufanya nini yeye aliichukua kama nafasi ya kwenda kujifunza zaidi ili aweze kuishauri vizuri serikali pamoja na kuongeza ufahamu ktk yale aliyokuwa anayajua kuhusu bandari.

Hapo ume-comment as if huyo mbunge ni mtu asiyejielewa ili tu aonekane hafai nakwambia huko ccm wangekuwepo kumi (10) kama yeye haya yote yasingetokea.
 
Huyu msukuma itakuwa alitumwa kuwasilisha mada ili muandaliwe kisaikolojia. Vyovyote iwavyo, wame mess up kwenye timing. Wstu watajiuliza, wezi waliohusika ripoti ya CAG wamewekwa pending lakini masuala ya kukodishwa bandari linaletwa kwa dharura.
Mbona hujaandamana?
 
1. Lakini kumbuka pia kuwa uchangiaji hoja ndani ya bunge huwa kati ya dakika 5 hadi 10.

2. Katika hizo, alisema aliyoweza kusema. Na kumbuka pia zile interruptions za kimkakati za wabunge wa CCM na spika wao aliyejigeuza kuwa mwanasheria wa serikali siku hiyo kujibu hoja kinzani.

3. Kwa circumstances hizo, tuseme ndiyo, hakulisema ndani. Sasa kalisema nje ya bunge. Una shida nalo? Mzushi? Kama ni uzushi humo bungeni ndiyo Kuna wasema ukweli? Sio kwamba humo ndo Kuna wazushi halisi kabisa?

Kama watu wanahongwa ili kufanya ujinga na upumbavu huu kwa nchi yao, tuwaiteje watu hawa kama sio wazushi na Wala rushwa bila kujali hadhi zao??
 
Umesikiliza kuanzia dk 7?

Yeye anasema japo hakuambiwa anaenda kufanya nini yeye aliichukua kama nafasi ya kwenda kujifunza zaidi ili aweze kuishauri vizuri serikali pamoja na kuongeza ufahamu ktk yale aliyokuwa anayajua kuhusu bandari.
Exactly.

Lakini cha ajabu, kilichokuwa kinafanyika huko ni mapichapicha yasiyoeleweka na Kila akiuliza alipata majibu yasiyoeleweka.

Honestly, hii ni aibu sana kwa taifa letu, kwamba viongozi wanaojidai walichaguliwa na wananchi wanaweza kuhujumu nchi na taifa lao hivi hivi kwa kuliuza Kwa mataifa ya kigeni.

Hii haikubaliki hata kidogo
 
Ukodishwaji wa bandari itahusisha bandari zote za maziwa, bahari na mito. Mwisho wa mkataba ni mpaka shughuli za.bandari zitakapokoma. Itakuwa wanamaanisha mwisho wa dunia. Kipengele hicho hapo. Kasome mkataba wewe sasa utuambie kama hakipo
Toa ushahidi sio porojo tuu
Mkataba huu hapa.
 

Attachments

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…