battawi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2014
- 2,712
- 2,577
Aida kasema neno muhimu sana ,kuwa taharuki hii inatokana na Hofu tuliyonayo kutokana na uzoefu wa mikataba kadhaa ambayo tumeingi huko nyuma ambayo Watanzania tumepigwa na imeonekana haina maslahi kwa Taifa.
Hoja hi ni ya msingi.sana.
Na m,zee mboe yeye katahadharisha kuwa hili suala ni la Kimuungano, kwa nini bandari za Zanzibar hazimo?
Ukweli ni kuwa Waziri alijibu kuwa Mkataba huu unaihusu bandari ya Dar es salaam tuu.
Ila ikonekana kuna ufanisi tunaweza kungia kwenye mikataba ya nyongeza huko mbeleni .
Ama hili la Kimuungano kuwa Bandari ni za Muungano kweli limo ndani a Katiba, ya 1977. lakini ukweli ni kuwa katiba hii haitumiki tena tanzania, Serikali ya CCM inatuma Akili na uzoefu tuu.
Tazama hapo chini:
_________
NYONGEZA YA KWANZA
_________
(Imetajwa katika ibara ya 4)
Mambo ya Muungano
1. Katiba ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
2. Mambo ya Nchi za Nje.
3. Ulinzi na Usalama.
4. Polisi.
5. Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari.
6. Uraia.
7. Uhamiaji.
8. Mikopo na baiashara ya Nchi za Nje.
9. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
10.Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika,
ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa
nchini Tanzania unaosimamiwa na Idara ya Forodha.
11.Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na
simu.
12.Mambo yote yanayohusika na sarafu na fedha kwa ajili ya
malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki (pamoja
mabenki ya kuweka akiba) na shughuli zote za mabenki;
fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika
na fedha za kigeni.
13.Leseni ya viwanda na takwimu.
14.Elimu ya juu.
15.Maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya
motokaa na mafuata ya aina ya petroli na aina nyinginezo za
mafuta au bidhaa, na gesi asilia.
16.Baraza la Taifa la Mitihani la Tanzania na mambo yote
yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
17.Usafiri na usafirishaji wa anga.
18.Utafiti.
19.Utafiti wa hali ya hewa.
20.Takwimu.
21.Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
22.Uandikishaji wa Vyama vya siasa na Mambo mengine
yanayohusiana navyo.
Article nilizo tia Rangi zina utata mkubwa , CCM wenyewe upande wa ZNZ na Tanganyika hawakubaliani ,
Zanzibar wan baraza lao la Mitiani,
Zanzibar wanakusanya kodi kwa idara yao inayoitwa ZRB(zamani) /(sasa ZRA)
zanzibar wana simamia Bandari yao wenyewe (ZPA) iko chini ya SMZ
Zanzibar inapata shida sana kukopa , ndo maana inataka itolewe kwenye Muungano suala la Mikopo.
Zanzibar imekwama kwa kushindwa kutowa leseni za Viwanda, Kila kiwanda kinapoanzishwa Zanzibar Tanganyika inadai Haki ya Kutoa leseni na Kupata Mrejesho wa Kodi, Kiwanda kinakufa au kufungwa.
Mh.Mbowe hapa ndipo alipolenga na kuonesha Mgogoro tulionao kitaifa.
Ama Upande wa Jamuhuri ya Muungano imeshindwa hadi leo Kufungua Account Ya pamoja ya Muungano ambayo imo ndani ya Katiba.Imeshindwa kutekelezwa na kuisababaishia Zanzibar kukosa stahiki yake katika Mgao wa Muungano.
Hili likoUpande wa Tanganyika nalolimekwama.
Tanganyika lazima Irudi na Zanzibar ipewe mamlaka kamili.