Mkataba wa Bandari: Mbunge Aida Khenani akiri kupelekwa Dubai, lakini mpaka wanarudi hakujua walikwenda kufanya nini

Rostam Azizi ndo number moja kudhoofisha maendeleo ya nchi. Huyu Jamaa alitakiwa asiwepo Tanzania hili nchi iwe salama. Nyuma yake kuna wastaafu wanakaribia kuchungulia kaburi lakini wanafukuzana na pesa ya dunia badala ya kutubu dhambi zao.
 

Attachments

  • IMG-20230621-WA0091.jpg
    62.8 KB · Views: 3
  • IMG-20230621-WA0014.jpg
    70.1 KB · Views: 2
  • VID-20230620-WA0005.mp4
    6.7 MB
  • VID-20230620-WA0008.mp4
    6.8 MB
  • VID-20230620-WA0009.mp4
    19.6 MB
  • VID-20230620-WA0007.mp4
    9.1 MB
Usimuamini Samia

Mimi ni mbobevu wa saikalojia

Samia ni mtu mbaya sana
 
Rostam Azizi ndo number moja kudhoofisha maendeleo ya nchi. Huyu Jamaa alitakiwa asiwepo Tanzania hili nchi iwe salama. Nyuma yake kuna wastaafu wanakaribia kuchungulia kaburi lakini wanafukuzana na pesa ya dunia badala ya kutubu dhambi zao.
Yaaani wewe hufikii hata thumni ya mazuri aliyoifanyia hii nchi Rostam Aziz. Wewe utaishia kuwa mpiga kelele tu
 
Kuna jamaa anaitwa poisonous aliposti kitu pia siku 10 zilizopita. Inafikirisha na kushangaza sana. Anayeweza kusoma asome tafadhali..

Kinachofikirisha sana kwenye hoja ya jamaa huyu aliyiposti humu siku kadhaa nyuma ni;

1. Inawezekana kweli hii kitu ndiyo imetokea humo ndani serikalini. Hii nzuri sana kwa wote wanaotaka mabadiliko maana ni kweli na hakika kuwa, ili kuifyekelea mbali CCM lazima kwanza wapatikane watu toka humohumo watakaokuwa wamechochwa na ujinga na upumbavu kama huu wa Rais Samia Suluhu na DP WORLD wajiunge na harakati...

Na kama kweli hili liko kama alivyolileta poisonous, ujumbe tunaoupata ni kuwa, ufalme wa shetani tayari umeshafitinika, hakuna maelewano na wana CCM walio wengi hawataki huyu mama na Kwa kifupi hawautaki muungano..!!

2. Kwa maoni yangu, japokuwa nyuma ya kundi hili linaweza kuwa lina malengo yake kama ambavyo poisonous anasema, lakini ktk sura nyingine mimi naona uzalendo wa watu hawa wa waliovujisha hii kitu kwa manufaa ya Watanganyika.

Kiufupi mkataba haufai, ni mbaya na Kwa hili Rais Samia Suluhu Hassan hatufai..!!

3. Kwa kuvujishwa Kwa mkataba huu huku TISS wakiwa kimya kumshauri Rais kutoa kauli ya kunyamazisha hii kitu, basi huu ni ushahidi kuwa huyu mama ni jeuri na amedhamiria kutekeleza Nia yake hii ovu dhidi ya Tanganyika huku akilinda maslahi ya Zanzibar nyumbani kwao. Tusikubali..

4. Mwisho poisonous anawalaumu wanaomkosoa Rais Samia Suluhu Hassan na kuupinga mkataba wa DP World juu ya bandari zetu na akasema "wanacheza ngoma wasioijua". Ni wazi poisonous hajui siasa..

Yaani anadhani kama CCM chama kilichomo madarakani serikali yake inafanya madudu na ujinga kama wa mkataba huu wa DP WORLD kiasi cha CCM wao kwa wao kuanza kulaluana na kusalitiana, anategemea CHADEMA au chama kingine kilicho nje ya serikali kianze kufanya kazi wa kuwasuluhisha?

NO WAY BRO!...... Yaani haijalishi wanataka kumpindua Rais wao au kumuua ama vyovyote vile, hiyo kwao ni fursa ya ku - attack na kuwa - weaken zaidi na zaidi..

Kwa sababu Rais Samia anayedhoofishwa na kufanyiwa figisu si ni naye ni CCM vile vile? Hilo genge linalomfanyizia Rais Samia kwani nalo linatoka chama gani eti? Si ni ma - CCM hayo hayo?. Upinzani (CHADEMA) watapambana na yeyote.

Kwa hiyo ndugu poisonous, CHADEMA wanacheza ngoma wanayoijua kuliko unavyoijua wewe!!!
 
Sipingi huja ya mbunge lkn Kuna shida nyingine naiona kwa sisi wa bongo.
Hivi mbunge atoke Tanzania hadi Dubai hajui alienda kufanya nn? Hatupo serious kiasi hiki kweli?

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wakati wanaondoka waliambiwa wanaenda kutembelea dpw kuona utendaji uliotukuka. Walipofika Dubai wakaishia mahotelini wakatanua halafu wakarudishwa. Ndo anashàngaa walienda kufanya nini.
Shopping ndiyo ilikuwa namba moja kwao.
 
Aunt na Dr. M-Push wamemzunguka ,wamelamba V8 na Nyumba ,akaongee nao na yeye apate mgao wake.
 
Ni wakati sasa vyama vya siasa kufanya marekebisho makubwa ya michakato ya mabadiriko ya vigezo na Sifa za wanaogombea nafasi zenye mapana kiuongozi kuanzia Serikali Za Mitaa,Udiwani na ubunge..

Kama taifa Lenye kuhitaji Kwa lazima kusonga mbele kiuchumi hatupaswi kuwa na viongozi Wasio na elimu,Ufahamu na ujuzi wa mambo muhimu ya kulikwamua taifa..

Hakuna watu wa kuogopwa Kama wafanyabiashara wanaoingia ktk siasa ili kupata fulsa Za utajiri na ulinzi wa maslahi Yao..Tunategemea nini?

Nchi yetu ni tajiri sana Sana Sana ..Yatusapa kujitambua na kutambua wajibu wetu wa kutengeneza mifumo,sera na utaratibu wa kunufaisha vizazi vya sasa na vijavyo..
 
Mimi naona katika kila awamu ya bunge ya miaka mitano basi wabunge huwa wanakwenda nje ya nchi kwa mambo mbali mbali. Na wala siyo ajabu kuwa wengine wamekwenda Dubai na wengine kwenda India.
Kwa hili ni ajabu sana kuliko ajabu yenyewe..!

Mlienda kufanya nini miezi takribani nane baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwa ameshasaini MoU na mkataba wenyewe? Kutuzuga siyo?

Kwa hili utetezi wako haufai na hausimami bibie..!
 
Huyu Mbunge kajilipua' na ametusaidia sana kama Taifa. Kwa hili atakumbukwa !

1. Ofisi ya Spika ajibu hoja kwanini kulikuwa na safari bila kueleza lengo lake
2. Kwanini kulikuwa na Wabunge kutoka kamati nyingine? Lengo lilikuwa nini
3. Kwanini hatujasikia maelezo ya wale waliokwenda India, na ni akina nani? Orodha kwanini imefichwa
4. Pesa zimelipwa Dubai, kwa utaratibu wa Bunge ni sawa?
5. Mbunge Kenani alizua Hoja ya kuwa Zabar haipo na Wabunge wa Zanzibar wakasema wana 'Katiba yao'
- Wabunge Wazanzibar walikwenda Dubai na pengine India wakimwakilisha nani?
- Mkataba wa muungano unasema ni jambo la muungano. Sheria ipi ime exclude Zanzibar
-Kama Zbar wana katiba yao , katiba inayotetea Tanganyika na rasilimali zake ipo wapi
-Kwanini Wazanzibar wanashiriki mjadala wa jambo la Tanganyika lisilo wahusu. Mbowe amekosea wapi?
- Kwanini huko kwenye kamati hawakuona Ubaguzi ikiwa Aida alitoa hoja na kujibiwa na Wazanzibar?

Ukimsikiliza Mbunge halafu ukafuatilia Spika Tulia alivyosimamia kujibu hoja na si Waziri mkuu au Mwanasheria mkuu, utaelewa Ofisi ya Spika '' inahusika'' . Kuna harufu, Spika Tulia ajitokeze

Kuna ushahidi kumbe alichoeleza Mh Mbowe tayari kilijadiliwa katika kamati ya Bunge.

Kwa hili Mbowe amesafishwa , hakusema lolote baya, alitahadharisha. Tunajua kumbe wanakwepa hoja kufunika madud. Ukweli unamweka Mh Mbowe HURU

SSH amefaninikiwa kuirudisha Tanganyika na ACT Wazalendo wanakila sababu ya kumfurahia
Swali moja kwa Rais SSH, je, ataumudu kishindo kama Nyerere? Wenye muungano wameamka!

JokaKuu Pascal Mayalla Mag3
 
Kama kuna rushwa aseme, tutamsamehe
OKW BOBAN SUNZU unataka atumie lugha ili uelewe kuwa rushwa imetembea? Kwa maelezo yake;

1. Kwa Tanzania, walilipwa posho zao na kila gharama na TPA Kwa pesa ya Tanzania..

2. Huko Dubai, wakalipwa posho zao na DP WORLD wenyewe ambao kimsingi ndiyo mfalme mwenyewe wa Dubai maana ndiye mmiliki wa kampuni hii kwa 100%...

3. Hakuishia hapo, anasema, walilipwa na kampuni hizi mbili "kwa utaratibu wa Bunge". Mpaka hapa unaelewa nini wewe? ....... Complete contradiction!!

Lakini pia, hebu tujiulize hili:

Inawezekana vipi kampuni inayoomba deal la mkataba mnono kama huu iwachukue waidhinishaji wa tenda hiyo mahali kwa tour huku walilipa gharama zote na posho juu?

Tafsiri yake ni nini? Obviously ni RUSHWA HIYO. Ndiyo maana wengine humo ndani ya bunge walikuwa wanazungumza kama vile wameamushwa toka usingizini au kama watu mazuzu vile kuonesha kuwa hawajui lolote kuhusu hilo jambo!!.

Ndugu OKW BOBAN SUNZU, elewa kuwan aliyesemaga kuwa RUSHWA HUPOFUSHA FIKRA ZA WATU HUSUSANI UKIWA KIONGOZI WA UMMA hakukosea. Ushahidi ni huu..

Na sheria ya maadili ya viongozi wa umma hapa Tanzania kwetu inasemaje eti kuhusu hili?
 
Sheria ya manunuzi ya umma inazuia kutoa tender kwa upendeleo na kwa kushawishiwa na vitu vinavyoashiria rushwa, sijui hawa watu wanadhani hizi sheria zinamhusu nani hasa? maana kwenye hili la bandari ni kama sheria ya manunuzi ya umma imekanyagwa.

Hakuna mahali tender imetangazwa, tunashtukia tu mkataba wa bandari uliosainiwa huku kukiwa na tuhuma za safari ya utalii kwa wanasiasa kwenda dubai na asali ya haja kumwagwa na mwarabu kwa hao wanasiasa njaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…