Mkataba wa Bandari: Mbunge Aida Khenani akiri kupelekwa Dubai, lakini mpaka wanarudi hakujua walikwenda kufanya nini

Wewe ambae hata bandari hupajui, hata biashara ya usafirishaji huijui unapataje nguvu ya kupinga watu wanaoongelea maslahi ya Taifa?

Ukisema kitu ukiulizwa uthibitisho kuonesha umakini wako jibu unachoulizwa
Ukifikia kujibu namna hii, ni dalili tosha kuwa huna au umeshindwa kujibu hoja.
 
Ngoja tuendelee kushaangaana

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Cc. Lord denning & Co
 
Mtu mwongo hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi sembuse ubunge? Wana nkasi mfukuzeni huyo shetani mwongo mchonganishi na adui wa maendeleo yenu na ya inchi
 
"Wapinzani walichelewesha sana Maendeleo" alisikika Mwendazake mara nyingi na mwiho 2019 na 2020 akafanya maajabu ambayo hatukuwahi yaona Tanzania.Faida yake ni hii tutunze kumbukumbu vizuri.
 
Hivi mwanasheria
Mkuu wa serikali mbona haongei chochote sindio wajibu wake huu?
Ndugu@nyembela bado hupati picha tu kuwa huko serikalini mambo si shwari, hawaelewani na wengine wameshazila na kusema, "shauri lake, na apambane na hali yake?"

Ushahidi wa kimazingira unatupa picha kuwa, si tu yeye AG bali ofisi yote ya AG haijui lolote kuhusu mkataba huu Kwa maana ya kwamba haijashirikishwa nao wanashangaa tu kama tunavyoshangaa sisi..!

Huu ni uchafu wa Bunge (Tulia Ackson - Spika wa Bunge na baadhi tu ya wabunge) na ofisi ya Rais wa JMT Bi. Samia Suluhu Hassan..!!
 
Hivi CHADEMA inawabunge? Anyway kwani Tatizo liko wapi hao wabunge kwenda DUBAI? Hii si roho mbaya hii na choyo
 
Hivi CHADEMA inawabunge? Anyway kwani Tatizo liko wapi hao wabunge kwenda DUBAI? Hii si roho mbaya hii na choyo
Unauliza swali kana kwamba hujasoma ulichokikwoti na kumsikiliza muhusika mwenyewe anayetoa maelezo hayo..

Jifunze kusoma na kuelewa hoja za wengine kabla hujamkwoti mtu. Vinginevyo, utakuwa hujui namna ya kuji - engage kwenye mijadala..

Soma, tazama na sikiliza tena hiyo video mwanzo mpaka mwisho. Kisha njoo na hoja specific ili tujadiliane vizuri..

Asante
 
Acha wavurugane mwakani uchaguzi huwenda Mungu anampango wake
 
Kwa hili ni ajabu sana kuliko ajabu yenyewe..!

Mlienda kufanya nini miezi takribani nane baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwa ameshasaini MoU na mkataba wenyewe? Kutuzuga siyo?

Kwa hili utetezi wako haufai na hausimami bibie..!
ajabu ya kusafiri nje ya nchi au ajabu ipi?

Mimi siyo mbunge nilikuwa nakueleza tu kuwa hawa wabunge huwa wanapangiwa safari za nje katika nchi mbali mbali, kama mtu amefika huko bila ya kujua malengo basi itakuwa amelala usingizi.
 
ajabu ya kusafiri nje ya nchi au ajabu ipi?

Mimi siyo mbunge nilikuwa nakueleza tu kuwa hawa wabunge huwa wanapangiwa safari za nje katika nchi mbali mbali, kama mtu amefika huko bila ya kujua malengo basi itakuwa amelala usingizi.
Rudi kwenye hoja yako ya awali niliyoikwoti Kisha linganisha na jibu lako hili☝️☝️

Anyway, acha ni - recall. Nilikuuliza hivi

"Kama ni ishu ya kwenda kuona na kujifunza ili waje washauri serikali kabla ya kuingia makubaliano/mkataba, hiyo mantiki ya lengo la safari hiyo ya wabunge iko wapi maana MoU na mkataba wenyewe ulishasainiwa tayari na Rais na watu wake tangu mwaka 2022 na mkataba umeingia bungeni juzi ukiwa signed already?

Umenielewa?

Kama umenielewa, sasa maswali yangu kwako wewe na kwa kadiri ya akili na ufahamu wako, ni haya;

1. Hiyo wewe unaipa tafsiri gani?

2. Bado unadhani tu kuwa hiyo ilikuwa ni safari ya kawaida tu kwa wabunge kwa kuwa ni kawaida yao kusafiri mara kwa mara kwa shughuli za kibunge siyo?

3. Bado huoni tu kuwa ni safari ya kirushwa rushwa waliyopewa ili waje kutumika ku - rubber stamp maamuzi haya ya hovyo na mabaya ya Rais Samia Suluhu Hassan na wenzake dhidi ya Tanganyika na rasrimali zake ambazo ni urithi wao halali walizopewa na Mungu kupitia hiki kinachoitwa mkataba??

4. Je, unajua kuwa hata wabunge wasio wa kamati husika akiwemo huyu Aida Khenani nao walipelekwa? Unadhani ni kwanini?

MWISHO;

Kama bado huelewi tu, basi utabaki hivyo hivyo na maneno yako ya "si ni kawaida tu kwa wabunge kusafiri nje" bila kutumia kichwa na akili yako sawasawa kufikiria nje ya box..

To cut it short, mimi nakuambia safari zingine za wabunge nje ya nchi na hata za ndani ya nchi huwa si za kawaida bali huwa kama rushwa ya ushawishi kuwalainisha wapitishe jambo fulani la serikali ikiwemo hii tunayojadili. Narudia tena wakati mwingine tuwe tunatumia akili vyema kufikiri nje ya boksi kudadisi mambo..!!...
 
Umejaribu kutoa maoni yako nayaheshimu , lakini kuna jambo la msingi hujaligusia
Kuwa na genge ndani ya Serikali linalofanya uhaini sio jambo la kushabikia, hata mwalimu Nyerere kuna watu walikua wanamfanyia uhaini mpaka ikafikia muda akawaweka detention .

Pili, kuwa mpinzani sio kushabikia serikali iporomoke, bora ushabikie chama kiporomoke kwa maana ya CCM kama wewe ni CHADEMA, lakini Serikali ikiporomoka ama isipoelewana kwa sababu ya uchu wa madaraka wa watu flani , wanaoumia ni ndugu zetu wanaotegemea kutibiwa kwa mkono wa serikali, kusoma kwa mkono wa serikali.


Kuna tofauti kubwa sana kati ya uzalendo wa chama na uzalendo wa nchi, hapa tuko kwenye suala la nchi


Vyama vya upinzani hasa CHADEMA kitendo cha kuwa tayari cheza ngoma yeyote ile ilimradi inadhoofisha nchi sio uzalendo.

Leo hii likitokea taifa la nje linataka kuiondoa madarakani serikali yetu kama URUSI na UKRAINE ilivyo , CHADEMA unataka kusema mko tayari kuungana na taifa hilo imradi serikali ianguke?


Tuwe wazalendo , na tupime madhara ya kucheza ngoma zisizo tuhusu

Lakini umejitahidi ku analyse , kuna maeneo umepatia , except sehemu ya uzalendo kwa nchi
 
Kama hayo anayoyasema ni kweli na sikutaka umaarufu kwa nini akuyasemea bungeni na nafasi ya kuyasema aliipata?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…