Amenisikitisha sana huyo mbunge na hiyo statement yake, yaani hakujua hata malengo ya safari yeye amekurupuka tu kufurahia shopping ya Dubai? Loh!
Labda hujamsikiliza mpaka mwisho...
Rudia tena kumtazama na kumsikiliza Kwa makini...
Tuchukulie Kwa mfano, wewe unapoitwa ghafla na boss wako kisha anakuambia jiandae kwa safari ya kikazi kwenda Kigali Rwanda, utahpji nini at that stage?
Obviously, cha kwanza ni kutii wito. Maswali mengine ya tunakwenda kufanya nini ni baadae huko. Na wengine wanakuambia tu, utajua hukohuko..!!
Hivyo ndivyo alivyofanya huyu mama na kalieleza vyema kabisa.
Shida iko kwa waandaaji wa safari hiyo, yaani bunge Kwa kutumiwa na waziri (serikali). Hawakuwa clear kwenye malengo ya safari hiyo. Hata walipokuwa wanaulizwa huko Kwa "what are doing here specific?", hawakuwa wakitoa majibu...
Na ndugu yangu
bitimkongwe, hivi ndivyo mambo hutendeka katika mfumo wa serikali corrupt kama ya kwetu na hiyo ya Dubai...!!
Na wewe hujiulizi, hiyo timu nyingine ya wabunge walioenda India walikwenda kufanya nini? Si waliambiwa tu nyie nendeni mkafanyie shopping yenu huko na mambo yatakuwa hivi???
Unataka usikie nini zaidi tena ili utambue kuwa jambo hili limegubikwa na giza la rushwa tupu?
Kwa hili la mkataba DP WORLD, Rais Samia Suluhu Hassan katukosea sana Watanganyika..!!