Mkataba wa Bandari: Mbunge Aida Khenani akiri kupelekwa Dubai, lakini mpaka wanarudi hakujua walikwenda kufanya nini

Mkataba wa Bandari: Mbunge Aida Khenani akiri kupelekwa Dubai, lakini mpaka wanarudi hakujua walikwenda kufanya nini

Kwani ni jukumu la mkataba kuhakikisha ulinzi wa vitisho dhidi ya ugaidi?

Tangu lini masuala ya ulinzi wa nchi yetu yakawekwa kwenye mikataba ya uwekezaji au ushirikiano wa uwekezaji?

Masuala ya Ulinzi wa nchi yetu yanasimamiwa na vyombo vyetu vya ulinzi wa usalama na hakuna popote pale mwekezaji amewahi kupewa kazi ya kushughulikia masuala ya ulinzi na usalama wa nchi yetu.

Una lingine?
Wewe mpuuzi umewahi kufika loliondo? Kule mlikomuuzia mwarabu? Mpaka cm zinasema karibu falme za kiarabu ndani ya Tanzania unafikiri unaweza kuingia kama unavyoingia chooni kwako? Mnauza uridhi wa vizazi alafu unajiona msomi huko shule ndivyo mlivyoenda kusomea kuuza nchi?
 
Siasa za majitaka na kujitafutia umaarufu tu!! Kama ilikuwa hivyo kwa nini hakusema hayo wakati alipata nafasi ya kuchangia bungeni kuhusu huu mkataba?

Alipata nafasi ya kuchangia akaishia kumtetea Mbowe na kuweka clip ya Mbowe tuseme hili halikuwa na umuhimu wa kulisema bungeni wakati ana kinga anapoongea?

Hizi kisheria tunaziita after thought. Anajitafutia umaarufu tu
Kuna shida gani kutafuta umaarufu kusema ukweli? Usilamishe aseme lini ukweli wake. Kaamua kusema leo mbele ya waandishi wa habari kuliko bungeni kwa wahuni.
 
Ila mheshimiwa Angekuwa amefanya vizuri kama angetusanua kabla ya kwenda Dubai.
 
Sheria ya manunuzi ya umma inazuia kutoa tender kwa upendeleo na kwa kushawishiwa na vitu vinavyoashiria rushwa, sijui hawa watu wanadhani hizi sheria zinamhusu nani hasa? maana kwenye hili la bandari ni kama sheria ya manunuzi ya umma imekanyagwa.

Hakuna mahali tender imetangazwa, tunashtukia tu mkataba wa bandari uliosainiwa huku kukiwa na tuhuma za safari ya utalii kwa wanasiasa kwenda dubai na asali ya haja kumwagwa na mwarabu kwa hao wanasiasa njaa.
PPRA wanasemaje?
 
Sipingi huja ya mbunge lkn Kuna shida nyingine naiona kwa sisi wa bongo.
Hivi mbunge atoke Tanzania hadi Dubai hajui alienda kufanya nn? Hatupo serious kiasi hiki kweli?

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Nami ninashangaa kidogo kwa wewe kuuliza swali kama hilo.

Hivi kweli wewe uliona u'seriousness' wa aina yoyote mule ndani ya Bunge; ukianzia kwa Speaker mwenyewe na hata Mawaziri, akina Nnauye waliochangia?

Hebu jaribu kuwa mkweli wa nafsi yako mwenyewe juu ya hili, badala ya kuhoji umakini wa mbunge, tena aliyepewa fursa tu ya kwenda matembezi nje ya nchi.

Katika hali ya kawaida, hivi kweli pasingekuwepo na maandalizi ya kina sana kwa hao wabunge kabla ya safari yao hiyo?
Kuna mbunge yeyote, aliyeeleza ni kwa namna gani waliandaliwa kabla ya safari yao muhimu kama hii? Walipewa seminar yoyote juu ya watakayotarajia kuyaona katika hiyo safari?
 
Ila mheshimiwa Angekuwa amefanya vizuri kama angetusanua kabla ya kwenda Dubai.
Angesanua vipi na hakukua serikali imeingia mkataba na Dubai? Wao wanaenda ziara nyingi nje ya nchi, hivyo hakuona shida
 
Kama ni kweli serikali imekosea sana,au ndio maana waziri Mkuu kapooza sana , pengine na yeye alizungukwa?

Mbunge Musukuma hili suala limemuacha uchi sana,ujinga wa viherehere kwa mambo mazito,kwa sasa simsikii tena,kaona haya ni maji marefu "kwerikweri " in MAGUFULI VOICE
Na kwanza safari yenyewe ilikuwa ya ghafla tu maana alikuwa jimboni kwake...

Ghafla akapigiwa simu ajiandae kwa safari kwenda Dubai..

Baada ya muda kidogo akapata barua rasmi ya bunge kumtaka kujiandaa kwenda huko..

Mpaka hapo alikuwa hajui lengo la safari hiyo ni nini specific ukiondoa statement ya jumla jumla tu ya kuwa "wanakwenda kujifunza"

Posho zao za safari kwanza walilipwa na TPA Kwa pesa za kitanzania na huko Dubai wakalipwa na Dubai Ports World Kwa pesa ya huko... Lakini cha ajabu na cha kushangaza mbunge anasema "Kwa kufuata utaratibu wa malipo ya bunge".

Swali kubwa ni hili:
Hivi TPA na DUBAI PORT WORLD ambao ndiyo wanataka washauriwe na bunge juu ya mkataba wao wanawezaje kufadhili safari kama hiyo wabunge kwa jambo lao ambalo wabunge ndio wanapaswa kulipitia waone ni zuri linafaa au baya halifai Kwa maslahi ya taifa?

JIBU NI RAHISI SANA HAPA: Hiyo ni rushwa, wabunge wamehongwa ili wakubali mkataba huu mchafu, mbaya na hatari Kwa nchi yetu...!

Kwa hili, Rais Samia Suluhu Hassan katukosea sana Watanganyika. Aombe radhi na aachane na kitu hiki. Kama amepewa hongo, arudishe vitu vya watu alivyochukua. Watanganyika tumekataa...!

Bunge lipo uchi wa mnyama. Serikali imejaa rushwa. mbuzi wamekula mkeka.
 
Kama ni kweli serikali imekosea sana,au ndio maana waziri Mkuu kapooza sana , pengine na yeye alizungukwa?

Mbunge Musukuma hili suala limemuacha uchi sana,ujinga wa viherehere kwa mambo mazito,kwa sasa simsikii tena,kaona haya ni maji marefu "kwerikweri " in MAGUFULI VOICE
Hujamuelewa msukuma,hizo ni political game na ame-win ....umeona wakisema tena maneno ya GANG ??

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mnafiki mkubwa, muongo mzandiki, hivi kweli utoke hapa upelekwe hadi dubai hujui unaenda kufanya nini?, kawadanganye huko huko nkasi sio kutuletea uharo hapa,
Wewe pinga kwa kuwa ni haki yako, ila usitudanganye eti ulikuwa hujui unaendea nini? Tapeli mkubwa mla rushwa mkubwa kwadanganye washamba wenzako huko
Na pengine uhamiaji wakuchunguze na wasiwasi si mtanzania wewe, kwa nini unatetea wakenya kwa juhudi hivi ?
 
Hakika shetani ana trick za ajabu sana anapotaka kutenda au anapotenda uovu wake kwa kuwatumia watu waovu hususani viongozi wenye dhamana kubwa za kuongoza nchi na wananchi wa nchi yetu..

Hebu twende pamoja, soma na sikiliza hii👇👇👇

Mkataba wa DP WORLD ni zaidi ya mkataba tu!

• Kumbe kulikuwa na timu mbili za wabunge. Moja ilienda India (kuzuga tu) na nyingine Dubai (kuliko na mpango mzima wa Rais Samia Suluhu Hassan na Prof. Makame Mnyaa Mbarawa). Aida Khenani yeye akapachikwa kwenye trip hii ya Dubai. Nadhani lengo likiwa ili waovu hawa waje kuwa na hoja kusema "hata CHADEMA walikwenda kule wakiwakilishwa na mbunge wao kuona uzuri wa uwekezaji wa kampuni hii..!!". Aidha bila shaka pia kuwa, ili wamtumie ndani ya bunge kuwa kama shahidi wa upande wa upinzani bunge litakapo - ratify mkataba huu. Kwenda kinyume, Spika Dr Tulia Ackson alionekana kushangaa na kupaniki kikatokea tulichokiona. Mpaka naibu Spika wa Spika ndugu Zungu naye akiwa kama back bencher, alisimama eti kumpa taarifa mbunge huyu!!

• Hauishia hapo, mbunge huyu ndani ya bunge akaendelea kuwashangaza wabunge wa CCM aliposema hakubaliani na mambo haya hadharani ndani ya bunge. Nadhani kimya kimya wakawa wanasonya amekula hela zetu bure huyu. Wakamzonga zonga mpaka akaipata fresh huku Spika Tulia Ackson akiwa amevaa koti la mwanasheria Mkuu wa serikali kujibizana naye, kumtoa hofu😂 na kumshawishi akubaliane na serikali..!

Haya ya Spika Tulia Ackson siku ile kiukweli yalikuwa ni kichekecho na upuuzi wa ajabu sana.. Ama kweli, rushwa hupofusha fikra na ufahamu wa mtu!!

• Walioenda India ripoti yao wala hata haihitajiki kwa sababu wahusika sio wahindi wa India bali ni waarabu wa Dubai ambako kabla huyu anayechaguzwa na kauli ya "nani kama mama" alishatangulia kabla kumalizana na "mfalme" na kuchukua chake mapemaaaa..!

• Hii haina shaka tena kuwa, nyuma ya mkataba huu kati ya DP World & Serikali ya Tanzania kuna rushwa kubwa imetembea kwa viongozi wetu.

• Hata hivyo mimi siamini kabisa kuwa huyu mama anaweza kuwa mbaya na mumiani wa kiwango hiki cha kufikia kuuza kipande cha nchi ya Tanganyika.

Maoni yangu binafsi

Ilisemwa na wahenga, ili nchi yoyote duniani ipate maendeleo ya kweli ya watu wake, lazima mambo haya manne yawepo katika ufanisi wake:

1. Ardhi
2. Watu
3. Siasa safi
4. Uongozi bora

Ukiyatazama hayo mambo na ukimsikiliza huyu mbunge ambaye kwa kweli ukimtazama usoni mwake na kile kitokacho kinywani mwake, hutapata shida kabisa kumwamini.

Ukiachilia mbali uwepo wa ardhi na rasrimali watu, Tanzania tunakabiliwa na tatizo moja kubwa la UKOSEFU WA SIASA SAFI ambayo imezaa tatizo la UKOSEFU WA UONGOZI BORA. Na matokeo yake ni haya tunayoshuhudia leo. Tunaulizanaga, hivi ni kwanini nchi yetu ni masikini hata baada ya miaka zaidi ya 60 ya uhuru? Jibu lake liko wazi sasa... Ukosefu wa uongozi bora wa nchi..!!

Laiti tungekuwa na hayo mambo mawili muhimu zaidi, hiki kinachoendelea sasa kati ya Tanzania na DP World, kisingekuwepo maana tungekuwa na viongozi walio madarakani wenye akili, ufahamu, hekima na busara na kujitambua.

Lakini kwa mkataba huu wa DP WORLD, inadhihirisha wazi sasa kuwa kumbe tuna viongozi wajinga, wasio wazalendo wa taifa lao, waliojaa tamaa ya kujilimbikiza mali kwa rushwa na kuwa tayari kujiuza kwa vipande vya fedha, wabinafsi, wala rushwa na wanaojipenda wenyewe na matumbo yao na hawa kamwe hawajawahi kutupenda sisi wananchi wa Tanzania..!!

Sara yetu wote ni:

Mungu wetu uliye juu mbinguni muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo tutie nguvu tupambane na hawa mumiani wanajiita viongozi wa nchi ya Tanganyika lakini kumbe ni mashetani katika sura za binadamu.. Amina

Rais Samia Suluhu Hassan katukosea sana Watanganyika kwa hili la mkataba wa DP WORLD kumuuzia bandari zetu zote za bahari na maziwa ya Tanganyika huku akiacha za kwao Zanzibar mikononi mwa Wazanzibari!
Hii ni rushua tu
TAKUKURU mpo?
 
Ubatili wake uko wapi?
Una kazi ndugu kumpinga kila mtu juzi ukaanzisha uzi ukimkosoa lissu.
Kwenye huu uzi kila anayepinga issue ya bandari unamkosoa sijui mwenzetu umelipwa shilingi ngapi.
Labda nikuchangamshe bichwa lako ulishwawahi kusikia kuwepo zabuni shindani ya kusimamia bandari hadi hiyo DPW ikapatikana
 
Ila mheshimiwa Angekuwa amefanya vizuri kama angetusanua kabla ya kwenda Dubai.
Angesanua vipi na hakukua serikali imeingia mkataba na Dubai? Wao wanaenda ziara nyingi nje ya nchi, hivyo hakuona shida
Ila kabla ya safari si wanaambiwa sababu ya safari?
 
Hata mimi ningeenda bila kujiuliza mara mbili, begi langu huyoooooo 😁 😁 😁 😁 , tatizo lipo kama wabunge WOTE walienda huku wakiwa hawajui wameenda kufanya nini...lol
 
Wazanzibari 3 wameshirikiana kutumia madaraka yao hapa Tanganyika kuiuza bandari yetu, hili hatutalikubali, watanganyika tuamke, ni kheri uwe na shamba linalotoa gunia 6 za mahindi lakini libakie kuwa la kwako kuliko kuliuza kisha uwe unapewa gunia 12, huo utakuwa ni ujinga.
 
Hata mimi ningeenda bila kujiuliza mara mbili, begi langu huyoooooo 😁 😁 😁 😁 , tatizo lipo kama wabunge WOTE walienda huku wakiwa hawajui wameenda kufanya nini...lol
wabunge walioiba kura wana uchungu gani na Tanganyika ndugu.
 
Mbunge wa Nkasi ameviambia vyombo vya habari Mwanasheria mkuu wa Serikali hadi MKATABA wa milele wa bandari ya Tanganyika na waarabu unaletwa bungeni kesho yake hakuwa na taarifa.

"...hilo jambo lililetwa kwa uharaka wa ajabu na nikuhakikishie ndugu WAANDISHI hadi jioni ya kuamkia kesho ya MKATABA ule kuletwa bungeni AG hakuwa na taarifa yeyote!"

Mbunge Aida Khenani.
Aisee, ndio maana Samia anajificha kwa aibu tu.
 
Back
Top Bottom